Mkurugenzi mkuu mwingine ajiuzulu Vodacom. Mtandao unaelekea shimoni?

Mkurugenzi mkuu mwingine ajiuzulu Vodacom. Mtandao unaelekea shimoni?

Duuh vodacom sitaisahau maana kipindi hicho inakuja ndio ujana nao ulikua unashika kasi kama moto kwenye nyika.

I miss those old good days.
 
Walionunua Hisa za Voda wanaenda kuwa masikini wa kutupa, watakula hasara, pia Hisa zao haziuuziki
Kuna jamaa nilimpa angalizo kwenye hizi hisa
Nilimwambia ingekuwa ni voda wenyewe wameingia kwenye hili soko sawa ila kwa kusukumiziwa huko na wamiliki wake wanajulikana sarakasi zao mda tu ndio utakaoongea
 
Ilipelekwa kule .. . Sasa inarudishwa kwa wenyewe.. ... Mkorofi keshaondoka zake.
 
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose amejiuzulu nafasi hiyo ambapo atatizimiza miezi nane tangu mtangulizi wake, Hisham Hendi nae ajiuzulu kwenye nafasi hiyo. Sio ishara njema kwa kampuni kubwa kama Vodacom ambayo watu wanaota kuiongoza.

Mwaka jana Vodacom ilisitisha mkataba wake na TFF kufadhili ligi kuu Tanzania bara kwa kigezo ya hali mbaya ya kiuchumi inayoikumba kampuni hiyo.

Mwaka 2019 tycoon wa biashara bongo, Rostam Aziz aliuza hisa zake zote Vodacom. Mwaka huu kanunua Tigo/Zantel.

Vodacom imekuwa ikipoteza kiwango cha soko(market share) kadri siku zinavyokwenda ambalo sasa limefika 29.4% kutoka 45% miaka kumi iliyopita.

Nini kinaikumba kampuni ya Vodacom pamoja na uzoefu wake kwenye sekta ya mawasiliano Tanzania anaangukia pua?

Huu mtandao binafsi nimeshaacha kuutumia
 
Back
Top Bottom