DOKEZO Mkurugenzi wa AUWSA asaini Mkataba wa kifisadi wa TZS 36.3 Bilion na Mchina bila Ridhaa ya Bodi ya Ununuzi ya AUWSA na wafadhili AfDB

DOKEZO Mkurugenzi wa AUWSA asaini Mkataba wa kifisadi wa TZS 36.3 Bilion na Mchina bila Ridhaa ya Bodi ya Ununuzi ya AUWSA na wafadhili AfDB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu
Upigaji Umezidi na anatamba waziri wa Maji Aweso na PCCB Arusha wapo kwenye payroll yake hivyo atishwi na chombo chochote cha Dola.

Ofisi ya CAG imetuma wakaguzi
Mara kadhaa bahati mbaya wakaguzi wanaotumwa wanapewa Pesa wanachomoa hoja.

AUWSA inatakiwa ifanyiwe Special Audit

PCCB Tumeni kikosi kazi waende wakachunguze AUWSA, Kamanda wa PCCB Arusha ameshindwa kutekeleza Majukumu yake
una hasira yakukosa mgao nini
 
Issue kubwa hapa sio hizo management procedure ni uhalali wa mkataba husika accoding to the contract husika (AfDB/FIDIC contract documents je inaruhusu jambo hilo ( threshold = should be less or equal to 25% of the original contract) Je hili lilizingatiwa hayo mengine yote siasa na husuda tu.
Twende Pole pole unakiri kuwa tender aikutangazwa amepewa Sinohdro extension of Work? Tuanzie hapa.
 
Mama alisema awamu iliyopita watu walifanya kazi kwa uoga. Mtaamua wenyewe kipi bora
 
Upeo wako ni mdogo ndiyo maana unaona ni sawa tuu 16 Bilion kupigwa
Issue kubwa hapa sio hizo management procedure ni uhalali wa mkataba husika accoding to the contract husika (AfDB/FIDIC contract documents je inaruhusu jambo hilo ( threshold = should be less or equal to 25% of the original contract) Je hili lilizingatiwa hayo mengine yote siasa na husuda tu.
25% unaipataje kwa kazi Mpya ambayo mkandarasi ajapatikana? Mipango yenu ya kutupiga changa ya macho kuwa ni Extension of water Network tunaifahamu… For Your Information mradi wa Water Network na Construction of water blending system for FLOURIDE reduction ni Vitu viwili tofauti.

Issue kubwa hapa sio hizo management procedure ni uhalali wa mkataba husika accoding to the contract husika (AfDB/FIDIC contract documents je inaruhusu jambo hilo ( threshold = should be less or equal to 25% of the original contract) Je hili lilizingatiwa hayo mengine yote siasa na husuda tu.
 
Twende Pole pole unakiri kuwa tender aikutangazwa amepewa Sinohdro extension of Work? Tuanzie hapa.
Kulikuwa hakuhitaji open tender. This was the fastest method ya kumaliza mradi haraka na kuwapa watu wa Arusha, na wilaya zinazoizunguka maji ya uhakika. Usipotoshe umma wa Watanzania kwa information finyu zisizo na mashiko kama hujui hujui tu. Kaa chini tafuta elimu usidandie gari kwa mbele.
 
Twende Pole pole unakiri kuwa tender aikutangazwa amepewa Sinohdro extension of Work? Tuanzie hapa.

Mimi nikushauri, inaonekana una ushahidi kabisa, na sitaki kubeza kuwa umekosa mgao, nachukulia kuwa wewe ni mzalendo sana. Nakushauri nenda ofisi ya TAKUKURU utoe ushahidi wote au piga namba 113 bure
 
Kulikuwa hakuhitaji open tender. This was the fastest method ya kumaliza mradi haraka na kuwapa watu wa Arusha, na wilaya zinazoizunguka maji ya uhakika. Usipotoshe umma wa Watanzania kwa information finyu zisizo na mashiko kama hujui hujui tu. Kaa chini tafuta elimu usidandie gari kwa mbele.
Fastest Method ndiyo mpandishe Gharama za Mkandarasi kutoka 20bilion kama ilivyoandaliwa na consultancy hadi 36 bilion?

16 bilion inasambaza Maji Kilomita Ngapi?

Nakushukuru kwa kukiri Tender aikutangazwa, Hakukuwa na Evaluation team kupitia Documents na Tender aikupitishwa na Tender Board… Asante sana

Mfadhili ametoa Fedha toka Mwaka 2016 Hii Fastest method unayosema kwanini aikutumika 2016, 2017, 2018, 2019 , 2020, 2021 ?
 
