KERO Mkurugenzi Manispaa ya Moshi awalazimisha watumishi kufyeka na kusafisha makaburi ya Karanga siku za mapumziko

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
May 31, 2024
Posts
42
Reaction score
38
Kichwa hapo juu cha husika, huyu Mkurugenzi tangu Jumamosi iliyopita aliwaamuru watumishi hasa walimu kuchukua mafyekeo na majembe kwa amri na vitisho kwenda kusafisha makaburi siku ambayo si ya kazi.

Leo tena Ijumaa ametoa vitisho kupitia kwa Walimu Wakuu kuwa asijekwenda kusafisha makaburi kesho tarehe moja asubuhi na mapema akiwa na jembe au fyekeo asimlaumu mtu kwa kitakacho mkuta. Sasa sisi kama watumishi tunahoji je hii ni haki? Manyanyaso haya yataisha lini kwetu?

Je, tusipoenda na ukizingatia ni siku ambayo si ya kazi hatua zitakazochukuliwa dhidi yetu si ni maonezi?

IMG-20240531-WA0004.jpg
 
Katiba mpya ndio suluhisho, wakurugenzi wa halmashauri na manispaa ni kero kubwa Kwa watumishi wa umma
 
Si ni jimamosi ya usafi hiyo?
Tumesafisha jumamosi iliyopita akasema tumefika wachache anataka turudie jumamosi ya kesho pia mkuu. Je? Hata kama ni jumamosi ya usafi ni utaratibu watumishi kwenda kusafisha makaburi bila kujali nauli tunapata wapi? Yaani ni amri saa 12 ufike bila kujali umbali unaotokea hii ni haki kweli?
 
Yan ndiyo kiongozi kafikiri hapo hadi mwisho? Watumishi kazi wanayo. Aje atuambie sisi bodaboda ambao hatuna D mbili atapata majibu.
Mimi nilishawahi kushauri kiundwe chama cha wasio na ajira rasmi wenye uchungu ile hawa waramba asali waondolewe hawana uchungu na rasilimali watu au rasilimali zetu
 
Katiba mpya ndio suluhisho, wakurugenzi wa halmashauri na manispaa ni kero kubwa Kwa watumishi wa umma
Kazi yao ni kunyanyasa watumishi na kukamua kodi za akina mama wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwaacha wafanyabiashara wakubwa wakitorosha rasilimali za Taifa
 
Viongozi wengi hasa wale wa kuteuliwa hawana uwezo wa kuongoza. Not at all "visionary leader ". Utamlazimishaje mfanyakazi afanye kitu ambacho hakipo kwenye mkataba? Shame on you!
 
Na ukiuliza unatishiwa kufukuzwa kazi afu uhamishwe kwenda mazingira magumu ya kazi
 
Back
Top Bottom