Mkurugenzi Mtendaji TANESCO aelezea hali ya maji Mtera na Kidatu

Mkurugenzi Mtendaji TANESCO aelezea hali ya maji Mtera na Kidatu

March 12, 2020
Kilombero, Morogoro
Tanzania

Mabwawa ya Mtera na Kidatu ya kuzalisha umeme yazidiwa nguvu na maji

Wananchi waombwa kuhama toka maeneo yao yaliyo karibu na Mto Ruaha Mkuu (Great Ruaha River). Hii inatokana na mvua nyingi kupita kiasi zinazonyesha ktk maeneo yanayotiririsha maji katika mto Ruaha alisema mkuu wa wilaya ya Kilombero alipokutana na wananchi wa Kilombero.



Mkuu wa wilaya ya Kilombero amewataka wananchi kuhama kutoka maeneo hayo hatarishi yaliyoko katika mkondo wa mto huo mkubwa mkoani Morogoro.
Source: ITV Tanzania
 
March 9, 2020
Morogoro

Mto Ruaha / Kilombero Morogoro, Tanzania hali ya maji / mto kufurika baada ya mvua nyingi kunyesha maeneo yanayo tiririsha maji katika mto Ruaha Mkuu na Kilombero



Source: MDY TV
 
February 22, 2020
Mahenge, Morogoro

Hali ilivyo ktk mkondo wa Mto Ruaha



Source : ALII TV
 
March 20, 2020
Morogoro, Tanzania

Mto Ruaha wazidi kufurika ktk mkondo wake
Kufuatia mvua kubwa zinazonyesha ktk vyanzo vinavyotema maji ktk mito ya Ruaha na Kilombero hii ndiyo hali mkoani Morogoro
Wananchi makazi yao n mashamba yamezingirwa na maji
MAFURIKO VIJIJI VYA
  1. NYANGE-MBANANO,
  2. KICHANGINI,
  3. MKANYAGENI,
  4. MTULULA NA
  5. MSOLWA STATION.


source : Adelaide Daycare Kilombero
 
RUFIJI YA YAKUMBWA NA MAFURIKO

Vijiji vyakumbwa na mafuriko, njia ya kupeleka vifaa na zana za ujenzi ktk mradi mkubwa wa umeme bwawa la Nyerere maarufu kama Stiegler's Gorge Rufiji haipitiki amesema mkuu wa wilaya ya Rufiji Mh. Mohamed Mchengerwa wakati akiongea na waandishi wa habari.



Kata zote kumi na tatu za wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani zimeathirika na mafuriko. Maeneo yote ktk tarafa za Muhoro, Ikwiriri , Mkongo pia zimeathirika.

Mvua zinazoendelea ktk Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania, pia mkoa wa Morogoro zinatiririsha maji mengi ktk mto Ruaha, Ruaha Mkuu, Kilombero na Rufiji hivyo kuleta mafuriko maeneo ya Rufiji mkoani Pwani, Tanzania.
source: DOM 27 ONLINE TV
 
March 20, 2020

Taarifa ya Habari ITV

Mafuriko nyumba 200 zaathirika Kilombero mkoani Morogoro



Source : ITV Tanzania
 
March 18, 2020

LIVE: MAFURIKO RUFIJI HALI MBAYA SANA| WANANCHI WANAVYOMLILIA RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

Wananchi wa Rufiji wanalia viongozi wa Rufiji hawawasiliani na serikali kuu Dar es Salaam na Dodoma kuwaambia ukweli kuhusu hali mbaya ya mafuriko Rufiji.



source: Jambi online TV
 
March 20, 2020

Waziri atembelea bwawa la Umeme Kidatu

Waziri wa Nishati atembelea bwawa la umeme la Kidatu ambapo kuna kituo cha kuzalisha nguvu za umeme na kuangalia hali ilivyo baada ya maji kujaa sana na pia apate taarifa juu ya uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka kituo hicho



Source: Tanesco Yetu
 
March 21, 2020

Waziri afika ktk bwawa la Mtera

Waziri wa Nishati atinga bwawa la Mtera kuona kiwango cha maji yaliyofunguliwa kutokana na mvua nyingi pia na uzalishaji wa umeme unaoingizwa ktk gridi ya umeme wa taifa



Pia waziri alisisitiza lazima bwawa la Mtera wafungulie maji ya ziada yaingie mtoni kuepusha bwawa la Mtera lisipate madhara na hivyo akawaambia wakuu wa wilaya zilizopo ktk mkondo wa Mto Ruaha wafahamishe wananchi waishio kando ya mto kuchukua hatua ya kuhama wasipatwe na mafuriko.

