Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe asimamishwa kazi kupisha Uchunguzi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe asimamishwa kazi kupisha Uchunguzi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe (DED) mkoani Kigoma, Essau Ngoloka kupisha uchunguzi.

Mkurugenzi huyo amesimamishwa ikiwa ni siku chache zimepita tangu, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aeleze kutoridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Buhigwe.

Dk Mpango alisema anazo taarifa za baadhi ya miradi utekelezaji wake haufanani na fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi hiyo na kwamba hawezi kukubaliana na hali hiyo, ni lazima waliosababisha wawajibishwe.

Leo Jumanne Julai 11, 2023, taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tamisemi, Nteghenjwa Hoseah imeeleza Waziri Kairuki amechukua hatua hiyo baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti matumizi ya fedha ya miradi ya maendeleo.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari Kahimba ambayo ilipelekewa fedha Sh1 bilioni, hata hivyo mradi huo haujakamilika na fedha zote zimetumika.

“Kutokana na tuhuma hizo, Waziri Kairuki amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, kuunda timu ya uchunguzi ya matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Buhigwe na kuwasilisha taarifa kwake,” amesema Nteghenjwa

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kairuki amewataka wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za mitaa kote nchini kuendelea kusimamia vyema miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa utekelezaji wa miradi, zinakamilisha miradi husika kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha.

MWANANCHI
 
Jamani Magereza sio kuzuri, kwa nini hawa jamaa hawariziki na mishahara na vihela vya mitaani wanakula ela Mama? Huyu mtasikia ana kesi siku nyingi na hakuna mdhamana.
 
Sasa kama wakurugenzi wenyewe wanateuliwa kwa kigezo cha kuwa kada wa chama tawala, shida iko wapi wakiiba?

Maana hata hao wenyewe wanaolalamika hela kuibwa, wameingia madarakani kupitia wizi wa kura.
 
Back
Top Bottom