Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Sijui kama unajibu kulingana na hoja au unajibu kulingana na hisia?
Hatutaweza kufanya mjadala na wewe, tufanye hivi wewe upo sahihi mimi na tunaosifia jitihada za serikali kwenye sakata la madini hatupo sahihi.
Mwisho wa mjadala.
Huoni kuwa unajichanganya?Unasifiaje mambo kama hayo badala ya kuchukua hatua na kuhakikisha waliotuingiza kwenye hiyo mikataba wachunguzwe,ikibainika walifanya mchezo mchafu wafikishwe katika vyombo vya kisheria?
Kweli watu wetu wanaangamia kwa kukosa maarifa na uthubutu.Tuanaishi kwa kukariri Yale wanayotuambia wale tunaowaunga mkono bila kuwa na mawazo huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hizo ripoti ndizo zimekuwa msingi wa majadiliano na kufikia muafaka!

Unaweza kuziita kwa jina lolote upendavyo lakini ukweli wake ni kuwa Mkurugenzi wa Barrick Gold amesema thamani ya makontena yaliyoko bandarini Dar yana thamani ya dola milioni 280.

Unajua wamesafirisha makontena mangapi kabla ya haya kuzuiwa pale bandarini? Ukiyajua ndio utafahamu kama ripoti ya Prof Mruma na Ossoro ni proffessorial rubbish.

..Ni rubbish ndiyo maana imebidi tukubali usd 300 million badala ya usd 191 billion.

..zingekuwa siyo rubbish tungeweza kuzitumia kama USHAHIDI na kuwashitaki MIGA na wakatulipa usd 191 billion + riba.
 
Kwahiyo huyo jamaa kaamua kusema kweli?
Mkuu barrick walikua wanasafirisha dhahab iliyochenjuliwa tayar wakiichanganya na makinikia ili kukimbia kodi,ndomana ishu ilibumburuka,ila kwa maana ya makinikia kama makinikia,ni ngum sana kukuta kiasi king hvyo cha dhahab

Ulikua ni mchezo mchafu walicheza barrick

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MsemajiUkweli,
Kwa shehena ile:

Millioni 280 x miaka20 = Millioni 5600 au 5,600,000,000 USD na hapo ni behewa chache tu.
Shehena 10 tu ni dola billioni 56! Imagine that
56,000,000,000/7000 unapata NOAH 8,000,000 😂😂😂😂
Mkuu;
Tugange yajayo!

Ukifikiria sana unaweza kuugua kichwa!
 
Yalikuwa makontena mangapi?Wataalamu wetu waliokagua awali walisema yalikuwa na thamani gani?
 
MsemajiUkweli,
$100M now (kama watatoa that's which I doubt - nawajua sana wazungu)
$100M after 5 years
$100M after another 5 years.

nyie endeleeni tu kutenda dhambi ya kumdanganya ngosha wa watu!
Kilicho cha muhimu wameingia kwenye makubaliano kisheria kuwa watatoa bila kujali itachukua muda gani!
 
Huoni kuwa unajichanganya?Unasifiaje mambo kama hayo badala ya kuchukua hatua na kuhakikisha waliotuingiza kwenye hiyo mikataba wachunguzwe,ikibainika walifanya mchezo mchafu wafikishwe katika vyombo vya kisheria?
Kweli watu wetu wanaangamia kwa kukosa maarifa na uthubutu.Tuanaishi kwa kukariri Yale wanayotuambia wale tunaowaunga mkono bila kuwa na mawazo huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekujibu unachopenda kusikia bado unataka nini tena?
Hatutawea kujadiliana wewe na mimi tuna tofauti kubwa mno namna ya kuchanganua mambo.
Tuna uwezo tofauti wa uelewa baada ya kusoma au kusikia kitu (comprehension).
Mimi sio shabiki au kada wa chama chochote.
Mimi sina chuki binasi na mtu yeyote.
Mimi sivutwi na ukabila wowote na ndio maana namshabikia JPM ambae tofauti sana na kabila yangu, na nampinga mwansiasa flani maarufu na wenye nguvu sana anae weza kumtingisha JPM japo kuna ujirani wa makabila na asili zetu na huyo mwamba.

Kabla ya 2015 niliipenda CDM, sasa sipendi chama chochote ila namkubali JPM.
Mwaka huu 2020 naweza kujikuta nakipenda chama chochote kama kikileta sera mbadala na bora zaidi ya CCM, CDM, NCCR, CUF, na ACT.
 
Tuliambiwa na baadhi ya ‘’wataalam wa madini’’ nchini kuwa ule ni mchanga hauna thamani kama ambavyo serikali kupitia Rais Magufuli wanadai!

Ukweli umeanza kujitokeza kupitia kwa ''wenye mchanga''!

Ninazidi kuamini kuwa uongo hutumia lift kuwafikia walengwa lakini ukweli hutumia ngazi!

Inawezekana hata haya makadirio (estimate) ya Mkurugenzi wa Barrick niya chini kwa faida yake ya kibiashara!

Tuendelee kuusubiri ukweli!

JPM asilegeze kamba. Salama yetu kama nchi sio siasa za maji taka ambazo tulizoea kufanya. Na kulindana. Wezi wakubwa wa mali za Tanzania ndio walijinadi kama wazalendo wa kweli. Acha waumbuke. Soon or later hata hizo siasa walizozoea hawataweza kuzifanya tena
 
Back
Top Bottom