Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

..nadhani viongozi wanadanganya.

..hakuna mtu aliyesema ule ulikuwa mchanga sawa na unaochimbwa maeneo mengine.

..kwa uelewa na kumbukumbu zangu ule ulikuwa ukiitwa mchanga wenye dhahabu. baadaye ukapata jina jipya la makinikia.

..wakati mwingine VIONGOZI wanadanganya na kupotosha kitu ambacho siyo sahihi.
Wacha kuteleza wewe. Walikua wanasema ni mchanga wanaenda kukamua machicha ya mbege tu.
 
JokaKuu,
Nikisoma mawazo yako nafikia hitimisho kuwa unakuwa kama mtu anayepiga kelele zisizoeleweka!

Hueleweki hoja yako ni nini!

Hoja iliyopo mezani ni kuwa, Mkurugenzi wa Barrick Gold amesema thamani ya makinikia yaliyoko bandarini Dar ni dola milioni 280. Kwa mantiki hii, hoja yako ni nini? Unakataa au unakubali?
 
Nikisoma mawazo yako nafikia hitimisho kuwa unakuwa kama mtu anayepiga kelele zisizoeleweka!

Hueleweki hoja yako ni nini!

Hoja iliyopo mezani ni kuwa, Mkurugenzi wa Barrick Gold amesema thamani ya makinikia yaliyoko bandarini Dar ni dola milioni 280. Kwa mantiki hii, hoja yako ni nini? Unakataa au unakubali?

..unawasikiliza VIONGOZI au unasikiliza Barrick?
 
CC: Zitto , Lissu ujumbe uwafikie.
Sehemu ndogo tu ya kilichosemwa ni Professerio rubbish kina thamani ya Bilioni 600 na ushee za kitanzania.
Je kwa miaka yote waliyo safirishwa makontena ya rubbish yana thamani ya jumla shilingi ngapi?
Zitto,Lissu na wanasiasa wengine ndio waliowaleta Barrick/ACCACIA na kuingia na mikataba ya Kimangungo kuchimba Dhahabu na kuwapat makinikia wasafirishe bure?
Tuwe wakweli kuwa CCM/Serikali/Viongozi ndiyo tatizo hapa Tanzania na wanaanzisha tatizo na kulitatua ili wawaaminishe Watanzania kuwa ni wakombozi wetu dhidi ya mabeberu.
Tusiangalie tulikoangukia na badala yake tulikojikwaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zito hii kwake ni nyundo ya utosi na genge lake lisu



USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Lumumba kwa kweli wamejaa ma MBUMBUMBU.

Waliosema tunaibiwa ni kina Zito na wenzake, ninyi mliwasikiliza wenzenu wanasemaje mkawa mnaunga juhudi, na kuwaponda wapinzani.

Leo ukweli umebaonika mnajitia kusema kina Zito wameumbuka!!!

Kweli Lumumba wamejaa maMBUMBUMBU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MsemajiUkweli,
Zile trillions za ma Profesa Mruma na Ossoro zimefia wapi?

Tundu Lissu alisema ule ulikuwa upuuzi mkubwa akaitwa majina yote.. Sasa kiko wapi?
Tujifunze kusikiliza upande wa pili.. Tanzania ni moja..
Tumeufyata mikia ndani huku "Mabeberu"" wakicheka kuelekea bank
 
Gellangi,
Sawa tatizo viongozi wa CCM walio tangulia, kwa hivyo unaona ni vibaya Magufuli akijaribu kusahihisha makosa ya watangulizi kiasi cha kustahili kutukanwa yeye na wale maprofesa sababu tu wamesema ukweli uliotokana na uchunguzi wa kisayansi?

Tafiti inajibiwa kwa matusi kama alivyo fanya Lissu na kushabikiwa na Zitto?
Ukikuta mababu zako walikuwa wanafanya kosa flani kwa miongo mingi huwezi kubadili hali hiyo?
Hupaswi kujipongeza na kupongeza ulioshirikiana nao kuleta mabadiliko hayo?
 
MsemajiUkweli,
Mkuu kwa waliokimbia hisabati unaweza kudhani ni fedha nyingi sana. ila kwa sababu suala la makinikia halikuruhusu factbased public discussion bado hata likiisha halitakuwa na valuable lessons learned.

Mfano kwa Content ya madini waliyosemaga Acacia, tena wakatoa mafafanuo Public.
Kwa hicho kiasi ni sawa hata kwa hesabu za hao acacia na baada ya kukaguliwa na gov agencies.
Kwanza sio za siku moja, ni tangu zilipozuiwa (aggregate).
Pia Hapo hawajatoa gharama ya kuzalisha hizo products za kiasi hicho.

Hiyo figure kisiasa ni ya kushtusha ila kwa kurudi kwenye details unaweza kukuta mzungu kaongea lugha ileile aliyokuwa anasema na watafiti wakiserikali waliipinga.

tuzidi kujifunza kwa ukaribu zaidi ili tuone nani yuko sahihi.
 
Kwa hiyo hawa jamaa walikuwa wanajibebea tu.

Ina maana wale waliokuwepo kabla ya Mzee baba walikuwa wameridhika au walikuwa sehemu ya mpango?

Mwisho wa siku unabaki kujiuliza "hivi hawa jamaa walituonaje?" maana hii haina tofauti na Mtu kukuchapia Mkeo.
 
Back
Top Bottom