DOKEZO Mkurugenzi wa AUWSA asaini Mkataba wa kifisadi wa TZS 36.3 Bilion na Mchina bila Ridhaa ya Bodi ya Ununuzi ya AUWSA na wafadhili AfDB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi nadhani ni mikataba miwili tofauti yenye terms and conditions tofauti, kama kachelewesha wa kwanza vigezo na masharti lazima vizingatiwe na huo wa pili pia utakuwa na terms zake.
 
Tundu Lissu yupi unamzungumzia mkuu? yule wa MIGA alounguna na mabepari kukwamisha juhudi za JPM za kuboresha mikataba ya madini ili inufaishe Taifa?
 
Mimi nadhani ni mikataba miwili tofauti yenye terms and conditions tofauti, kama kachelewesha wa kwanza vigezo na masharti lazima vizingatiwe na huo wa pili pia utakuwa na terms zake.
Tunapongeza Vyombo vya Dola kwa kuanza kufanya uchunguzi.. Pongezi Zetu za dhati ziwafikie Admnin wa JF , Member wote wa JF , Kamanda wa PCCB Arusha ,Ofisi ya Mkurugenzi wa PPRA,na Vyombo vyote vya Dola ambavyo kwa namna Moja ama Nyingine wameshiriki kuchunguza Upotevu wa zaidi ya TZs 36 bilion .

TZs 36 Bilion kwa Gharama ya Ujenzi wa Darasa kwa Tzs 18 Milion kwa kila Darasa Serikali itaweza Kujenga Madarasa 2000.


Tusubiri tuone Report zao.. Tutaanzia watakapoishia.
 
Uchunguzi umulike kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na waziri wa Maji ikiongozwa na Dr. Nditi wamelipwa Posho mara mbili , Wamelipwa Posho na Wizara ya Maji na AUWSA pia imewalipa,

Waraka wa Serikali wa 2016 unataka Malipo yote yanayofanywa na Taasisi za Serikali zipitie Bank.. Dr. Nditi na team yake walilipwa Cash na AUWSA Huu ni Ujumu Uchumi maana wamelipwa Posho mara mbili na Malipo ya AUWSA yamefanyika kwa Njia ya Cash kinyume na taratibu

Uchunguzi ufike mbali kuchunguza Malipo mangapi Yamefanyika AUWSA kwa njia ya Cash badala ya Kupitia Bank?
 
Mheshimiwa Waziri Wa Maji Juma Aweso tuna taarifa Kesho utaongea na Watumishi wa Mamlaka ya Maji AUWSA Watanzania watapenda kujua Umechukua hatua gani dhidi ya waliofanya Ufisadi AUWSA.



Mkataba Kati ya na AUWSA ulisainiwa tarehe 9 Oktoba,2018 na alianza Ujenzi rasmi tarehe 09 Disemba, 2018 na Muda wa Ujenzi wa mradi ulikuwa ni miaka miwili(2) yaani miezi 24. Sinohyro alitakiwa kukabidhi mradi tarehe 08 Disemba,2020 lakini kutokana na Usimamizi mbovu wa kula rushwa wa Mkurugenzi wa AUWSA hakuweza kukamilisha Mradi.

Sinohydro aliomba kuongezewa muda wa miezi nane (8)hadi agosti,2021 akashindwa kukamilisha mradi kwa kuwa usimamizi mbovu wa Kula rushwa wa Mkurugenzi AUWSA.

Sinohydro akaomba kuongezewa muda wa miezi wa miezi minne (4) hadi Disemba, 2021. Akashindwa kukamilisha mradi kwa kuwa na usimamizi mbovu wa Mkurugenzi AUWSA.

Sinohydro akaomba kuongezewa muda wa miezi saba hadi 07 Julai,2022. Mkandarasi akashindwa tena kukamilisha mradi na kukabidhi mradi ili Wananchi wa Jiji la Arusha waanze kutumia maji yaliyo safi na salama ambayo hayana fluoride.

Kazi ambazo sinohydro hajakamilisha ni
Ujenzi wa Visima Ishirini (20) vya Majimoto- Hai ambavyo maji hayana madini ya fluoride.
Ujenzi miundombinu ya Mabomba kutoka kwenye visima 20 hadi PS1: CHEMKA.
Ujenzi wa mashine za kusuma maji kutoka PS1-CHEMKA kwenda PS2-Mbuguni Kwa sasa maji yanasukumwa kutoka visima kumi (10) Mbuguni ambavyo vina fluoride zaidi ya 6mg/l. Wananchi wanakunywa maji yanayosukumwa kutoka PS2 hadi Themi.

Katika Mkataba kati ya AUWSA na Sinohyro unaruhusu Variation-Addendum Sub-Clause 13.1.3 any additional work, plant, Materials or Service necessary for the Permanet works, including Any associatedTests on Completion, boreholes and other testing and exploratory work kipengele kinataka Mkandarasi aongezewe kazi mpya endapo bila Mkandarasi kuongezewa kazi mpya hataweza kukamilisha kazi ya awali na pia hataweza kufanya majaribio ya kazi ya awali kwa kuwa zitakuwa zinategemeana. Kwa kifungu hiki Sinohydro alikuwa hana sifa za kupata Addendum ya Construction of De-fluoridation system at Seedfarm kwa kuwa tayari kashindwa kumaliza kazi ya awali kwa wakati.

Sababu za Mkurugenzi wa AUWSA kumpatia variations(Addendum) ya Construction of De-fluoridation system at Seedfarm kampuni ya Sinohydro ni kama hizi:

Kubadilisha gharama za ujenzi kutoka Tshs 20 Bil. hadi Tshs 36.3 Bil kinyume na Engineering Estimate ili aweze kupata rushwa kutoka kwa Mkandarasi. Zaidi ya Tshs 16. 3 Bil zinakuwa zimeenda kwenye matumbo ya watu, Serikali inakuwa imepata hasara

Kumuokoa Mkandarasi na Delay Damages kinyume na Sub-Clause 8.7.1 ya Mkataba ambavyo Mkandarasi alitakiwa kukamilisha kazi tarehe 07 Julai,2022 na utekelezaji wa mradi umefikia 78% na Particular Condition ya mkataba sub-clause 8.7.1 & 14.15.1 (b)-0.1% of the Contract Price per day and Maximum amount of delay deamages -8.7.1- 10% of the final contract price . Kulingana na kazi ambazo hajafanya anatakiwa kwa siku akatwe Tshs 100 Mil(100,000,000) na kama hatakuwa hajamaliza kazi ndani ya siku 100 anatakiwa awe amekatwa Tshs 10 Bil. (10,000,000,000).

Kumuongezea Muda kijanja Mkandarasi bila Mkandarasi kuomba kuongezewa muda na wala Consultant kupitia nyongeza ya Muda ili Mkandarasi aweze kuongezewa muda wa kukamilisha kazi zake za awali kinyume na mkataba sub- clause 8.2.1 cha kukamilisha kazi ndani ya muda wa Mkataba.

Mkataba wa Addendum kati ya AUWSA na Sinohydro umeisababishia Serikali hasara ya Tshs 26.3 bil na hii bila kuweka gharama za athari za Wanachi kutumia maji ambayo yana fluoride kwa sababu za kuchelewesha mradi. Makubaliano ya aide Memoire- special supervision mission kati 13-17 Juni,2022 yalisema kwamba rejea kipengele 3.24 &25

3.24 Construction of De-Fluoridation system at SeedFarm: The consultant has finalized the preparation of designs and tender documents for the construction of the De-Fluoridation System at SeedFarm. The bidding documents were submitted on 8 February 2022 for Bank’s review and consideration for “no objection”. During the review, the AUWSA came with an option of intending assign the construction work to the contractor (M/S Sinohydro Corporation Ltd) who is on site implementing the contract of the New Water System. The Bank advised the AUWSA to come up with clear justification including work rates and completion time of the proposed option.

3.25 The proposed option was discussed during the mission and agreed that; The AUWSA will prepare the justification together with contractor’s offer and share with the Bank for review and consideration for “no objection” by 24 June 2022. In case the justification won’t be accepted or the contractor on site refuse to accept the additional works, the AUWSA will proceed with the procurement procedures which will shorten the process of engaging a new contractor. The mission agreed that AUWSA will share the bidding documents together with the specific procurement note by 30 June 2022 for the Bank review and consideration for no objection.

Mkurugenzi wa AUWSA hakutaka kufuata hata maelekezo ya AfBD akasaini Addendum bila kupata No Objection ya bank ambavyo yeye mwenyewe alisaini hayo makubaliano. Bank hawajatoa no Objection kwa kuwa rate za BoQ za Addendum zimepanda kwa 82% kutoka kwenye zile rate za awali na Hakuna Engineering Justification.

02- Mkataba wa Ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka Mkandarasi alitakiwa kufanya marekebisho kipindi cha Defects Liability kama Sub-Clause 11.1 inavyoelekeza, kipindi cha DLP ili kurekebisho Plastic Membrane ambayo yalikuwa yanajaa upepo na kuelea juu ya maji, lakini Mkurugenzi AUWSA alituma Watumishi wa AUWSA kutoboa na kuweka mawe ili kuyakandamiza kuyazuia yasielee. Kazi hii ilitakiwa kufanywa marekebisho na Mkandarasi kwa sababu ilikuwa ndani ya DLP na hata hivyo kutobolewa ni kinyume na Mkataba ila yote haya ni sababu za Mkurugenzi wa AUWSA kuchukua rushwa. Kwa sasa Makaratasi hayo hayana kazi na Serikali imepata hasara zaidi Tshs 2.8 Bil, taarifa hii ni ya kwel, tunaomba Serikali iunde tume na kuwauliza Watumishi wa Kitengo cha Majitaka na hata pia Wananchi wanaoishi karibu na bwawa hili. Serikali kupoteza Tshs 2.8 Bil ni gharama kubwa sana kwa walipa kodi.

03- Mkataba wa AUWSA na Tumaini Engineer Wenye thamani ya Tshs 2.5 Bil kujenga mtandao wa majitaka kutoka A to Z ni Wakifisadi na haukufuata taratibu za manunuzi.

Mfano wa ufisadi kwenye Mkataba unakifungu cha kuchimba na kufukia bomba Tshs 358,500,000 umbali wa kuchimba =8500m maana yake 1m inachimbwa Tshs 42,176 badala ya T.shs 12,000/=

Mkataba kutopitishwa na Bodi ya Zabuni (Tender Board) ya AUWSA kinyume na Sheria ya Manunuzi PPA,2011 section 35(1),(2) & (3)

Zabuni kutofuata Sheria ya Manunuzi (The Public Procurement (Amendment) Regulation,2016- section 91- Method of tendering for Non Consultancy Services.

Tumaini Engineer hadi Mkataba unavunjwa alikuwa tayari kalipwa zaidi Tshs 200,000,000 Mkurugenzi AUWSA na Tumaini Engineer wanatakiwa warudishe hizi Fedha kwa kuwa mkataba ulikuwa batili
 
Waziri Aweso uwa unajifanya mtetezi wa Wanyonge kwanini huu Ufisadi wa AUWSA unashindwa kuchukua hatua ?

Au na wewe ni msharika wa huu Ufisadi? Ulimsimamisha Manager wa RUWASA Mkoa wa Tanga kwa tuhuma za Tzs 12 Milion unashindwa nini kuchukua hatua Ufisadi wa Tzs 36 Bilion AUWSA?
 
Vyombo vya Dola penyezeni Vijana wa kazi Kesho kikao cha AWeso na Watumishi wa AUWSA kitafanyika Jengo Jipya la AUWSA Kisongo

Kesho waziri Aweso atakuwa Arusha kukemea watumishi wa AUWSA kwanini wanatoa taarifa za Ufisadi, Mheshimiwa Waziri hawataki watumishi wanaopambana na ufisadi unaoendelea AUWSA ..

Rais wa Jamhuri wa Muhungano Samia Suluh Hassan waziri Aweso hakufai akiwa Jukwaani anajifanya ana Uchungu na Nchi kumbe ni Fisadi.
 
Huu uzi uliishia wapi ??? Au mmehamishiwa vijijini. Ili hii nnjjjiiii
 
Huu uzi uliishia wapi ??? Au mmehamishiwa vijijini. Ili hii nnjjjiiii
Tuliamua kukaa kimya ili kutoa Fursa kwa vyombo vya Dola kufanya uchunguzi ,inasikitisha sana PCCB Arusha wameshindwa kukamata Mafisadi walioaaini huu Mkataba wa Bilion 36
 
Tuliamua kukaa kimya ili kutoa Fursa kwa vyombo vya Dola kufanya uchunguzi ,inasikitisha sana PCCB Arusha wameshindwa kukamata Mafisadi walioaaini huu Mkataba wa Bilion 36
DG wa PCCB Kamishna Salim Hamduni safisha PCCB Mkoa wa Arusha inanuka Rushwa
 
Kama mradi unaenda na unafanya kazi hebu tuambie shida ipo wapi?!
 
Laiti mngejua! Hawa unaowaambia wafanye uchunguzi nao wanahitaji kuchunguzwa!
 
DG wa PCCB Kamishna Salim Hamduni safisha PCCB Mkoa wa Arusha inanuka Rushwa
Wasafishe wao una uhakika ni wasafi? Haya mambo siyo marahisi kama unavyodhani. Kuanzia kule juu kabisa hakufai. Hawa wa chini wanakula makombo tu.
 
