Mkurugenzi wa Green Acres Secondary School Aumbuka.

Mkurugenzi wa Green Acres Secondary School Aumbuka.

Tuwe wakweli kwa hilo la matokeo wala wasimtishe kwani hata mimi ofisini kwangu kuna vijana wanne wamekuja kuangalia matokeo na kukuta wamepewa points kwenye masomo ya Sayansi wakati hawakuyafanya. Hilo ni kweli wala si uongo.

tuwekee number zao hapa tuthibitishe, otherwise hata wewe hatutakuamini.
 
mama mdogo 1012?????

Samahani wasomaji, nimesahihisha!! Jamani hii ni kutokana na kuwa nimeandika nikiwa nimejawa na hasira nyingi kuhusu mfumo wetu wa Elimu, nilikuwa na maana ya 2012. Jamani tutamkumbuka Marehemu Makwetta na jinsi alivyofufua sekta ya Elimu wakati wa Mwl Nyerere.
 
Bujugo alizoea kufanya udanganyifu kwenye mitihani sasa amedhibitiwa kusawasawa na NECTA kwa hiyo ameamua kutoa uzushi wa hali ya juu kwani hakuna dosari yoyote na wala hakuna aliyepewa matokeo wakati hajafanya mtihani walimu wake walienda NECTA jana na wameumbuka na kufadhaishwa na uongo uliotolewa na mmiliki wa shule kwa vyombo vya habari
 
Tuwe wakweli kwa hilo la matokeo wala wasimtishe kwani hata mimi ofisini kwangu kuna vijana wanne wamekuja kuangalia matokeo na kukuta wamepewa points kwenye masomo ya Sayansi wakati hawakuyafanya. Hilo ni kweli wala si uongo.

hatusikilizi porojo zibitisha mkuu matokeo siyapo weka hapa.
 
Nimesikia tetesi kutoka Facebook kuwa katika matokeo ya kidato cha IV ya mwaka 2012, mwanafunzi Marehemu Alex katika Shule ya Sekondari Lubala iliyopo wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya apata DIV 4, wakati alifariki Aprili, 2012!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!

Nani hawajui hii ni vita dhidi ya Dr Ndalichako ang'oke baraza baada ya kuwadhibiti wezi wote wa mitihani hapo baraza.
 
Wadau nasisi tuache ushabiki. Kwani hiyo database ya NECTA si wao ndio wana uwezo wa kui-update? Tuna uhakika gani kama hakuna ujanja ujanja hapo? Hivi kweli mtu akurupuke tu na kuongea jambo kubwa namna hiyo?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
HAJAUMBUKA. Tumeumbuka tuliolipa ada 4 years halafu vijana wetu wanachanganyiwa matokeo. maana yake ni kwamba elimu yooooooooooooote ya Olevel imo ndani ya namba ya mtihani tu. no need to go to school.

kichwat unamaanisha marehemu nao wanafanya mtihani???? Kweli kina Mwigulu Nchemba tunao wengi sana
 
Last edited by a moderator:
Nimesikia tetesi kutoka Facebook kuwa katika matokeo ya kidato cha IV ya mwaka 2012, mwanafunzi Marehemu Alex katika Shule ya Sekondari Lubala iliyopo wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya apata DIV 4, wakati alifariki Aprili, 2012!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!

Tetesi haijengi tuhuma.........pata uhakika na urudi tena
 
Tatizo la wabongo tunapenda sana cheap popularity hata kwenye vitu visivyo na uhakika na huyo mkurugenzi lazima itakula kwake shame on you mkurugenzi
 
Tuwe wakweli kwa hilo la matokeo wala wasimtishe kwani hata mimi ofisini kwangu kuna vijana wanne wamekuja kuangalia matokeo na kukuta wamepewa points kwenye masomo ya Sayansi wakati hawakuyafanya. Hilo ni kweli wala si uongo.
Lete ushahidi usikurupuke, mimi jana nilikwenda ofisi za NECTA kwa masuala binafsi, nikakuta baadhi ya watahiniwa wamekwenda kudai madai hayo hayo, kilichotokea ni kwamba:
Kwa kuwa mwaka huu NECTA wametoa matokeo kwa kutumia namba za mitihani tu (Index Number) bila majina. Hivyo watahiniwa wenyewe walikuwa wamesahau namba walizofanyia mitihani hivyo walipokwenda kwenye NOTICE BOARD wakachukua matokeo ya aliyekuwa jirani yake, wengi waliondoka NECTA kimya kimya kwa aibu, sasa sijui nyinyi mnaoongea mitaani mmezipata wapi hizo habari. Nendeni NECTA mkapate ukweli.
 
lile Sakata la Islamic Knowledge lilitukanisha sana Waislaam na Uislaam, leo kibao kimegeuka ! Allah'u Akbar !
 
Hivi lakini, wana consent ya hawa wanafunzi kujadili matokeo yao hadaharani hivi?
Ni kuwaongezea watotot Trauma tu
 
Lakini haiingii akilini kwanini atoe tuhuma nzito namna vile kama sio kweli,mh mi naamini there is something wrong somewhere.Kama aliprint basi ndo salama yake kama hakuprint basi kaisha.
 
Wadau nimesoma kwenye thread inayosema Katibu Mtendaji it is time to go na mle ndalni nimeona kuna tangazo lilitolewa na NECTA la kukanusha madai ya Green Acres na wameweka mpaka saini za wanafunzi waliposaini wakati wa mtihani jamaa amechemka kweli aliyoyasema ni uongo mtupu
 
Nimesikia tetesi kutoka Facebook kuwa katika matokeo ya kidato cha IV ya mwaka 2012, mwanafunzi Marehemu Alex katika Shule ya Sekondari Lubala iliyopo wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya apata DIV 4, wakati alifariki Aprili, 2012!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!

angalia mama mdogo usije ukaolewa tena mara ya nne hyo alex unayemsema jina lake ni
ALEX ALICKO na namba yake ni 109 sasa fanya namna hii mcheki huyu S1645/0109 ndo hyo mtu unayemsemea ila kwa kuwa sasa ni zama za namba tu ndo kila mtu anadanganya
 
Nimesikia tetesi kutoka Facebook kuwa katika matokeo ya kidato cha IV ya mwaka 2012, mwanafunzi Marehemu Alex katika Shule ya Sekondari Lubala iliyopo wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya apata DIV 4, wakati alifariki Aprili, 2012!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!

Matokeo kidato cha nne ‘feki’

• Mkurugenzi Green Acres afichua siri nzito


WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.

Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.

Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.

Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.

Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alama za juu.

Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.

Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.

Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.

Hata waziri alipopigiwa simu pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.

Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.

na Betty Kangonga|Tanzania Daima


attachment.php

attachment.php


attachment.php

attachment.php

attachment.php


 
Back
Top Bottom