TANZIA Mkurugenzi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Abdul Mussa afa ajalini

TANZIA Mkurugenzi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Abdul Mussa afa ajalini

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Katiba na Sheria Dk. Abdul Mussa, amefariki dunia leo Jumapili Aprili 23, 2023 saa sita mchana baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Dodoma kupata ajali eneo la Mdaula wilayani Bagamoyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo baada ya gari aina ya Toyota Hilux alilokuwa akisafiria likiendeshwa na Alex Festo kuligonga kwa nyuma gari aina ya Howo lililokuwa linaendeshwa na Rashid Mohamed.

"Tunaendelea kuwashikilia madereva wote waliokuwa wanaendesha magari hayo na chanzo cha ajali bado tunaendelea kukichunguza,"amesema.

Amesema kuwa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda Lutumo amesema katika ajali hiyo hakuna majeruhi yoyote zaidi ya kifo cha Mkurugenzi huyo na amewataka madereva kuongeza umakini pindi wawapo barabarani ili kuepusha ajali zinazoepukika ambazo husababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu.

Mwananchi
 
Madereva wa Serikali sijui wanapatikana kwa njia gani. Fikra zangu zinanituma kuwa hawa madereva wa Serikali kama ilivyo kwa watumishi wengi wa Serikali, wanapatikana kwa njia ya vimemo na siyo weledi.

Yaani gari ya Serikali iwapo barabarani ni potential hazard kwa watumiaji wengine wote wa barabara.

Madereva wa magari ya Serikali, kabla ya kuajiriwa wapelekwe chuo maalum, na iwepo kampuni maalum ya kuwafanyia grading.

Poleni sana wafiwa.

Tunamwomba Mungu wa huruma amjalie pumziko jema la milele.
 
Acha wafe wote nature inafanya KAZI yake kutuondolea madereva wabovu.

Hawa jamaa wakiwa barabarani wanajiona dunia ni Yao Acha wafe Tu.
 
Madereva wa Serikali sijui wanapatikana kwa njia gani. Fikra zangu zinanituma kuwa hawa madereva wa Serikali kama ilivyo kwa watumishi wengi wa Serikali, wanapatikana kwa njia ya vimemo na siyo weledi.

Yaani gari ya Serikali iwapo barabarani ni potential hazard kwa watumiaji wengine wote wa barabara.

Madereva wa magari ya Serikali, kabla ya kuajiriwa wapelekwe chuo maalum, na iwepo kampuni maalum ya kuwafanyia grading.

Poleni sana wafiwa.

Tunamwomba Mungu wa huruma amjalie pumziko jema la milele.

Katika ranking ya madereva wa hovyo. Baada ya madereva wa bodaboda wanafuatia wa Serikali.
 
Mkuu uwe unasoma taarifa husika kabla ya kufanya majumuisho..gari aliyopata nayo ajali ni ya binafsi..hivyo labda alikuwa anaendesha mwenyewe au mtu mwingine ambaye kwa uhakika siyo dereva wa Serikali.
Shukrani sana, ila nilisoma na taarifa inasema madereva wote wawili wanashikiliwa Kwa uchunguzi zaidi! Inawezekana wakawa wamemshikilia marehemu. Asante Mkuu kwa reminder pia japo nilishasoma!
 
Back
Top Bottom