Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Hatimaye tutakujua uliyekuwa unamtukana Nyerere na watu wengine kadhaa. Kungwi utapatikana.
Hii si sheria ilianza kuandikwa na Waziri January Makamba? Hapa Rais Magufuli kaweka tu sahihi ila muanzilishi ni Rais Kikwete.

Insikitisha sana. Tunamuombea kila la kheri Max.
 
I thought wangefanya jitihada kuhack hii jf na kutafuta wanachokitaka instead ya kumuwajibisha mmiliki.

Inanikumbusha kesi ya Apple na FBI kuhusu kuwapa backdoor ya IOS, mahakamani walishindwa FBI then they bypass it kupitia third person.

Kuna haja ya kuongeza wataalam wa ethical hacking katika kitengo chao. I can't believe imewashinda kuhack server.
 
JF ina rensponsibility kubwa sana, kama vivlivyo vyombo vingine vya Habari, kuna mambo mengi ya uongo na uzushi huletwa humu na kuachwa, ikumbukwe kwamba nchi nyingi kama Kenya, Rwanda, Burundi n.k Vita ililetwa na Vyombo vya Habari kama redio na TV, hivyo JF ina jukumu la kulinda amani ya nchi, kama ni kweli amekamatwa, na kama siyo kweli basi wajifunze na wabadilike, watambue jukumu lao kwenye Jamii!

CEO wa JF asipumbazwe na watu wanaosapoti kwenda kinyume na Serikali hapa, wengi wao wana maisha yao na wala hawaishi TZ, na JF ikifa kesho, au ofisi ya JF kunyimwa kibali cha kufanya kazi TZ hawana cha kupoteza, zaidi ya kuhamia kwenye mtandao mwingine na kuendeleza wanayoyafanya, hivyo angalia maisha yako na familia yako, fanya lililo sahihi na jinsi Serikali inavyokutaka kwani mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye nchi, watakushauri wanachama wa JF wanavyotaka lkn Serikali ndiyo wasimamizi wa hii nchi!
Andiko lako la vitisho lina maana gani ? Kwa muda mrefu umetumia jf kutukana chadema bila kuguswa , leo viongozi wako wakikosolewa unaomba msaada wa polisi ili iweje ? Hivi wewe ni wa kuitisha jf kweli ?

Mwigulu Nchemba ambaye ni waziri wa hawa polisi ni member humu , na ameitumia sana jf kutoa dukuduku lake , leo hii mnasahau nini ?
 
Nimeukuta Uzi umefika mbali ila niwape neno la tumaini:

"Watashindanaaaaaaaaaa lakini hawatashindaaaaaaaa"

Malaika wa Mungu Muweza Yote Yupo na wenye haki wote.
 
nimekumbuka ule uzi wa kipindi kile wa sijui blah blah members wa jf tujuane kwa majina na picha na mawasiliano blah blah! Nilitrash mbaya tupa kule
 
Nilijua tu hili iko siku itatokea. Tatizo moderator wamekuwa too soft hasa kuacha maada zinazo chafua hali ya hewa. Mfano kuna maada kibao tu za kumtukana rais nilishaomba zifutwe ila moderator wanapotezea. Kikubwa watu wasilete habari za uongo hapa jukwaani
Tatizo lako upo kusifia vitu vya uongo, hivi siku hizi habari ya kweli inaitwa ya uongo? Najua wewe upo salama sabb kila siku unasikia ujinga, wacha sie tunaotafutwa tusubiri siku ya kupelekwa jela kwa kukataa kumsifu mtukufu malaika. Kumbuka hata kagame anayafanya kama haya ya kuwakamata wakosoaji wake
 
Tofautisha kukosoa na kuleta habari za uchochezi.
Ingekuwa ni kukosoa JF ingekuwa imeshafungiwa muda mrefu sana. Lakini kwa kuwa kuna haki ya mtu kujieleza au freedom of speech ndio maana ipo mpaka leo.

Wanaotafutwa hapa ni wale wachochezi ambao ndio wamemponza maxence mello watu ambao ni chadema na kosa kubwa ni kuitumia JF kama Propaganda tool yao kueneza uchochezi.

Kama utakumbuka vizuri taarifa za kujiuzulu
Makamu wa rais zililetwa humu na pia ni humu humu JF ilitolewa taarifa ikiw na nembo ya ikulu
Pamoja na Sahihi ya msemaji wa ikulu
Ikielezea juu ya kutenguliwa kwa mrisho Gambo.

Hakuna nchi yoyote itakayovumilia uchochezi kama huo na hao ndio haswa wanaotafutwa na serikali Kwasababu aliyefoji amefanya kosa la jinai na anatakiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria na hao waovu ndio mello
Anawalinda.
Hivi yule aliyefoji amri ya mahakama umeya kinondoni. Alifanywa nini
Na ni nani atang'amua kua hii taarifa au habari ni uongo uongo!? Kama serikali ina nia njema kwanini isikamate mashoga wanao jiuza FB!? Lengo hapa ni kutoa Taarifa zitakazo msifia na kumtukuza mtukufu.
 
Habari za mashoga zinahusiana vipi ?
Kung'amua kama sio ukweli ni swala la mtoa habari
Kwanini alete habari ya kizushi ?
Serikali iwe kilasiku kukanusha uzushi !!!
Kwani wasemaji wa ikilu wanalipwa kwa kazi gani
 
Watakaosalimika humu ni Lizaboni, Ruttashobolwa na wote wanaoegemea upande wao, wadau wenye mawazo huru tuko mashakani.


Vv
Unaweza kuwa na wazo huru lakini la kizushi na hali itakapochafuka watu watakupatia wapi wakati unasajili humu JF detail zako zote zipo kwa Maxence Melo ambae leo hii yeye ndio anasota rumande wewe unakatisha tu mitaa.
kama detail ulizoweka ni za uongo hapo ni inshu nyingine yeye anatakiwa kuweka vigezo na masharti ya kujiunga humu JF vinavyoendana na sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom