Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,171
Reaction score
23,996
Wakati akiongea na shirika la habari ya Uingereza liitwalo Reuters, Mkurugenzi wa Kampuni ya Barrick Gold, Mark Bristow amesema Makontena ya Makinikia yaliyozuiwa na serikali ya Tanzania Bandarini Dar es Salaam yana thamani ya Dola za Kimarekani milioni 280 ambapo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania bilioni 647.

Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa wako mbioni kutekeleza makubaliano ya mkataba waliokubaliana na serikali ikiwa ni pamoja na kuilipa serikali ‘’kishika uchumba’’ cha thamani ya dola milioni 300.

‘’Tunavyoongea kwa sasa tumeanza mchakato wa kuyasafirisha Makinikia na baadaye tutailipa serikali ya Tanzania dola milioni 100’’, Mkurugenzi Mark Bristow alisema.

Alimalizia kwa kusema, ‘’Kwa sasa tuko mbioni kuanza tena uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu baada ya kuufunga kutokana na amri ya serikali kuzuia usafirishaji wa Makinikia’’.

Kwa mnaojua lugha ya Kiingereza mnaweza kusoma hapa:
 
Tuliambiwa na baadhi ya ‘’wataalam wa madini’’ nchini kuwa ule ni mchanga hauna thamani kama ambavyo serikali kupitia Rais Magufuli wanadai!

Ukweli umeanza kujitokeza kupitia kwa ''wenye mchanga''!

Ninazidi kuamini kuwa uongo hutumia lift kuwafikia walengwa lakini ukweli hutumia ngazi!

Inawezekana hata haya makadirio (estimate) ya Mkurugenzi wa Barrick niya chini kwa faida yake ya kibiashara!

Ikumbukwe Kamati ya Prof Mruma ilisema kuwa kwenye zile Kontena 277 kuna dhahabu ya USD 521.3mil, Copper ya Usd 10.6mil, Silver ya Usd 1.08mil, Iridium ya Usd 105mil, Iron ya 1.2mil, Ytterbium ya Usd 7.5mil, Beryllium ya 3.8mil, Tantalum ya Usd 1.3mil, Rhodium ya Usd 0.689mil, Lithium ya Usd 0.649mil, na Sulphur ya Usd 0.844mil.

Jumla kuu ya thamani ya madini yote kwenye zile kontena 277 walipata Usd 652.663 million.

Tuendelee kuusubiri ukweli!

''Uncle Magu'' ni king'ang'anizi kweli kweli!
 

..nadhani viongozi wanadanganya.

..hakuna mtu aliyesema ule ulikuwa mchanga sawa na unaochimbwa maeneo mengine.

..kwa uelewa na kumbukumbu zangu ule ulikuwa ukiitwa mchanga wenye dhahabu. baadaye ukapata jina jipya la makinikia.

..wakati mwingine VIONGOZI wanadanganya na kupotosha kitu ambacho siyo sahihi.
 
Mkuu barrick walikua wanasafirisha dhahab iliyochenjuliwa tayar wakiichanganya na makinikia ili kukimbia kodi,ndomana ishu ilibumburuka,ila kwa maana ya makinikia kama makinikia,ni ngum sana kukuta kiasi king hvyo cha dhahab

Ulikua ni mchezo mchafu walicheza barrick
 
Wauze tunuliwe Noah Zetu. Bahati nzuri nina watoto 7, mke house gal hivyo kwangu tutapaki Noah 10.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu;
Soma vizuri na uelewe maoni yangu!

Ni wapi nimesema huo ni mchanga kama mchanga wa kawaida?

Nimesem, ''Tuliambiwa na baadhi ya ‘’wataalam wa madini’’ nchini kuwa ule ni mchanga hauna thamani kama ambavyo serikali kupitia Rais Magufuli wanadai!
 

Mkuu usitulishe matango pori - kama viognozi wanadanganya - sasa Barrick walikubali uongo wa viongozi? Sasa tofauti zilitokea wapi kati ya Serikali na Barrick - kama viongozi wanadanganya??
 

Mkuu usitulishe matango pori - kama viognozi wanadanganya - sasa Barrick walikubali uongo wa viongozi? Sasa tofauti zilitokea wapi kati ya Serikali na Barrick - kama viongozi wanadanganya??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…