Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Bila shaka serikali inabidi itoe muongozo kwa wananchi mambo yafuatayo
1.Maneno ya kuongea
2.Maneno ya kuandika
3.Maneno ya kufikiria n.a. kipi cha kufikiria
4.Maneno ya kuipongeza serikali
Namba tatu hiyo ndio jambo la msingi zaidi.... maana haya tunayoandika yanaakisi kile tunachofikiri sasa tukipewa muongozo wa nini cha kufikiri basi tutajua pia nini cha kuandika
 
Ni hivi huyo Maxence Mello hata hii jf ikifungwa anaweza kuanzisha forum nyingine kabisa. Magazeti mangapi yamefungiwa na bado watu wametoka kivingine? Tunajua wanaotafutwa ni watu wanaomwaga ukweli unaowaumiza watawala na wala sio waandika uzushi kama unavyotaka kutuaminisha. Kuna mtu alitoa nyaraka fake ya mahakama kuhusu zuio fake la mahakama kwenye umeya wa Dar kipi alifanywa? Nondo zinazomwagwa humu usipime, watu wanasema ukweli kiasi watawala hawalali hivyo namna pekee sio watawala kujirekebisha bali ni kuwafanyizia hao watoa ukweli. Ww kwa sasa uko salama japo ni mmoja kati ya watu wachochezi na wanaovunjia wengine heshima ila salama yako unasifia watawala.


Kama nilivyosema huo ni uamuzi wake, lkn najua kwamba ninyi mnaomchochea kesho akihitaji mtu wa kumdhamini mtaanza sababu sijui nasomesha mara mama kalazwa n.k.
 
Ww kweli akili 3

Ina maana IP na Mac address zako zote feki
ehe we taratibu,umetumwa nini?vyote unvyoona hapo ni halali najua wewe ni mmoja wa mnaomshikilia mkulu wa jf ndugu maxele,unataka nijikamatishe kwako siyo?
 
Sidhani kama watakuwa wamemshindwa Mange Kimambi. Inawezekana ni suala la muda tu. serikali haishindwi kitu. Cha kuombea mtandao wetu ubaki salama
Max atafunga jukwaa hili namfahamu sana homeboy hakubali mambo ya kijinga ya kutoa taarifa atatengeneza kitu kingine
 
duhh hapa kazi kweli kweli, polisi wangetumia utalaam wao na ukachero, au ndo sheria ya owner wa group or blog or media anything member ekitenda wanakula na mwanzilishi wa hilo kundi nasikia hata wastaup, ukilianzisha mtu akarikoroga huko wanakufuata wewe
 
Kama kusema ukweli kwenye utawala huu ni kosa tutafungwa wengi sana
 
Kama mimi nipo huku Songea. Hata ATCL haileti ndege. Itakuwa ngumu kufika

Kwenda zako huko Lizaboni, ww huna tatizo maana unafahamika na hao wanaotaka taarifa na huwa huwapondagi. Usitake kujifanya eti na ww unaogopa, unaogopa kitu gani wakati unasubiri kupewa cheo kwa kazi nzuri ya kuwatusi cdm na Lowassa?
 
Mungu mjalie Rais wangu Busara na hekima kwa kila afanyalo na amualo atufikishe salama.
 
View attachment 445705
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.
Kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria vikiwa kwenye uchunguzi wa jambo ni wajibu ! Kwanini ufiche au ni sehemu ya tatizo ?!
 
Hahahaha kwa hiyo unajiona upo salama na IP Address yako unaijua,
wanasema virtual ip, inapoteza maboya!! halafu huyo member kama aliingia JF kupitia deep Web itakuwaje?
====
mimi naomba haki itendeke. niko tayari kumsaidia Max, kwa kile nitakachoweza kusaidia ili apate uhuru wake.
 
ASasa kwanini wasiwavamie wamiliki wa Instagram??
 
Jamiiforums ndiyo chombo pekee huru cha watanzania kubadilishana mawazo-mgongano kwa kina na kunoa bongo zetu . Kiasi kwamba kila hoja tata iletwayo humu hupewa hitimisho zuri lenye afya kwa jamii. Mpaka sasa sioni tatizo la Jamiiforums kiasi ya Maxence Melo kubebeshwa msalaba kisheria maana hoja zote tata huwa tunamalizana humu humu kwa hoja au moderators kufunga, kufuta au kutoa adhabu. Sasa sijui serikali inataka nini zaidi toka baraza letu la majadiliano huru.
 
Back
Top Bottom