DOKEZO Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mjini inanuka rushwa, ichunguzwe!

DOKEZO Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mjini inanuka rushwa, ichunguzwe!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Napoandika hii post leo, na siku za karibuni Waziri Mkuu amekuwa ziarani Mkoa wa Kilimanjaro, naomba na kumsihi Waziri Mkuu aifanyie uchunguzi Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mjini, mipango miji na TARURA kwa kula rushwa na kuuza maneno ya wazi au kuwezesha maneno ya wazi kuuzwa kwa watu binafsi.

Hizi kesi zimekuwa common sana siku za karibuni kwenye jamii, na viongozi wahusika wamekuwa wanalipuuzia na kulifumbia macho baada ya kupokea rushwa.

Kata niliyopo kuna mfanyabiashara anaitwa Mawalla amekuwa kwenye mgogoro na wananchi kwa takribani miaka 3 sasa na kuanzia Serikali za Mtaa mpaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa wamekuwa wakimpa kinga huyu bwana, malalamiko ya wananchi yamekuwa yakigongamwamba kwasababu ya viongozi haswa wa Manispaa ya Moshi Mjini kukejeri na kupuuzia malalamiko ya wananchi.

Namuomba Waziri Mkuu na Ofisi yake wachukue hatua juu ya kero hii, Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mjini imekuwa doa kwa kukithiri na kuongozwa na rushwa.

Soma pia: DOKEZO - Ofisi za Ardhi Moshi Mjini Zadaiwa Kula Milioni 15 Ili Kufanikisha Uporaji wa Eneo la Umma
 
Back
Top Bottom