Source : IPC Mkombozi TV
 
WASIOJULIKANA WAIPA HASARA TANESCO

Hujuma kubwa katika mfumo wa kusambaza umeme



Abeid Abeid meneja wa TANESCO wa masuala ya usalama Tabora akionesha hujuma yenye hatari kubwa si kiuchumi tu bali hata kuhatarisha maisha ya watu inayofanywa na watu wasiojulikana

Source : millard ayo
 
April 7, 2020
Rufiji, Tanzania

LIVE MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA UMEME RUFIJI

Mradi wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) almaaruf mradi wa Stiegler's Gorge huko Rufiji mkoani Pwani Tanzania

 
14 February 2021

Tanesco yasema hali ya Mtera inaridhisha, yarekodi mita 697.97 juu ya usawa wa bahari ​


Meneja wa kituo cha kufua umeme cha Mtera, Elias Mwalupilo akitoa wasilisho kwa Bodi iliyotembelea Mtera ikiongozwa na Dk Kyaruzi, amesema kina cha maji bwawa la Mtera kimeongezeka kama ilivyo rekodiwa leo Februari 14, 2021 na kufikia mita za ujazo 697.97 juu ya usawa wa bahari.

Amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha bwawa limebakiza mita 0.53 kufika kina cha juu ambacho ni mita 698.50.

Bwawa la Mtera ndilo inalotumika kufua umeme kwenye vituo vya Mtera na Kidatu ambapo linapata maji kupitia vyanzo vya mto Ruaha Mkuu, Ruaha Mdogo na Kisigo.

Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi, Dk Kyaruzi ametoa wito kwa wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo vya maji kuhakikisha shughuli hizo hazileti athari katika upatikanaji wa maji na wayatumie kulingana na maelekezo yanayotolewa na wataalamu kutoka Bonde la Mto Rufiji.

Ameongeza mradi wa Rufiji wa bwawa la Julius Nyerere JNHPP maaruf kama Stiegler's Gorge ukikamilika utategeme maji yanayotoka Mtera pia, hivyo kuathirika kwa Mtera kutaathiri ufuaji wa umeme Julius Nyerere.
 
February 10, 2020

​



Bwawa la Mtera lenye uwezo wa kufua umeme megawatts 80 linazidi kujaa maji na hivyo TANESCO huenda wakalazimika kufungulia maji, hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco. Maji yakitoka hapo pia huenda kituo cha Kidatu na kufua umeme mwingine wa Megawatts 204. Hii inatokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa miezi miwili iliyopita nchini.

Kufuatia hatua hiyo wananchi wa mikoa ya Dodoma, Morogoro na Bonde la Ruaha /Rufiji wametakiwa kuchukua tahadhari maana mkondo wa maji ktk mito ya maji kama Mtera itazidi kujaa katika maeneo yao iwapo bwawa la Mtera litazidi kujaa maji kufikia ukomo wake na kulazimika kufungulia maji.

Maeneo yatakayopata ongezoko la mtiririko wa maji ktk mito na vijito ni wilaya za Mpwapwa, Kilolo, Kilombero, Kilosa na Bonde la Mto Rufiji.

Hivyo wananchi wanaoishi maeneo hayo waendelee kufuatilia taarifa juu ya hali ya Bwawa la Mtera zitakazokuwa zinatolewa na Tanesco kila mara. Mara ya mwisho kufungulia bwawa la Mtera ili kutiririsha maji ya ziada kulifanyika mwaka 2008 hivyo TANESCO ina uzoefu wa kufanya zoezi hili kwa usalama bila kuleta madhara kwa watu waoishi katika mkondo wa maji. Taasisi zingine zote zimetaarifiwa kuhusu tahadhari hiyo. Mwisho wa kumnukuu Mkurugezi Mtendaji wa Tanesco Dr. Tito Mwinuka.

Source: TANESCO Yetu

Hizo mita 650 hazijumuishi tope lililojaa huko chini?

Kwanini umeme unakatika hovyo wakati maji ni mengi ya kutosha?
 
Hizo mita 650 hazijumuishi tope lililojaa huko chini?

Kwanini umeme unakatika hovyo wakati maji ni mengi ya kutosha?

Swali zuri sana la kitaalamu, inabidi TANESCO wajitokeze kujibu.
 
16 February 2021
Bwawa la Mtera

Dkt. Alexander Kyaruzi mwenyekiti wa bodi Tanesco na wajumbe watembelea bwawa la Mtera ambalo sasa limejaa maji mengi kutosheleza 2021/2022



Source : TANESCOYETU
 
Back
Top Bottom