Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Maelezo yako ni mazuri kwako. ukabila wako hauna nafasi Tanzania. Tunaweza kuendelea kama taifa hata tusipozingatia haya mawazo yako yako ya Kikabila.
Ukweli uko palepale kuna tofauti kati ya kuropoka na Freedom of speech.
Max yuko ndani kukutea watu kama wewe.

Be peacefully, obey laws.
 
 

Watumiaji wa mtandao wa JamiiForums wako huru kuweka mijadala, kuanzisha mijadala, kuchangia chochote pasipo kuvunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa.

What if wakivunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa?
 
Better
 
Nawashauri jamiiforums wafungue company USA then hii JF iwe chini ya hiyo company ili iwe inaoperate kwa sheria za huko America. Ila pia vijana mkiwa nyuma ya keyboard muwe na staha, mtaiponza hii forum, No Freedom With No Limit. Tujifunze kwa Snowden, amekuwa mtumwa kwasababu ya kuongea ukweli tena kwenye nchi tunayoamini ni ya kidemokrasia. Mwisho kwa kila mtumiaji wa JF tuwe tunasoma privacy policy kabla ya kutoa taarifa zetu itatusaidia pia kujua kipi cha kuchangia na kipi ambacho sicho. Gob bless Jamiiforums, Gob Bless Maxence Melo.
 
Yaani hadi sasa hawajamfikisha Maxence mahakamani! Huyu ndugu hatafanyiwa kama G. Lema kweli?

Vv
 
Ilianza kidogo kidogo kabla ya kufikiwa gazeti la mbunge wa Ubungo Kubenea, yakafuatia mazuio ya UKUTA baadhi yetu tukabeza. Ikaja Lema wengine wakasema ni mkorofi na sasa ni Maxence, ni nani atafuata ...who'll be next!?
Kwa hiyo mawazo huru yasiwepo au wanataka sote tuwe kama wa redio ya wafu!
Yaani hadi sasa hawajamfikisha Maxence mahakamani! Huyu ndugu hatafanyiwa kama G. Lema kweli?
 
Kulikuwa na ulazima gani wa kumkamata na kumnyima dhamana mtu ambaye mamlaka ikimhitaji atakwenda mwenyewe? Ni bahati mbaya kubwa inayojitokeza kuwa mahabusu kunatumiwa kukomoa baadhi ya makundi kinyume cha matumizi ya mahabusu ambayo yalikuwa ni mahali pa kuhifadhia wachache walio na madhara kwa jamii au wale ambao watakuwa huru watakuwa na athari au kuathiriwa na jamii.

Ni muendelezo wa mikomoano kama hii ambapo mahabusu na magereza zinaendelea kujaa watu pomoni wasio na hatia bali waliowekwa huko kwa ajili ya kukomolewa.

Pole zenu bwana Melo, poleni Lema, na poleni wapigania haki wote mnaoathirika na matumizi mabovu ya madaraka tunayoyaona kila uchwao wakati ambao wangekuwa huko wakiendelea kudunda mtaani Kijecha jecha.
 

Ni kweli nadhani Jamiiforums yenyewe itabidi wajilaumu, wameruhusu siasa zitawale zaidi kuliko chochote kile, Watu wanaamini wanaweza kuongea chochote kile bila hata kuchukuliwa hatua na mbaya zaidi watu wamehamisha propaganda kutoka kwenye social networks wamezileta huku, hii pia imefanya watu kuona JF ni kama jukwaa la siasa au sehemu ya kufanya propaganda tu kumbe siyo hivyo, JF ni zaidi ya shule hapa, watu wamejifunza na kufanikiwa kibiashara kupitia JF na kuna benefits nyingi sana watu wamepata kupitia hii Forum, sasa mtu mmoja au jukwaa moja tu la siasa linaweza kuigharimu jamiiforums nzima.
 
Hongera Max, naamini Tanzania umebaki wewe tu ambaye unaweza kusimama na kuwatetea watanzania wote na sio watumiaji wa jamiiforums tu. Mungu azidi kukusimamia. watanzania tunaamini utatoka soon. Tunataka watu wanaojitambua kama wewe Max
 

Nadhani ni sahihi wakachukua hatua hiyo ,maana dhamana ni haki ya Mtuhumiwa. Lakini kwa bahati mbaya Polisi wamekuwa wakitumiwa kuwaumiza watuhumiwa Kisaikolojia.

Ni muda sasa Mawakili kuweza kuiangalia Sheria ikiwezekana kufungua Kesi ya Madai dhidi ya Jeshi la Polisi kwa hivi Vitendo vya kuwanyima Dhamana watuhumiwa.
 
Lakini serikali ikihitaji information zozote toka Jf wanashindwaje kudukua ktk server za Jf mpaka wamkamate jamaa
 
Wakurugenzi wa Mitandao kama Watsaap, Facebook, Weakleaks na mingineyo duniani wanaishi vipi kama mmiliki wa kimtandao kidogo tu cha JF kinachotumiwa zaidi na wasomi anahenyeka kiasi hicho?

Katika mitandao kama ya weakleaks watu mashuhuri duniani huchafuliwa,hutajwa Wazi kwa sifa zao na anayechukia huambiwa akashtaki.Lakini hatujawahi kusikia hata siku moja DG wa mtandao huo akihenyeka kama anavyohenye kama alivyo Max.
 
Hivi haujui kama serikali inaweza kuzuia facebook,instagram,etc... kutokuwa hewani kwenye ardhi ya Tanzania sembuse ije iwe jf?
 
Hivi kweli Max akipewa taarifa uje Polisi tarehe kadhaa ili tukufikishe mahakamani hatakwenda kweli mpaka mpaka awekwe ndani kama jambazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…