TANZIA Mkurugenzi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Abdul Mussa afa ajalini

TANZIA Mkurugenzi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Abdul Mussa afa ajalini

madereva wa serikali shida ni kwamba wanalipwa kidogo, na wanaendesha magari wakiwa na hasira. waongezeeni mishahara.
 
Ofisi zimehamishiwa Dodoma ila Kila siku wapo Dar yaani barabara ya Dar - Dom ndo imekuwa ofisi sasa hivi
 
Kibaha. Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Katiba na Sheria Dk Abdul Mussa, amefariki dunia leo Jumapili Aprili 23, 2023 saa sita mchana baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Dodoma kupata ajali eneo la Mdaula wilayani Bagamoyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo baada ya gari aina ya Toyota Hilux alilokuwa akisafiria likiendeshwa na Alex Festo kuligonga kwa nyuma gari aina ya Howo lililokuwa linaendeshwa na Rashid Mohamed.

"Tunaendelea kuwashikilia madereva wote waliokuwa wanaendesha magari hayo na chanzo cha ajali bado tunaendelea kukichunguza,"amesema
Also Read

Amesema kuwa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda Lutumo amesema katika ajali hiyo hakuna majeruhi yoyote zaidi ya kifo cha mkurugenzi huyo na amewataka madereva kuongeza umakini pindi wawapo barabarani Ili kuepusha ajali zinazoepukika ambazo husababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu.

Mwananchi
Dereva wa Hilux nina mashaka naye sana.

Anyways mambo ya serikali yana uzito mkuu

Mungu ampokee mtangulizwa mja wake
 
Hili swala lilinishangaza, kazi kama udereva ni kazi inayohitaji experience zaidi, waliwaonea
Kuna dogo mmoja wa mtaani kwetu. Alikuwa ni dreva wa tug boat zile zinazovuta meli toka nje ya mlango hadi maegesho. Naye alikuwa na cheti feki pamoja na wenzie. Wote mwaka 2018 walipigwa chini. Lakini TPA ikawa inawatumia kama vibarua kufanya kazi ile ile kwa miezi kama 6 kwa kuwa wenye vyeti halisi walikuwa hawana uwezo wa kuegesha meli.

Tukisema Magufuli alikuwa wa hovyo mutuelewe
 
Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Katiba na Sheria Dk. Abdul Mussa, amefariki dunia leo Jumapili Aprili 23, 2023 saa sita mchana baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Dodoma kupata ajali eneo la Mdaula wilayani Bagamoyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo baada ya gari aina ya Toyota Hilux alilokuwa akisafiria likiendeshwa na Alex Festo kuligonga kwa nyuma gari aina ya Howo lililokuwa linaendeshwa na Rashid Mohamed.

"Tunaendelea kuwashikilia madereva wote waliokuwa wanaendesha magari hayo na chanzo cha ajali bado tunaendelea kukichunguza,"amesema.

Amesema kuwa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda Lutumo amesema katika ajali hiyo hakuna majeruhi yoyote zaidi ya kifo cha Mkurugenzi huyo na amewataka madereva kuongeza umakini pindi wawapo barabarani ili kuepusha ajali zinazoepukika ambazo husababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu.

Mwananchi
Mdaula tangu lini ikawa Bagamoyo?
 
Pamoja na Hilo hiko kipande cha Kibaha Pwani nacho kinaongoza kwa ajali, lazima kuna engineering errors ambazo hatujawahi kukaa chini kuulizana.. Why njia hiyo ina ajali nyingi sana
Ni uchawi tu mkuu, pana ugwiji sana hicho kipande.
 
Back
Top Bottom