Mkurugenzi TRC asema Treni ya SGR, NO abiria kubeba vyakula, NO mafurushi makubwa

Mkurugenzi TRC asema Treni ya SGR, NO abiria kubeba vyakula, NO mafurushi makubwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa wameweka utaratibu kwa abira watakaosafiri na treni ya umeme kwamba hawataruhusu mtu asafiri na mizigo mikubwa au chakula kama ilivyo kwenye treni ya MGR, kwamba lengo la kufanya hivyo ni kutunza mazingira ya usafiri huo ili uweze kudumu kwa miaka mingi


Video: Nipashe Digital
 
Waliopanga nauli za treni ya SGR Ni wamiliki wa mabasi.
Reli imejengwa kwa pesa zetu, MATRENI yamenunuliwa kwa pesa zetu. Umeme tunao wa kumwaga, iweje nauli ziwe juu ya baadhi ya mabasi?
Ulitaka nauli iwe bei gani?
 
Huko duniani Inasemekana treni ndio usafiri wa gharama nafuu zaidi
Mnadanganywa na nani? Treni kutoka London to Manchester ni £80-120 ukipanda bus la National Express ilikuwa kama £15. Ndege unaweza kupata cheaper kuliko treni sema. Kuna EasyJet wakati huo trip za within EU unaweza kwenda hata kwa £50. Naongea nikiwa nimetumia sana treni na buses UK over ten years ago.
 
Bado soko la mabasi litakuwa juu,watu wataishobokea treni mwanzo mwanzo kisha wataipotezea
Kuna classes katika haya maisha. Jiulize kwanini boat ya kilimanjaro VII ina VIP ambayo gharama mara 3 na ya economy na inajaa. Kama hii treni itaendeshwa vizuri kwa ufanisi mabasi yatapunguza soko labda wahuni waihujumu,maana wamiliki mabasi ni hao hao vigogo wa gavoo.
 
Back
Top Bottom