Mkurugenzi mkuu mwingine ajiuzulu Vodacom. Mtandao unaelekea shimoni?

Mkurugenzi mkuu mwingine ajiuzulu Vodacom. Mtandao unaelekea shimoni?

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose amejiuzulu nafasi hiyo ambapo atatizimiza miezi nane tangu mtangulizi wake, Hisham Hendi nae ajiuzulu kwenye nafasi hiyo. Sio ishara njema kwa kampuni kubwa kama Vodacom ambayo watu wanaota kuiongoza.

Mwaka jana Vodacom ilisitisha mkataba wake na TFF kufadhili ligi kuu Tanzania bara kwa kigezo ya hali mbaya ya kiuchumi inayoikumba kampuni hiyo.

Mwaka 2019 tycoon wa biashara bongo, Rostam Aziz aliuza hisa zake zote Vodacom. Mwaka huu kanunua Tigo/Zantel.

Vodacom imekuwa ikipoteza kiwango cha soko(market share) kadri siku zinavyokwenda ambalo sasa limefika 29.4% kutoka 45% miaka kumi iliyopita.

Nini kinaikumba kampuni ya Vodacom pamoja na uzoefu wake kwenye sekta ya mawasiliano Tanzania anaangukia pua?

Vodacom.jpg
 
Back
Top Bottom