Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza na waandishi wa habari Dkt. Aneth amesema kwamba katika kufanikisha hilo watakuwa kwenye maadhimidho miaka 50 ya TET wameandaa kampeni ya 'Kitabu Kimoja kwa Mwanafunzi Mmoja' ambayo itachochewa na hamasa na wadau mbalimbali.
Amesema kuwa maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi hiyo yatafanyika Machi 7, 2025, ambapo yataambatana na matembezi ya Hisani ya Kilomita tano (5), ambapo ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia na kushiriki matembezi hayo.
Aidha imeelezwa kwamba Mgeni Rasmi katika matembezi hayo anatarajiwa kuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa, ambapo Matembezi yataanza saa 12.00 alfajiri hadi saa 2.00 asubuhi na baadaye yatafuatia na hafla ya uzinduzi wa sherehe za Miaka 50 ya TET itakayoanza saa 3:00 asubuhi katika viwanja vya TET Makao Makuu.
Lakini Dkt. Aneth ametoa utaratibu kwa wadau ambao wanataka kushiriki matembezi hayo, kwamba wanatakiwa kujisajili na kuchangia TSH. 50,000 (Fulana) au 150,000 (Trakisuti).
"Fedha hizi zitaelekezwa moja kwa moja katika uchapaji na usambazaji wa Vitabu vya Kiada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Tanzania Bara na Zanzibar. Taratibu za kuchangia na kujisajili zimebainishwa katika mitandao ya kijamii ya TET ya X, instagram na facebook inayopatikana kwa anwani ya taasisiyaelimutanzania. Karibu tutembee pamoja kufanikisha lengo la Kitabu Kimoja kwa Mwanafunzi Mmoja."
Vilevile ameweka bayana utaratibu ambao wadau wanaweza kutumia kwa ajili kuchangia kampeni ya kitabu Kimoja kwa Mwanafunzi Mmoja kwa kutumia namba ya malipo ya serikali ambayo ni 994040118259. Ambapo amesema kwamba Kampeni hiyo ni endelevu, kuwa tayari michango imekwishaanza kupokelewa na itaendelea kupokelewa
mpaka siku ya kilele cha maadhimisho hayo Mwezi Juni, 2025.
Hata hivyo amefafanua hali ya upatikanaji wa vitabu kwa sasa kwamba tayari umefikiwa wiano kitambu kimoja Mwanafunzi mmoja kwa baadhi ya masomo, ametolea mfano kwamba masomo ya sayasi wiano ni kitabu kimoja Mwanafunzi mmoja na masomo mengi ya sanaa wiano ni kitabu kimoja Wanafunzi watu. Lakini pia amedokeza kwamba zinaendelea kufanyika tafiti kuona namna wanavyoweza kuhusisha zaidi matumizi ya vifaa vya tehama katika mazingira mbalimbali.
Ikumbukwe Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ni Taasisi ya Umma iliyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Tenolojia. Taasisi hii ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 13 ya Mwaka 1975. Hivyo, Mwezi Juni, 2025, TET inatimiza Miaka 50 toka kuanzishwa kwake.