Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Janabi asema magonjwa ya moyo yataongezeka kutokana na ukuaji wa uchumi

Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Janabi asema magonjwa ya moyo yataongezeka kutokana na ukuaji wa uchumi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amesema magonjwa ya moyo yataongezeka zaidi kutokana na uchumi kukua kwa sababu maisha yanakuwa rahisi.

Prof Janabi ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam, wakati wa utoaji wa huduma za kijamii One stop Jawabu katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke.

Prof. Janabi amesema kuwa ukuaji wa uchumi unafanya maisha kuwa rahisi kwa watu kuwa na uwezo wa kununua vyakula vya aina tofauti lakini pia utumiaji wa usafiri wa mara kwa mara yote ni sababu ya ukuaji wa magonjwa ya moyo.

“Kadri uchumi unavyokua na watu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa hayo kwa sababu watu wanakuwa na fedha za kununua vyakula vingi sambamba na matumizi ya usafiri binafsi” amesema Prof Janabi.

Chanzo: EATV
 
Mkurugenzi huyo akiwa Temeke leo amesema kuwa anatarajia magonjwa ya moyo kuongezeka kutokana na uchumi wa nchi kukua kwani maisha yatakuwa rahisi hivyo watu watabweteka.

My take!
Mimi kwa upande wangu nimeshindwa kabisa kuelewa kama ni utani au amemaanisha alichoongea!
 
Angeainisha na hatua stahiki na jinsi gani walivyojipanga kuikabili hali hiyo.
Pale kwenye hiyo taasisi kama huna pesa za matibabu basi hali yako inazidi kuwa mbaya hata zaidi ya huo ugonjwa wa Moyo.
 
Watu wasio elewa watapinga hoja hii.

Kadri ya uchumi unavyoongezeka ndivyo watu hula junk foods kama za KFC na kuacha kula dona na bamia. Soda zitanywewa sana na energy drinks, flavoured foods, preserved foods kama nyama na samaki za kopo.
Unene utaongezeka.

Watu hawatatumia miguu kusafiri, mwendo mdogo tu ni gari au toyo kwa vile pesa ipo.
Kazi za nguvu zitapungua kwa vile watu wana pesa ya kutumia mashine na kuzifanyia automation. Wataweza afford kulipia kirikuu, bajaj, etc kubeba mizigo ambayo ingeamwishwa na njemba. Watanunua vyombo vya moto na kuvitumia popote.
Mazoezi yatapungua.

Na mengineyo.
 
Kwa huu uchumi wa kati tutegemee makuli kuugua cardiovascular diseases maana automation itakua kila pahala[emoji2][emoji2]
 
Sasa kweli uchumi ukue watu waumwee....labda mabarabara yajae mengii alafu mtu anaendesha gari kuwahi kazini wakati nyumbani hakuna chakulaa na mshahara mdogo apo ugonjwa wa moyo lazima utampata
 
Mkurugenzi huyo akiwa Temeke leo amesema kuwa anatarajia magonjwa ya moyo kuongezeka kutokana na uchumi wa nchi kukua kwani maisha yatakuwa rahisi hivyo watu watabweteka.

My take!
Mimi kwa upande wangu nimeshindwa kabisa kuelewa kama ni utani au amemaanisha alichoongea!
Anaunga mkono juhudi ambazo hazina uhalisia. Nchi hii watu wamekuwa waongowaongo tu. Nilidhani atasema magonjwa ya moyo yataongezeka kwasababu maisha yanatarajiwa kuwa magumu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijui kasomea wapi huyu

Yule ni prof mzee tena wa medical anaongelea kwenye uwanja wake

Sasa kwa sababu watu kama ninyi mpo wacha tukusaidie kitu iko hivi

Ukiwa na pesa na mambo yako mazuri utakuwa na gari kwahiyo mizunguko yako yote utatembelea matako tofauti na njaa kali amabaye anapuyanga tu kwa jua pia ni wachache wenye commitment ya mazoezi

Kingine ukiwa na pesa vyakula vya hovyo hovyo kama KFC ni rahisi zaidi kuvipata na ndo maeneo wanayotembelea wenye pesa nafikiri unajua vizuri kabisa vyakula madhara yake ni nini baada ya muda
 
Huyo doctor ametafakari kweli kabka ya kutoa hiyo statement.?
 