Wakazi wa Mkoa wa Arusha wanakunywa Maji yenye Chumvi na Fluoride Nyingi kutokana na Ufisadi wa Eng Rujomba.

Mradi wa Water Blending System for Fluoride Wenye Thaman ya Tzs 36 bilion Umesimama kutokana na Mfadhili AFDB kugoma kutoa Barua ya No Objection ( Kuruhusu Mradi uendelee) Baada ya kugundua taratibu za kumpata Mkandarasi zilikiukwa

Waziri Mwenye Dhamana ya Maji Juma Aweso ni Mla rushwa Mkubwa , Yupo tayari kuona Wakazi wa Rushwa wanakunywa Maji yenye Fluoride na Chumvi nyingi ambayo yanasababisha Madhara kwa Binadamu .
 
Wasafishe wao una uhakika ni wasafi? Haya mambo siyo marahisi kama unavyodhani. Kuanzia kule juu kabisa hakufai. Hawa wa chini wanakula makombo tu.
AUWSA imegeuzwa Shamba la Bibi kuna wakaguzi wapo wanaitwa Reliable Consultant ni mafisafi wapo AUWSA toka 2018 hakuna ukaguzi wanaofanya wa
Maana wanashinda Bar ya Ken Garden muda wao wa kukaa Arusha ukiisha wanatishia kuwa wana hoja wanavuta mpunga ( Rushwa) wanasepa,

Ni nani ataiokoa AUWSA ? Kote kumeoza kuanzia waziri Aweso, Katibu Mkuu Sanga, MD Rujomba.. PCCB Arusha wamewekwa Mfukoni, Mkaguzi anayemwakilisha CAG kampuni ya Reliable Consultant ( Ni Wazee
Wastafu wa Bandari) Wanashinda Ken Garden Siku zao zikiisha wanapewa Fungu ( Rushwa ) wanasepa…

Ninalia kwa Uchugu nikiwa nyikani nani ataiokoa AUWSA?
 
OCD Arusha hacha Kunyanyasa Raia ,Rudisha simu ya Eng Tarimo…Mmemweka Ndani ( Selo) amelala Siku tatu kwa maelekezo ya Rujomba kuwa yeye Ndiyo Moshi Town anatoa taarifa za Ufisadi Jamii Forums ,Mmemnyanganya simu yake.. Mmemweka Lock Up ( Selo) Siku tatu

Nasema kwa Sauti kubwa mrudishieni Eng Tarimo simu yake kabla sijaandika waraka wa wazi kwa IGP .. Msidhani IGP wambura ni Kama Siro. IGP Wambura hapendi unyanyasaji… Hapendi Uonevu

Kituo cha Polisi Arusha hacheni kufanya kazi kama Askari wa kikoloni,
 
CAG futa kampuni ya Reliable Consultant katika orodha ya wakaguzi ,hakuna wanachofanya AUWSA wanakula Rushwa tuu.
 
Kama mradi unaenda na unafanya kazi hebu tuambie shida ipo wapi?!
Mradi wa Water Blending System Umesima, Kwa sasa wakazi wa Arusha wanakunywa Maji yenye Fluoride nyingi na Chumvi nyingi ambayo ni hatari kwa Afya ya Binadamu
 
AUWSA inatumia Pesa nyingi sana Kuzima hii Kashfa

Wametumia Tzs 98 Milion kumpeleka Arusha Mkurugenzi wa Habari maelezo Ndg Greyson Msigwa Arusha ili atulie

Wametumia tzs 67 Milion kumpeleka Arusha Balozi hewa wa Maji Msanii Mpoki

Waziri Aweso aliitisha kikao cha wafanyakazi wa AUWSA na kutisha watumishi kuwa wakae kimya kila mtu ale kulingana na urefu wa Kamba yake…alipoambiwa Maji yana Fluoride na Chumvi nyingi akajibu wapambae na hali zao… hii kauli inafaa kutolewa na Waziri kweli?

Eng Rwetabula ambaye ni mnufaika wa huu ufisadi kila Siku anatishia watumishi wa Mradi Mkubwa kuwa wakae kimya na anawadanganya atatoa No Objection … ENg Rweitaba ni mtu mdogo sana AFDB acha kuwatisha watumishi.. Tunajua ulifukuzwa Kuwa MD wa Mz… Narudia kaa kimya kabla atujafikisha taarifa zako AFDB

Nimacheeka…. Eng Rwetabula toa No Objection Subiri Ijumaa…Eng Rwetaibula toa No Objection subiri Ijumaa… huu ni Mwezi wa Sita sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…