Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Na wapiga zumari wake
..nadhani viongozi wanadanganya.

..hakuna mtu aliyesema ule ulikuwa mchanga sawa na unaochimbwa maeneo mengine.

..kwa uelewa na kumbukumbu zangu ule ulikuwa ukiitwa mchanga wenye dhahabu. baadaye ukapata jina jipya la makinikia.

..wakati mwingine VIONGOZI wanadanganya na kupotosha kitu ambacho siyo sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hawa jamaa walikuwa wanajibebea tu.

Ina maana wale waliokuwepo kabla ya Mzee baba walikuwa wameridhika au walikuwa sehemu ya mpango?

Mwisho wa siku unabaki kujiuliza "hivi hawa jamaa walituonaje?" maana hii haina tofauti na Mtu kukuchapia Mkeo.
Kumbuka pia kufanya kosa ni sehemu ya kujifunza!

Tumejifunza kama Taifa na kinachofanyika kwa sasa ni kurekebisha makosa!
 
Nani amesema Tanzania sio moja? Hii statement inaonyesha inferiority complex! Wewe jenga tu hoja zako kama zina nguvu za hoja basi zitasimama!

Hizo trillions za ma Profesa Mruma na Ossoro zimefia kwenye majadiliano ambayo yamefikia mwafaka kwa kutiliana saini za makubaliano.

Msingi wa majadiliano yoyote ya maana unajengwa katika msingi wa mutual concessions and compromises.

Kama serikali ingetaka kuzipata hizo pesa basi ingeenda mahakamani ambako msingi wake ni take or lose.

Utauliza kwa nini serikali haikwenda mahakamani? Serikali haikwenda mahakamani kwa sababu ya hekima ya kisiasa. Ninaposema hekima za kisiasa nina maana kuwa, kesi kama hizi ambazo ni transnational litigation zinachukua muda mrefu sana kumalizika na kuna uwezekano mpaka muda wa awamu ya tano ungeisha bila hukumu ya kesi hiyo kutolewa.

Kilichofanyika ni concessions and compromises kwa pande zote.
Tanzania sio moja. You can take that to the bank
Ipo Tanzania ya mtu mmoja. Yeye nu Bunge na Mahakama. Ni Sultan anayefanya atakalo akishangiliwa na praise singers na walamba miguu.
Tanzania nyingine ni wengine wote waliobaki kati yao anawaita Wanyonge kama kitu cha sifa hivi.
 
MsemajiUkweli,
Mkuu kwa waliokimbia hisabati unaweza kudhani ni fedha nyingi sana. ila kwa sababu suala la makinikia halikuruhusu factbased public discussion bado hata likiisha halitakuwa na valuable lessons learned.

Mfano kwa Content ya madini waliyosemaga Acacia, tena wakatoa mafafanuo Public.
Kwa hicho kiasi ni sawa hata kwa hesabu za hao acacia na baada ya kukaguliwa na gov agencies.
Kwanza sio za siku moja, ni tangu zilipozuiwa (aggregate).
Pia Hapo hawajatoa gharama ya kuzalisha hizo products za kiasi hicho.

Hiyo figure kisiasa ni ya kushtusha ila kwa kurudi kwenye details unaweza kukuta mzungu kaongea lugha ileile aliyokuwa anasema na watafiti wakiserikali waliipinga.

tuzidi kujifunza kwa ukaribu zaidi ili tuone nani yuko sahihi.
mitale na midimu
Inawezekana unachokisema ni kweli!
 
..ukisikiliza hotuba ya Prof.Kabudi ni kwamba makubaliano haya yametokana na "hisani" na "huruma" ya mabeberu wa barrick.

..Prof.Kabudi anakiri kuwa alishindwa. Kuna wanasheria walikuwa wameweka msimamo.

..sasa hiyo maana yake ni kwamba serikali ilikuwa haina hoja zenye uzito wa kisheria dhidi ya accacia na barrick.

..CCM ndiyo waliotuingiza ktk hasara na fedheha hii. Wao ndiyo waliopitisha sheria mbaya za madini na nishati. Ni serikali za CCM ndizo zilizosaini mikataba mibovu ya kinyonyaji.

..Kwa miaka kadhaa CCM na mawakala wao walikuwa wakitetea mikataba mibovu ya madini.Walipaswa kuamka mapema na siyo miaka 20 baadae.
Waliambiwa mapema lakini ujuaji mwingi kumbe ujinga mtupu.
 
Karibu Wilayani Misungwi Mkuu.. hiyo ID isikutishe
Sasa kama uko misungi kwa nini usilime hata bustani ya mbogamboga ili kuondokana na ugumu wa maisha!

Acha kupoteza muda wako kwenya mitandao ya kijamii kama kweli una maisha magumu!
 
