Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Una hoja lakini mifano unayotoa bado ni irrelevant! Muuza machungwa vitu vyake vipo open kila mtu ataona kuwa yule ana machungwa ana ndoo ya maji ana kisu na kadhalika lakini mwenye bastola yake kwa ajili ya ulinzi binafsi hakuna anayeweza kuiona kirahisi ndo maana nikasema atakayempora afanye uhalifu basi alimplania sana au lao mojaWale wanaakili timamu, wanajua ni mambo ambayo yamewahi kutokea
Muuza machungwa kaingia na machungwa yake bar then ugomvi umetokea mtu kawahi beseni la machungwa kachukua kisu kamchoma mwenzake kafa
Ujue sikia nikwambie kaka blaza, bastola ni kwa ajili ya ulinzi binafsi na mtu mpaka kufika nayo kwenye check point maana yake ana uhakika amekidhi hatua zote za kuwa nayo. Kumnyang'anya aingiapo kwenye treni ndani ni kuhatarisha usalama wake kwa sababu kwenye treni watu ni wengi na hivyo kunafanya sehemu hiyo iwe ni more vulnerable kwake yeye
Kwingine kote mmemuamini lakini hapa tu ndo mmeona ni hatari basi bora msingemruhusu kabisa kumiliki chuma. Nasema haya lakini sijui sheria ikoje hebu wataalamu watusaidie hivi kwa mtu (mfano wale wafanyabishara wakubwa wakubwa) akiwa anamiliki silaha kwa ajili ya ulinzi binafsi ni maeneo gani haruhusiwi kuwa nayo? Maana tumezoea tu kwenye mikutano ya kitaifa!