Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande ameongelea mahitaji ya umeme miaka ijayo ambapo amesema mpaka 2035 angalau megawatt 80,000 zitahitajika akikadiria nchi itakuwa na watu milioni 70-80 kutoka milioni 61 iliyopo sasa ili watoto wanaokua wapate ajira kwenye viwanda na kinyume chake itakuwa tatizo kubwa.
Maharage amesema umeme huo ndio utahitajika kuendesha uchumi lakini sasa wanaongelea megawatt 5000 kufikia 2025 huku mpango mkakati mkubwa uliopo ukisema mpaka 2035 Taifa liwe angalau linazalisha megawatt 40,000.
Chande amesema rasilimali za kukuza uzalishaji wa umeme kwa kiwango hicho sio kutoka Serikalini peke yake bali zitoke sekta binafsi na ameitaka jamii ielewe sekta binafsi kuchangia kwenye umeme sio tatizo bali inawezekana.
Chande amesema gharama ya uwekezaji ni kubwa na ataeweka hela inapasa kuwa wote, serikali na sekta binafsi.
Kipindi cha gesi ya mtwara tuliaminishwa kuwa tatizo la umeme litaisha zaidi ya miaka50 mbele.Sasa hivi mmeanza tena uwekezaji binafsi ili mturudishie Iptl ili tuanze kulipishwa bill kubwa za umeme?
Mkurugenzi wa Tanesco, Maharage Chande ameongelea mahitaji ya umeme miaka ijayo ambapo amesema mpaka 2035 angalau megawatt 80,000 zitahitajika akikadiria nchi itakuwa na watu milioni 70-80 kutoka milioni 61 iliyopo sasa ili watoto wanaokua wapate ajira kwenye viwanda na kinyume chake itakuwa tatizo kubwa.
Maharage amesema umeme huo ndio utahitajika kuendesha uchumi lakini sasa wanaongelea megawatt 5000 kufikia 2025 huku mpango mkakati mkubwa uliopo ukisema mpaka 2035 Taifa liwe angalau linazalisha megawatt 40,000.
Chande amesema rasilimali za kukuza uzalishaji wa umeme kwa kiwango hicho sio kutoka Serikalini peke yake bali zitoke sekta binafsi na ameitaka jamii ielewe sekta binafsi kuchangia kwenye umeme sio tatizo bali inawezekana.
Chande amesema gharama ya uwekezaji ni kubwa na ataeweka hela inapasa kuwa wote, serikali na sekta binafsi.
Ya IIPTL Richmond Dowans, Songas et al bado tu anaona haitoshi? Tuendelee kulipa mabilioni kila mwezi ya capacity chqrges! wale wahindi waliopewa mktataba wa mabilioni output yao ndio hiyo.!