Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

HAMNA KITU HAPO HIYO WAMEKADIRIA 260 TO 280 .TUTAIBIWA MPAKA TUKOME. HAKUNA CHA MAGUFURI WALA NANI
 
Hivi kuna mtu aliwahi kusema huo mchanga hauna dhahabu?

Ni mpumbavu gani angeuandaa na kuusafirisha mchanga usio na thamani ? Ukweli ni kuwa Serikali imekuja kukubaliana na madai ya Acacia kuwa average concentration of gold ndani ya mchanga ule ni 200 - 300 ppm (0.02 - 0. 03%) na Cu ni 1.5 - 2.5% kama ilovyooneshwa kwenye lab certificates za Acacia. Na siyo ule upuuzi uliotamkwa kuwa ni 90% gold. Kwa mwenye uelewa angejua wazi kuwa hakuna uwezekano hata wa kuwa 10% gold achilia mbali hiyo 90%.

Gold ni karibia ya 20 times of water gravity. Kitu ambacho kinafanya kama gold ingekuwa 90%, kusingekuwa hata na lorry la kubeba container kama hilo. Na wala hakuma container ambalo lingeweza kunyanyuliwa likiwa na uzito huo bila kupasuka.

Jambo jingine ni kuwa sarikali imekubaliana na madai ya Acacia kuwa kwa productions ya concentrates zilizopo Tanzania ni uneconomical kujenga plant ya recovery ya metals kutoka kwenye refractory ore.
 
Nimejikumbusha summary ya taarifa ya Kamati ya Prof Mruma iliyosema kuwa kwenye zile Kontena 277 kuna dhahabu ya USD 521.3mil, Copper ya Usd 10.6mil, Silver ya Usd 1.08mil, Iridium ya Usd 105mil, Iron ya 1.2mil, Ytterbium ya Usd 7.5mil, Beryllium ya 3.8mil, Tantalum ya Usd 1.3mil, Rhodium ya Usd 0.689mil, Lithium ya Usd 0.649mil, na Sulphur ya Usd 0.844mil. Jumla kuu ya thamani ya madini yote kwenye zile kontena 277 walipata Usd 652.663 million. Kimsingi kazi yao ilikuwa nzuri japokuwa haikuwa kwenye uhalisia sana. Hata hiyo inayotamkwa sasa ya Usd 280 ni makadirio tu, thamani halisi itajulikana baada ya kupembua makinikia hayo kwenye smelter au mnunuzi kufanya uchunguzi wake. Hivyo, si sahihi kwa sasa kuweka conclusion katika suala hilo.
 
Mkuu,
Naomba tukumbushane tafadhali;
Wataalam wa acacia walisema una thamani gani, serikali ilizuia kwa sababu thamani iliyotajwa wakati huo ni ndogo.
Kuna tofauti gani kati ya thamani ya kabla ya kuzuiwa na ya sasa?
 
hivi mtu akikulipa kishika uchumba si anataka kukuoa ?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu,
Naomba tukumbushane tafadhali;
Wataalam wa acacia walisema una thamani gani, serikali ilizuia kwa sababu thamani iliyotajwa wakati huo ni ndogo.
Kuna tofauti gani kati ya thamani ya kabla ya kuzuiwa na ya sasa?
Kamati ya Prof Mruma ilisema kuwa kwenye zile Kontena 277 kuna dhahabu ya USD 521.3mil, Copper ya Usd 10.6mil, Silver ya Usd 1.08mil, Iridium ya Usd 105mil, Iron ya 1.2mil, Ytterbium ya Usd 7.5mil, Beryllium ya 3.8mil, Tantalum ya Usd 1.3mil, Rhodium ya Usd 0.689mil, Lithium ya Usd 0.649mil, na Sulphur ya Usd 0.844mil.

Jumla kuu ya thamani ya madini yote kwenye zile kontena 277 walipata Usd 652.663 million.
 
Mark Bristow said $ 280 mil the value of all containers containing concentrates.. Am saying double that value..

So the real value will be around $ 560 mil..

Ila Mungu alimuumba Mh. Rais Magufuli kutuokoa aisee, kutoka utumwani Misri kwenda nchi ya ahadi kwa kweli.!!
 

 
Mkuu
Unazungumzia nn kwa taarifa ipi?

Unakumbuka vzr? Kuwa tuliambiwa huo mchanga ni mchanga kama michanga mingine? Haukuwa na thAmAni? Ila unalindw kwa mtutu na escort juu?

