Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mwendokasi analipwa zaidi ya milioni kumi kwa mwezi; hajawahi hata kutembelea abiria aone kero zao

Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mwendokasi analipwa zaidi ya milioni kumi kwa mwezi; hajawahi hata kutembelea abiria aone kero zao

Mwendokasi wenyewe walishakuja hapo JF kuomba ushauri na GT wa JF wakawapa nondo za kutosha lakini hakuna hata moja lililotekelezwa. Kwa kifupi ni sikio la kufa magari yanazidi kupungua barabarani hakuna magari mapya yaliyoinginzwa na yaliyoharibika yamejazana Ubungo na Gerezani.
Hao waliotoa maoni na mapendekezo wapewe vitengo hapo DART ili wafanye vitendo.
 
Hao waliotoa maoni na mapendekezo wapewe vitengo hapo DART ili wafanye vitendo.
Unamtisha nani? Watangaze kazi wafanye usaili wa haki. Watanzania watajitokeza. Na wanaofaa watapatikana. Watanzania wako nje ya nchi kwenye nafasi kubwa na wanafanya kazi katka viwango vya kimataifa.Wameshika nafasi hizo kipitia usaili wa haki siyo usaili wa wa maigizo. Fanya utafiti.
 
Hapo akiulizwa ana mabasi mangapi jumla yanayofanya kazi hajui!!!
 
Hii miradi inavurugwa makusudi, Nia ni kutaka ionekane haina ufanisi baadae wajigawiye.
 
Nilipojiuliza ikiwa Dangote anatumia mitungi ya gesi kwenye magari yake kupunguza gharama,
Na ni Mtu mgeni nchini kwetu sisi wazawa tunashundwaje

Hatuna Hela au wasomi wakufanya hivyo vitu hamna au ni ulimbukeni Wa akili au Kuna watu wanapika Hela kwenye mwendokasi

Maana gesi ipo kupunguza gharama za uendeshaji. Kwa bahati mbaya, uongozi wetu unaweza kuonekana kutokuwa na ubunifu na kuathiri maendeleo.

. Hii inaweza kuwa ni ishara ya kutokuwa na kipaumbele kwa mifumo endelevu. Viongozi wetu wanaweza kuonekana kama hawapendelei mabadiliko na wanajifanya wasomi, jambo ambalo linaweza kuzuia maendeleo yetu.

Ninaamini kuwa na rasilimali nyingi, Tanzania inaweza kufikia maendeleo makubwa zaidi. Hata hivyo, inaonekana tumekuwa nyuma kimaendeleo na kuwa wa mwisho katika uchumi. Ni wakati wa kuchukua hatua na kuonyesha ubunifu katika matumizi ya rasilimali zetu.

Nina imani kubwa kwamba kufunga mitambo ya gesi kwenye mwendokasi kunaweza kuleta mabadiliko chanya. Kwa kufanya hivyo, gari zinaweza kupita kila baada ya dakika 10, ikipunguza msongamano na kuboresha ufanisi. Tunahitaji kujitambua na kufanya maamuzi yatakayosaidia maendeleo, bila kufumbia macho changamoto zinazotukabili.
 
Back
Top Bottom