TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

MLIMAWANYOKA

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2019
Posts
631
Reaction score
2,247
Tumepokea taarifa ya ajali ya gari ndogo ambapo mmiliki wa Mabasi ya kampuni ya Sauli Luxury Solomoni Mwalabhila amefariki dunia kwenye ajali hiyo. Tunatoa pole sana kwa Kampuni ya Sauli Luxury.

Ajari ya barabarani imeondoka na roho ya mmiliki wa mabasi ya Sauli Luxury siyo mbali sana na ilipopata ajari basi yake mapema mwaka huu Kibaha na kuwaka moto na yeye pia mmiliki ajari imemwondoa maeneo ya Mlandizi leo hii asubuhi akiwa na gari binafsi

Atakumbukwa kwa kuleta upinzani wa huduma na kufikisha abiria kwa haraka kampuni zake kwa wasafri wa nyanda za juu kusini.

Hasa kwa sisi wanazi wa Scania tutamkumbuka sana mwamba kwa kuziheshimisha Scania road.

Rest in peace Mwilabila Sauli


IMG-20240804-WA0130.jpg
======

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Mwandishi wetu wa Pwani ameeleza kuwa ajali hiyo ilihusisha magari mawili yaliyokuwa katika sehemu moja gari namba T213 DQD aina ya Fuso.

Imeelezwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu ya kiufundi na kuligonga gari aina ya Jeep lenye namba za usajili T466EGW alilokuwemo mmiliki wa Sauli ambapo liligonga gari jingine aina ya Howo la kubebea kokoto.

Marehemu Sauli mkazi wa Mbeya alikuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka minne ambaye alipata michubuko na alipelekwa hospitali kabla ya kuruhusiwa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti kituo cha afya Mlandizi.

Sauli alikuwa mmiliki mabasi ya Sauli yaliyowahi kufanya safari za Dar Es Salaam - Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Azam TV

Pia, soma=> Wasifu wa Solomon Sauli Mwalabhila

IMG-20240804-WA0011.jpg
 
Duh hizi ajali hizi. Zinamaliza sana nguvu kazi.

Hatari sana aisee hizi ajali.

Ndio maana kuna ulazima wakuhatakisha hii SGR network na usafiri wa ndege uwe sasa rahisi na route ziwe nyingi na za mara kwa mara maeneo mengi.

Watanzania tunapoteza Sana maisha barabarani aisee, uzembe, Barabara zetu + hizi gari nyepesi za kijapani ndio hatari zaidi.
 
Back
Top Bottom