Uchumi gani uliokuwa? Huu wa kudhulumu Wafanyakazi, Wakulima na Wafanyabiashara? Atakuwa mwingine huyu aliyeokotwa jalalani.
Hivi Waliosema Kwamba Tanzania Sasa imeingia Uchumi wa Kati japo Ni Daraja la Chini Si ni World Bank (WB) na Bank Ya Maendeleo ya Africa (AFDB)

Sasa wao Wanaongopa ? Au Wamefika Bei ?? kama Sio hivyo kwanini Tukatae Kwamba Sisi Bado Maskini ??
 
Kama amemaanisha kwa kauli yake ilivyo basi inategemea na wanao mzunguka waka mtengenezea fikra tofauti.Wapo wanao zaliwa na hayo Matatizo ,wapo wanao yatengeneza kutokana na aina ya Maisha wanayo ishi.
 
Za kuambiwa changanya na zako Mkuu! Hizo namba walizotumia zimepikwa na BoT hivi huko Kitaa Watanzania walio wengi wanaonyesha wana maisha ya uchumi wa kati au uchumi wa chini kabisa!? Akili ni nywele hata mwenye kipara cha ukubwani ana zake.

Hivi Waliosema Kwamba Tanzania Sasa imeingia Uchumi wa Kati japo Ni Daraja la Chini Si ni World Bank (WB) na Bank Ya Maendeleo ya Africa (AFDB)

Sasa wao Wanaongopa ? Au Wamefika Bei ?? kama Sio hivyo kwanini Tukatae Kwamba Sisi Bado Maskini ??
 
Za kuambiwa changanya na zako Mkuu! Hizo namba walizotumia zimepikwa na BoT hivi huko Kitaa Watanzania walio wengi wanaonyesha wana maisha ya uchumi wa kati au uchumi wa chini kabisa!? Akili ni nywele hata mwenye kipara cha ukubwani ana zake.

Za kuambiwa changanya na zako Mkuu! Hizo namba walizotumia zimepikwa na BoT hivi huko Kitaa Watanzania walio wengi wanaonyesha wana maisha ya uchumi wa kati au uchumi wa chini kabisa!? Akili ni nywele hata mwenye kipara cha ukubwani ana zake.

"Methodologies – World Bank Data Help Desk" Methodologies – World Bank Data Help Desk

Kupitia hiyo Link utaona kuwa World Bank (WB) hawatumii Central Banks pekee kukusanya Taarifa pia Wana Official Sources Zao Hivyo Swala La Tanzania kuingia Uchumi wa Kati (Lower Middle) it's 100% True achilia Mbali AFDB

Nazichanganya mkuu
Binafsi Ni Mchunguzi Sana kwa Kipindi kirefu usajiri wa Magari umekua ukienda kasi Sana Namanisha Plate Numbers Mfano Hivi karibuni Tuu Usajiri Ulianza DU Yani T XXX DUA within a Month Namba zimefika DUJ Almost 8000Cars Maana Single Letter ina hold gari 898
So hao wanapata wapi hela ? Kwani Sio watanzania wa kawaida

Siku hizi nimeona Vijana wengi tukifungua Biashara ya Nguo Hivi kama ingekua hailipi kungekua na ongezeko hilo ?? Na Kama inalipa Means Watu si Wana hela Mpaka kufikia hatua ya kununua Luxury things

Pengine Ni kasumba tuu ndio iliyobaki ya kwamba Jiwe kabana Jiwe kabana
 
Back
Top Bottom