Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande asema pamoja na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Nyerere, watanzania tutegemee migao zaidi!

South Africa TU na uchumi wao mkubwa.
Kwa uzalishaji umeme niya 20 kidunia,
Na ya kwanza bara zima la Africa ila hata hizo megawatt 60,000 hawajafikisha.

Nchi nzima Wanazalisha megawatt 58,095
Itakua sisi uku ulimwengu wa tatu?[emoji848]

Bw.maharage arudi TU kwny ving'amuzi,
Haya mambo ya umeme Ni mweupe kabisa
 
Huyu maharage sijui kala maharagwe ya wapi. Namshauri arudi dstv akaendee kuuza ving'amuzi
Shida ni madaraka makubwa aliyopewa Rais ndani ya Katiba yetu, bila hata kuhojiwa, ni vigezo gani ametumia katika uteuzi wake!

Tukumbuke kuwa Rais Samia, ndiye aliyemteua Maharage Chande, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO.

Bila Katiba mpya, itakayompunguzia madaraka makubwa ya ki-mungu mtu, Rais wetu, basi tutegemee, nchi yetu itaendelea kuwa masikini wa kutupa, Hadi mwisho wa Dunia hii😎
 
Ukweli lazima usemwe, nchi inaendelea kwa kasi sana, Megawatt 5000,haziwezi kutosha,, tunahitaji Gigawatt, sio megawatt
 
Hawaoni Africa kusini, walijisahau kuweka long term plan za kuzalisha umeme, sasa wana mgao hatari, ndo wanakurupuka kuanzisha nuclear power plants
 
Yote hayo ni maandalizi kuleta mskampuni binafsi ya kipigaji aina ya iptl na yale mengine yaliyozalisha umeme kwa gesi aliyoyatimua jpm. Njia nzuri ni uwekezaji wa umma mradi udhibitiwe vizuri gharama za ujenzi. Wahuni walioko sasa lao ni kutafuta miradi ambayo watapiga hela ya umma.
Lengo liwe kushusha bei ya umeme kwa mteja kufikia viwango vya ulaya na marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…