Sijui kama unajibu kulingana na hoja au unajibu kulingana na hisia?
Hatutaweza kufanya mjadala na wewe, tufanye hivi wewe upo sahihi mimi na tunaosifia jitihada za serikali kwenye sakata la madini hatupo sahihi.
Mwisho wa mjadala.
Kuna baadhi ya watu ni kuachana nao kwa sababu watakupotezea muda wako! Hawajui kama ni wajinga lakini kikubwa zaidi hata kuelewa unachokiandika kwao ni mtihani!
 
Hapa sioni jipya ila kwakuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu basi kampeni ndiyo hizo zimeshaanza kwa namna ya kuwapamba watu fulani na wengine kuwachafua.

Mikataba mibovu toka mwanzo ni nani walioingia ni akina Mh Zitto, Mh Lissu na watu wao? Au ni ccm na serikali yake kupitia kwa wagonga meza wao?? Tutakutana kwenye majukwaa wakati wa kampeni ukifika na siyo humu jamvini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati akiongea na shirika la habari ya Uingereza liitwalo Reuters, Mkurugenzi wa Kampuni ya Barrick Gold amesema Makontena ya Makinikia yaliyozuiwa na serikali ya Tanzania Bandarini Dar es Salaam yana thamani ya Dola za Kimarekani milioni 280 ambapo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania bilioni 647.

Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa wako mbioni kutekeleza makubaliano ya mkataba waliokubaliana na serikali ikiwa ni pamoja na kuilipa serikali ‘’kishika uchumba’’ cha thamani ya dola milioni 300.

‘’Tunavyoongea kwa sasa tumeanza mchakato wa kuyasafirisha Makinikia na baadaye tutailipa serikali ya Tanzania dola milioni 100’’, Mkurugenzi Mark Bristow alisema.

Alimalizia kwa kusema, ‘’Kwa sasa tuko mbioni kuanza tena uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu baada ya kuufunga kutokana na amri ya serikali kuzuia usafirishaji wa Makinikia’’.

Kwa mnaojua lugha ya Kiingereza mnaweza kusoma hapa:
Dollar milioni 280?
Si tuliambiwa thamani yake ni dollar bilioni 108? Iliko kokotolewa gari aina ya Noah kwa kila mtanzania?
Kweli kushangaa ruksa ila usisahau kuchanganya na yakwako ukiyaacha ya mbayuwayu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Tuchague viongozi wa Chama kingine chenye Sera na viongozi tofauti.
2. Tuandike Katiba ya Wananchi ili mikakati na vipaumbele vya maendeleo viwekwe sawa.
3. Tutafute haki,maridhiano na kuepuka visasi kama Taifa.
4. Tujenge nchi bila ubaguzi wa dini,kikabila,kikanda,kivyama na aina nyingine za ubaguzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
1) Usijenge hoja kijumla jumla! Ni viongozi gani na chama gani? Nisaidie kunitajia!
2) Kwani Katiba ya sasa sio ya wananchi?
3) Haki zinatafutwa mahakamani na ukifanya kisasi unapelekwa mahakamani kupewa haki yako!
4) Hakuna nchi isiyokuwa na ubaguzi hapa duniani labda nchi inayoitwa ''cloud cuckoo-land''.
 
Watoe basi kiasi fulani kijenge barabara ya geita- kahama kupitia kakola kwa kiwango cha lami nitawashukuru sana sana
Nadhani hiyo barabara Barrick wamesema watajenga na kuboresha zingine ili kujenga uhusiano wa karibu na jamii/watu wanaozunguka migodi!
 
Kuna jamaa mmoja aliwaita kina Mruma rubbish, wana muambia huu sio mchanga kama mchanga wetu wa Baharini, nyuso zenu mnazificha wapi mkisikia taarifa kama hizi? sasa hivi hao Wamekimbilia nje kupigania human rights,from politicians to human rights,hayo ni madhara ya kushindwa kukubali ukweli.
 
Yapo makontena mangapi? Si tuliambiwa kule kuna dhahabu tupu tena ya US dola bilioni 108
 
Ni hizo ripoti ndizo zimekuwa msingi wa majadiliano na kufikia muafaka!

Unaweza kuziita kwa jina lolote upendavyo lakini ukweli wake ni kuwa Mkurugenzi wa Barrick Gold amesema thamani ya makontena yaliyoko bandarini Dar yana thamani ya dola milioni 280.

Unajua wamesafirisha makontena mangapi kabla ya haya kuzuiwa pale bandarini? Ukiyajua ndio utafahamu kama ripoti ya Prof Mruma na Ossoro ni proffessorial rubbish.
Hela ndogo sana hiyo kwa nchi we dogo, usidanganyike na hizo figure, sisi tunaofanya analysis tuona tumepigwa tayari
 
Back
Top Bottom