Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Mkuu barrick walikua wanasafirisha dhahab iliyochenjuliwa tayar wakiichanganya na makinikia ili kukimbia kodi,ndomana ishu ilibumburuka,ila kwa maana ya makinikia kama makinikia,ni ngum sana kukuta kiasi king hvyo cha dhahab

Ulikua ni mchezo mchafu walicheza barrick
Inawezekana unachokisema ni kweli!

Tatizo ni kuwa tuliambiwa na baadhi ya wanasiasa ambao ni ''wataalam wa madini'' kuwa hayo makontena ya mchanga hayana thamani kama ambavyo serikali/Rais Magufuli wanadai!
 
CC: Zitto , Lissu ujumbe uwafikie.
Sehemu ndogo tu ya kilichosemwa ni Professerio rubbish kina thamani ya Bilioni 600 na ushee za kitanzania.
Je kwa miaka yote waliyo safirishwa makontena ya rubbish yana thamani ya jumla shilingi ngapi?
 
Mkuu;
Soma vizuri na uelewe maoni yangu!

Ni wapi nimesema huo ni mchanga kama mchanga wa kawaida?

Nimesem, ''Tuliambiwa na baadhi ya ‘’wataalam wa madini’’ nchini kuwa ule ni mchanga hauna thamani kama ambavyo serikali kupitia Rais Magufuli wanadai!

..kasikilize hotuba ya DINGI utaelewa ninachosema.

..yeye ndiye aliyekuja na UONGO kwamba watu walikuwa wanadai kuwa ule ni mchanga usiokuwa na thamani.

..kwa muda mrefu watu wamekuwa wakihoji kuhusu thamani halisi ya mchanga wenye dhahabu au makinikia.

..Na ndiyo maana kulikuwepo na hoja ya kujenga SMELTER hapa nchini. Na hoja hiyo ilikuwepo tangu awamu ya nne, na huenda kabla ya hapo.

..Tunachosisitiza ni serikali kuwa na TAARIFA ZA UHAKIKA na kuacha udanganyifu au kuwajaza wananchi matumaini ya uongo.

..Serikali ilitoa ahadi kubwa-kubwa mwanzoni mwa suala hili. akini sasa hivi wamesalimu amri kwa barrick, na wanazungumza lugha za kutupooza na wameachana kabisa na ahadi walizokuwa wakitoa.
 
Maisha magumu.. Ajira akuna. Hata hizo huduma za jamii zinazotokana kwa kodi zetu wenyewe bado tunazilipita gharama kubwa ili kuzipata. Sasa nishangilie hizo pesa kwa misingi gani...
Maisha yatakuwa magumu kwako kwa sababu umekuwa ''Msukuma wa Dar''!

Rudi ''Usukumani'' angalau ukalime badala ya kuzamia dar!
 
Mkuu usitulishe matango pori - kama viognozi wanadanganya - sasa Barrick walikubali uongo wa viongozi? Sasa tofauti zilitokea wapi kati ya Serikali na Barrick - kama viongozi wanadanganya??
Nadhani huyo jamaa anajaribu kupambana na ukweli bila kujua kuwa ukweli haupuuzwi!
 
Back
Top Bottom