peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
mwananchi.co.tz
Moshi kujenga bweni la watoto wa kiume kukabiliana na ukatili
Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo akizungumzia ujenzi wa bweni la wavulana linalojengwa katika shule ya kutwa ya Msandaka iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kulikagua. Picha na Janeth Joseph
Muktasari:
Katika kukabiliana na matukio ya ukatili kwenye jamii, ikiwemo vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, imelazimika kujenga bweni la wanafunzi wa kiume katika shule ya kutwa ya Sekondari ya Msandaka iliyopo katika Kata ya Msaranga, Wilaya ya Moshi ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Moshi. Katika kukabiliana na matukio ya ukatili kwenye jamii, ikiwemo vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro imelazimika kujenga bweni la wanafunzi wa kiume katika shule ya kutwa ya Sekondari ya Msandaka iliyopo Kata ya Msaranga, Wilaya ya Moshi ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa bweni hilo, mkurugenzi wa manispaa hiyo, Mwajuma Nasombe amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kushamiri kwa matukio ya ukatili kwa watoto wa kiume.
“Hili bweni tumejenga makusudi kwa ajili ya kusaidia watoto wa kiume kwenye eneo letu, tukiangalia takwimu za ukatili kwa watoto wetu wa kiume, ukatili uko juu, kwa hiyo kupitia kamati ya fedha na mipango ya halmashauri, tukakubaliana tujenge bweni hili ili tuwe na uhakika wa kutengeneza baba bora baadaye,” amesemea Nasombe.
Bweni hilo ambalo ujenzi wake umeshaanza, linatarajiwa kukamilika Desemba 2024 ambapo litagharimu zaidi ya Sh150 milioni hadi kukamilika kwake na litakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.
Akizungumzia ujenzi wa bweni hilo, mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo amesema kujengwa kwa bweni la wavulana katika shule hiyo ni chachu ya kumlinda mtoto wa kiume kwa kuwa wamesahaulika katika jamii.
Tarimo amesema ujenzi wa bweni hilo, utapunguza matukio ya ukatili na unyanyapaa kwa watoto wa kiume kwa kuwa tayari jitihada za Serikali na taasisi za kimataifa za kumsaidia mtoto wa kike zimeshafanikiwa na hivyo mtoto wa kiume kusahaulika.
“Ukiangalia matukio mengi ya unyanyapaa yanayotokea hivi sasa dhidi ya watoto wa kiume madhara makubwa sio kwa mtoto wa kike kama ilivyo kwa mtoto wa kiume, kwa hiyo sisi tumekuwa wa kwanza kufanya hivyo, kuhakikisha watoto wetu wa kiume wanakula salama.
“Jitihada za kiserikali za ndani na za taasisi za kimataifa za kumsaidia mtoto wa kike zimeshafanikiwa kiasi kwamba kwenye jamii tunachokiona mtoto wa kiume amesahaulika, mtoto wa kike amewekewa mazingira mazuri sana, hivyo ujenzi wa bweni hili utasaidia kwa kiasi kikubwa kumsaidia mtoto wa kiume asikutane na madhila,” amesema Tarimo.
Tarimo amesema serikali imewekeza kwenye shule za wasichana kila mkoa, hivyo mtoto wa kike tayari ameshajengewa mazingira mazuri ya kumlinda na kwamba changamoto iliyopo kwa sasa ni kwa watoto wa kiume.
“Kwa hiyo, sisi tumechukua hatua sasa, kwamba tunapomlinda mtoto wa kike na mtoto wa kiume naye tumlinde, hivyo tunashukuru serikali yetu kwa kutoka fedha hizi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii ya maendeleo inayoendelea kwenye maeneo yetu,” amesema mbunge Tarimo.
Pamoja na mambo mengine, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo jimboni kwake ikiwemo shule ya sekondari Mawenzi ambayo serikali imetoa zaidi ya Sh234 milioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa tisa ambao ujenzi wake umekamilika.
Akiishukuru serikali wa niaba ya wananchi, diwani wa kata hiyo, Charles Lyimo amesema ujenzi wa bweni hilo utakuwa ni mwarobaini wa kukomesha matukio ya ukatili kwa watoto wa kiume ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda shuleni.
“Tunashukuru sana Serikali Kwa kuona umuhimu wa kujenga bweni hili hapa, maana shule hii iko mbali sana na makazi ya wannachi, kwa hiyo watoto wetu wa kiume walikuwa wakikumbana na matukio mengi ya ukatili huko njiani,” amesema diwani huyo.