Unakumbuka jinsi pale bAndarin watendaji walivyo thibitishA juu ya uthamAn wake?

Sasa mtendAj mkuu kathibitishA ukwel wa maneno yA Rais kuwA MAKINIKIA yanathaman kubwa(wanawez kutofautiana thamani kutokAnA na utAfiti)

Ila mwisho wA siku thAmani yA makinikia ni kubwa..

Sasa hApA kunaushAhid kuwa Rais ni mkwel, na mengine ya kiwango cha mchanga ni ya kitAaluma, hvyo kwa mdA muafaka tutapatA thaman halisi..

UnAweza usimpende Rais kwA anAyoyafanyA na kwa sabb zako binafsi lkn ukwel the PRESIDOR yupo sahihi100%

B

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu

Fanya uchunguzi wa kitabibu, elim yako inaweza kukufanyA ukAwa -100%

KunAugonjwa unAitwa personselfish desses(kamA ntakuwa nimekosea nisamehe ilA hospitAl wanAupima)

Kachunguze huenda unatattzo hlo, mAanA dalili zake nmeziona kwenye andiko lako.... ikiwa si hvyo bAsi Account yako kunamtu alisign in akAkuandikiA...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anko Magu nakumbuka alisema makontena yale yana dhahabu kama malori 27 ya tani saba. Tukaambiwa kila mtanzania angekamata Noah yake....

Kwahiyo Noah ndo zimeogelea baharini
 
CCM ni ile ile.....

ndiyo iliyoamua makontena ya mchanga yasafirishwe
na ndiyo iliyogeuka na kusema uamuzi huo ulikuwa ni wa hovyo na wizi wa ajabu kutokea Tanzania tangu Uhuru...

na si ajabu kesho wakaja kusema uamuzi wa kuyazuia kankotena ulikuwa hamna mantiki kabisa...ulikuwa wa kifisadi..

CCM mnatuchanganya wananchi.
 
Mkuu,
Naomba tukumbushane tafadhali;
Wataalam wa acacia walisema una thamani gani, serikali ilizuia kwa sababu thamani iliyotajwa wakati huo ni ndogo.
Kuna tofauti gani kati ya thamani ya kabla ya kuzuiwa na ya sasa?
Swali zuri sana.

Hii taaifa sioni utofauti wowote na ile taarifa ya hao Acacia ya kuwa concentrates zilikuwa na thamani ya U$260m. Kwa sasa hata kama itakuwa $280, itakuwa ni kutokana na ongezeko la bei ya dhahabu kwa sasa.

Tunatafuta sifa hata ambazo hazipo. Hivi tukiishi kwa uhuru wa nafsi bila ya ushabiki, uwongo na unafiki, tunapungukiwa nini?
 
Ungekuwa umenisaidia sana kama ungeniambia ni lipi lisilo sahihi.

Lakini kwa faida yako tu, Duniani kote concentrates huwa na kiwango kati ya 200 - 300 ppm, ambayo ni sawa na 0.2 - 0.3%; sawa na 200 - 300g/t.

Kwanza hii ya kusema makonteina yale ni ya mchanga na baadaye kuita makinikia, ni sisi tulivyotafsiri neno Au-Cu-Ag concentrate. Kama report zote zilikuwa zinataja kuwa ni concentrate, hii ya kusema ni mchanga tu usio na kitu chochote cha thamani, ni nani aliyewahi kutamka? Kama ni mchanga tu, ulikuwa u asafirishwa kwenda kufanyiwa nini?

Ninachojua konteina zile zilikamatwa ili kutengeneza mazingira ya majadiliano juu ya kutengeneza mikataba mipya ya kibiashara. Ni mbinu ya kibiashara ya kutengeneza mazingira yanayoweza kilazimisha mazungumzo.

Ninachoweza kumsifu Rais ni ile dhamira yake. Hakufanya vile ili kujinufaisha yeye kama mtu binafsi bali ilikuwa ni kwaajili ya Taifa.
 
Maisha magumu.. Ajira akuna. Hata hizo huduma za jamii zinazotokana kwa kodi zetu wenyewe bado tunazilipita gharama kubwa ili kuzipata. Sasa nishangilie hizo pesa kwa misingi gani...
Ukilinganisha na wapi
 

Asante sana Mkuu,

Sasa hivi yatauzwa kwa bei gani?
Tofauti na iliyotajwa mwanzo ni kiasi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…