Mimi nikushauri, inaonekana una ushahidi kabisa, na sitaki kubeza kuwa umekosa mgao, nachukulia kuwa wewe ni mzalendo sana. Nakushauri nenda ofisi ya TAKUKURU utoe ushahidi wote au piga namba 113 bure
Nipatieni Contact za DG wa PCCB kamanda Hamduni, Sina imani kabisa na kamanda wa Arusha Ndg Ruta tumempatia taarifa nyingi akishavuta Mpunga anauza Mechi..
 
Kulikuwa hakuhitaji open tender. This was the fastest method ya kumaliza mradi haraka na kuwapa watu wa Arusha, na wilaya zinazoizunguka maji ya uhakika. Usipotoshe umma wa Watanzania kwa information finyu zisizo na mashiko kama hujui hujui tu. Kaa chini tafuta elimu usidandie gari kwa mbele.
Hauoni kama Zabuni ingetangazwa AUWSA mngepata Mkandarasi Kwa Gharama za Chini ya 20 Bilioni?

Jiulize kwanini AFDB wamegoma kutoa No Objection? Eng Rutabula this time amewaingiza Mkenge.
 
.... wewe jamaa unamvyomsakama Mkurugenzi kwa id tofauti dah! Kungekuwa na ukweli Serikali haioni ikachukua hatua? Isije kuwa issues binafsi mnazifanya za kitaifa!
Yatakuwa majungu tu haya
 
Arusha Kuna chuki binafs Sana na wivu makazini
Chuki binafsi kivipi? Unaona ni Sahii zabuni yenye thamani ya Shilingi 38 bilion kutolewa bila Kutangazwa ni sahii?

AFDB waliogoma kutoa No Objection na wao Wana Chuki?

Unaoona ni Sahii Gharama za
mkandarasi kuongezwa kutoka 20 bilion hadi 36 bilion ni sawa? Ongezeko la 16 bilion inajenga zahanati ngapi? Inajenga madarasa mangapi? Hacha Umburura.
 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Eng Justin Rujomba Tarehe 7.7.2022 amesaini Mkataba wa Construction of water blending system for FLOURIDE reduction wenye thamani ya TZS 36.3 Bilion na Kampuni ya Sinohdro Engineering ya china bila zabuni kutangazwa , Mkataba Ulisainiwa Tarehee 7.7.2022 kisiri bila kushuudiwa na Bodi ya AUWSA, Meneja Mradi Eng Mkawe na Menejimenti ya AUWSA kama utaratibu unavyotaka

Eng Rujomba hakupata Ridhaa ya Tender Board ya AUWSA kusaini Mkataba na wafadhili wa Mradi mkubwa wa Maji.

Arusha Bank ya Maendeleo ya Afrika ( AFDB) ilishatoa maelekezo kwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji AUWSA kuwa.

Wasitumie mfumo
Wa single source bali zabuni itangazwe apatikane
Mkandarasi mwenye uwezo lakini Eng Rujomba amekaidi kwa madai kuwa Kuna 10% ya kwake na Viongozi wa Wizara ya Maji.

PPRA Mwezi Novemba 2021 walitoa maelekezo zabuni zote zenye thamani inayozidi 5Milion itangazwe kupitia TANEPS ,

Hata hivyo, Bank ya maendeleo Afrika ( AFDB) wamegoma kutoa kibali ( No Objection ) ya kusaini Mkataba bila zabuni kutangazwa,

Maswali ya Msingi kwa nini zabuni haikutangazwa? Engineer Rujomba ametumia vigezo gani kuipatia zabuni kampuni ya sinohydro mkataba wenye Fedha nyingi kiasi hiki thamani ya TZS 36.3 bilion ?Kwanini mradi umesainiwa bila kushuudiwa na Wajumbe wa bodi ya AUWSA? kwanini Mradi umesainiwa bila kushuudiwa na Meneja wa Mradi na Menejimenti ya AUWSA? Kwanini mradi umesainiwa kisiri? Kwanini ENG Rujomba amekaidi
Maelekezo ya wafadhili Bank ya AFDB,

Ufisadi huu unafanyika AUWSA katika kipindi cha miezi Mitatau baada ya Kuvunjwa kwa Mkataba wa kifisadi wa Tzs 2.5 Bilion wa Ujenzi wa mfumo wa uondoaji Majitaka wa A to Z. Cha kushangaza walioshiriki kusaini huu mktaba wapo huru wanatamba kuiweka PCCB na wizara ya Maji mfukoni.

Waziri Mkuu , DG wa TAKuKuRu na CAG fanyeni uchunguzi wa mkataba wa Construction of water blending system for FLOURIDE reduction wa AUWSA na Sinohydro muokoe hizi pesa za wananchi maana mwisho wa siku watakaoumia ni wananchi amba ni walipa kodi na wahusika walioshiriki kusaini huu mkataba wachukuliwe hatua za kisheria.
Huyu Eng..unakomaa naye balaa, Kuna kitu mnagombea nini ?
 
Back
Top Bottom