Mkurugenzi mkuu mwingine ajiuzulu Vodacom. Mtandao unaelekea shimoni?

Image_1652197682.jpg
 
Voda walibebwa sana na mapato ya m-pesa ila baada ya serikali kuweka tozo kwenye miamala matumizi ya m-pesa yameporomoka kwa speed ya mwanga
 
Ajiuzulu si ameshiba, mtaani watu kibao wanatamani nafasi hio
 
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose amejiuzulu nafasi hiyo ambapo atatizimiza miezi nane tangu mtangulizi wake, Hisham Hendi nae ajiuzulu kwenye nafasi hiyo. Sio ishara njema kwa kampuni kubwa kama Vodacom ambayo watu wanaota kuiongoza.

Mwaka jana Vodacom ilisitisha mkataba wake na TFF kufadhili ligi kuu Tanzania bara kwa kigezo ya hali mbaya ya kiuchumi inayoikumba kampuni hiyo.

Mwaka 2019 tycoon wa biashara bongo, Rostam Aziz aliuza hisa zake zote Vodacom. Mwaka huu kanunua Tigo/Zantel.

Vodacom imekuwa ikipoteza kiwango cha soko(market share) kadri siku zinavyokwenda ambalo sasa limefika 29.4% kutoka 45% miaka kumi iliyopita.

Nini kinaikumba kampuni ya Vodacom pamoja na uzoefu wake kwenye sekta ya mawasiliano Tanzania anaangukia pua?

Kampuni ya CCM hiyo.Rostam alijimilikisha hisa za chama vofacom mwendazake akamtight kwenye uhakiki na wamali za chama pamoja na channel ten ndio maana alijifanya anauza hisa zake kumbe anarudisha kwa wenyewe.
 
Hii movie mpya ya Tigo inaeleweka? Kuna wakati waswahili wanasema bora lawama kuliko fedheha.
Hivi nani anaangalia ethical part ya businesses na businessmen wa Tanzania? Kuna wakati ni ngumu sana for a proper corporate entity to fight the companies that don't have the words " business conduct" in their agenda
 
Kampuni ya CCM hiyo.Rostam alijimilikisha hisa za chama vofacom mwendazake akamtight kwenye uhakiki na wamali za chama pamoja na channel ten ndio maana alijifanya anauza hisa zake kumbe anarudisha kwa wenyewe.
Vodacom ni kampuni ya makaburu,acha uwongo uwongo na magu wako
 
Vodacom ndo mtandao naotumia na hakuna kizuri kisichosemwa
 
Back
Top Bottom