Mkurugenzi manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe atemwa. Ni yule aliyemnyima Greda mbunge Ibrahim Shayo

Mkurugenzi manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe atemwa. Ni yule aliyemnyima Greda mbunge Ibrahim Shayo

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa alifanya ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro.

Pamoja na mambo mengine Nchengerwa alizungumza na watumishi wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Moshi.

Moja ya jambo alilokemea ni kuwepo na mvutano baina ya mkurugenzi wa manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe (kwa wakati huo) na mbunge wa Jimbo la Moshi mjini,Ibrahim Shayo.

Mchengerwa akasema mbunge kama mwakirishi wa wananchi anaowajibu wa kuwatumikia wananchi.

Akaibua jambo lililofichika la Mbunge kunyimwa Greda na mkurugenzi huyo ambalo ilikuwa alitumie kuzifanyia ukarabati barabara za pembezoni mwa mji ambako wananchi kwa muda mrefu walikuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hizo.

"Umekuwa na mgogoro na mbunge aliyekuwepo, hivi wewe una uhakika utakaa hapa (Manispaa ya Moshi) miaka mitano? akahoji Mchengerwa.

Sasa alichohoji Mchengerwa kimetimia na hatimaye katika uteuzi uliofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan umemtupa nje Mkurugenzi huyo na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Upendo Eric Mangali (pichani chini ).

IMG-20260929-WA0263.jpg


Kwa faida ya wasomaji wetu naomba sasa umsikilize Waziri Nchengerwa alichokisema



Soma pia:

 
nimepuuzia hiyo clip ya Nchengerwa, tatizo la viongozi wengi ni kutaka kuonekana miungu watu. hili tukio linafanana like la baba levo na afisa wa TRA

Muhimu watu waendelee kukwepa kulipa KODI Kwa maslahi Binafsi.
 
Back
Top Bottom