Namba tatu hiyo ndio jambo la msingi zaidi.... maana haya tunayoandika yanaakisi kile tunachofikiri sasa tukipewa muongozo wa nini cha kufikiri basi tutajua pia nini cha kuandikaBila shaka serikali inabidi itoe muongozo kwa wananchi mambo yafuatayo
1.Maneno ya kuongea
2.Maneno ya kuandika
3.Maneno ya kufikiria n.a. kipi cha kufikiria
4.Maneno ya kuipongeza serikali
Ni hivi huyo Maxence Mello hata hii jf ikifungwa anaweza kuanzisha forum nyingine kabisa. Magazeti mangapi yamefungiwa na bado watu wametoka kivingine? Tunajua wanaotafutwa ni watu wanaomwaga ukweli unaowaumiza watawala na wala sio waandika uzushi kama unavyotaka kutuaminisha. Kuna mtu alitoa nyaraka fake ya mahakama kuhusu zuio fake la mahakama kwenye umeya wa Dar kipi alifanywa? Nondo zinazomwagwa humu usipime, watu wanasema ukweli kiasi watawala hawalali hivyo namna pekee sio watawala kujirekebisha bali ni kuwafanyizia hao watoa ukweli. Ww kwa sasa uko salama japo ni mmoja kati ya watu wachochezi na wanaovunjia wengine heshima ila salama yako unasifia watawala.
ehe we taratibu,umetumwa nini?vyote unvyoona hapo ni halali najua wewe ni mmoja wa mnaomshikilia mkulu wa jf ndugu maxele,unataka nijikamatishe kwako siyo?Ww kweli akili 3
Ina maana IP na Mac address zako zote feki
Max atafunga jukwaa hili namfahamu sana homeboy hakubali mambo ya kijinga ya kutoa taarifa atatengeneza kitu kingineSidhani kama watakuwa wamemshindwa Mange Kimambi. Inawezekana ni suala la muda tu. serikali haishindwi kitu. Cha kuombea mtandao wetu ubaki salama
Wanafunga mwili mzimamzina sio mdomo tenaSio kufungana midomo, ni zaidi.
ndo itafahamika sasa ..........................Kuna sheria gani kwenye katiba ya nchi inayosema nikimnyima polisi maelezo nanyimwa dhamana na kupelekwa mahakamani?
Kama mimi nipo huku Songea. Hata ATCL haileti ndege. Itakuwa ngumu kufika
Kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria vikiwa kwenye uchunguzi wa jambo ni wajibu ! Kwanini ufiche au ni sehemu ya tatizo ?!View attachment 445705
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.
Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.
Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.
Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.
wanasema virtual ip, inapoteza maboya!! halafu huyo member kama aliingia JF kupitia deep Web itakuwaje?Hahahaha kwa hiyo unajiona upo salama na IP Address yako unaijua,
Kwa mujibu wa maelezo"kosa ni kuwanyima polisi taarifa binafsi za wateja"kakamatwa bila sababu?
Viongozi wanaotukana watu je??Kwa nini tusiwe safe? Tunafanya maovu yepi? Labda wale wanaotukana viongozi
Safi sanaKugoma kutoa taarifa za watumiaji wa JF