Tanzania Railways Corp
Govt Institution
- Mar 23, 2018
- 292
- 690
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Salim Ramadhani Msangi akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Shirika la Reli Tanzania alipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya biashara (Sabasaba) katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Bwana Msangi amesema kuwa “reli ni Sekta iliyokua kwa kasi hivi karibuni, wengi walizoea kuiona treni ya zamani (MGR) lakini sasa hivi ukiangalia maendeleo yaliyopo mtu hawezi kuamini, haya ni maendeleo makubwa tunatakiwa tujivunie”.
TRC inaendelea na maonesho hayo ya kimataifa kuonesha miradi na huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya usafiri wa reli nchini