Mkurugenzi wa shule ya UWCEA Moshi na viongozi wa mkoa wakanusha taarifa za kufungwa kwa shule hiyo

Mkurugenzi wa shule ya UWCEA Moshi na viongozi wa mkoa wakanusha taarifa za kufungwa kwa shule hiyo

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
IMG_20210121_195638.jpg

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kufungwa kwa shule ya International School Moshi (ISM) kwa madai ya mwanafunzi mmoja kukutwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Wakati uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro ukikanusha habari hizo, mkurugenzi wa shule hiyo, Anna Marsden mbele ya wanahabari leo Alhamisi Januari 21, 2021 ameomba radhi kutokana na kusambaa kwa taarifa kuwa shule imefungwa na kusimamisha masomo, akisema ukweli ni kwamba masomo yanaendelea kama kawaida.

Madai hayo chanzo chake ni taarifa za ndani kutoka katika shule hiyo zilizowekwa katika tovuti yake Januari 19,2021 akitaarifu juu ya kuwepo kwa mwanafunzi aliyethibitika kuwa na Covid-19.

Kwa mujibu wa maagizo ya Serikali, ni viongozi wanne tu wanaotoa taarifa za Corona ambao ni rais, waziri mkuu, waziri mwenye dhamana ya afya na msemaji mkuu wa Serikali.

Leo katika maelezo yake, Mghwira ameieleza Mwananchi Digital akiwa mkoani Tanga kwamba kiini cha mtafaruku ni watoto wawili wa familia moja ambao shule iliwahisi kuwa na Covid-19.

Amesema kutokana na hali hiyo na baada ya taarifa kusambaa katika mitandao wa kijamii, alimtuma msaidizi wake pamoja na ofisa elimu wa mkoa ili waende katika shule hiyo kufahamu nini kilitokea.
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Rajabu Kundya na meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu kwa nyakati tofauti wamekanusha uwepo wa mwanafunzi aliyeathirika na virusi hivyo vya Corona.

Kabla ya kuzungumza na wanahabari, mkuu huyo wa wilaya na maofisa wengine wa Serikali walikuwa na vikao vya faragha na uongozi wa shule hiyo, wakifuatilia taarifa hiyo ambayo iliibua mtafaruku nchini.

“Kwanza shule haikufungwa. Wanafunzi wanaendelea na masomo na vikundi vya mjadala kama kawaida. Kwenye chakula wamekaa pamoja na hakuna tuliyemuona amevaa barakoa. Kwa hiyo, hiyo peke yake ni ishara kwamba taarifa ile ilipotoshwa,” amesisitiza mkuu huyo wa wilaya na kusema shule hiyo iko makini kwa vile inapokea wanafunzi kutoka nchi mbalimbali duniani.

“Shule hii ni shule inayopokea wanafunzi kutoka nchi mbalimbali duniani na tatizo hili liko katika nchi nyingine nyingi zikiwemo hata jirani zetu hapa, wamekuwa makini pale ambapo mtoto anaoonekana anazo dalili.”

“Akionekana na dalili zinazoendana na tatizo hilo Covid-19, basi haraka zinachukuliwa hatua za tahadhari ili kuzuia kwa dalili hizo asiwaambukize wengine,” alisema mkuu huyo wa wilaya na kuongeza kuwa,” amesema.

Akifafanua zaidi amesema, “ndio sababu hata mtindo wa ufundishaji ukabadilika lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba kama anapatikana mtu mwenye tatizo hilo au jingine linaloweza kuambukiza anadhibitiwa ili tatizo hilo lisienee kwa wengine.”

“Ninachopenda kuwahakikishia watanzania ni kwamba shule haikufungwa iko salama. Wilaya ya Moshi iko salama, mkoa wa Kilimanjaro uko salama na Tanzania iko salama bila Covid19.”


Kilichoandikwa kwenye tovuti
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, kampasi ya Moshi na Arusha zina jumla ya wanafunzi 600 kutoka mataifa 80 duniani huku kampasi ya Moshi pekee iliyoanzishwa miaka 51 iliyopita ikiwa na wanafunzi 300.

“Mwanafunzi wa darasa la M4 kampasi ya Moshi alithibitika kuwa na maambukizi ya Covid-19 Januari 18 (2021). Januari 19 mwanafunzi mwingine alionyesha dalili za Covid-19 ingawa alikuwa hajapimwa.”

“Kwa sababu hiyo, kampasi ya Moshi imesitisha kwa muda ufundishaji wa ana kwa ana na kuhamishia mafunzo yote kwa njia ya mtandao mpaka Februari 1, 2021. Taarifa kamili iko kwenye barua pepe ya mkurugenzi”

Taarifa hiyo ilifuatiwa na taarifa ya mkurugenzi wa shule hiyo, Anna Marsden katika tovuti hiyo akisema kutokana na tatizo hilo la Covid 19, kampasi ya Moshi ya ISM itakuwa katika karantini hadi Februari mosi, 2021.

“Wakati inabaki kuwa tuna mwanafunzi mmoja tu mwenye Covid-19, sasa tuna mwanafunzi wa pili ambaye anaonyesha dalili ambazo zinaweza kuhusishwa na virusi vya corona,” amesema Anna katika taarifa hiyo.

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa wanafunzi wa kutwa watasoma kwa njia ya mtandao kutokea nyumbani na wale wa bweni watabaki katika mabweni yao na kwamba walimu wote watafanyia kazi wakitokea nyumbani.

“Kwa hiyo wageni waendelee kuja wakijua wanakuja mahali salama. Ningependa sana mitandao ya kijamii izingatie utaratibu wa nani ni msemaji wa tatizo gani ili wapate taarifa kutoka chanzo sahihi,” amesema.

Kundya alisema hiyo itaisaidia mitandao hiyo kutoa kutoa taarifa sahihi akieleza kuwa taarifa hizo za ISM zimeleta taharuki kubwa Moshi mjini lakini walipofuatilia wamekuta kilichoandikwa na hali halisi havifanani.
 
Chukua tahadhari COVID19 ipo Tanzania na inaua haraka sana.


Askofu Amani awataka mapadri, watawa kuchukua tahadhari ya corona​

Thursday January 21 2021​

Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Amani ametoa waraka akiwataka waumini kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maelezo kuwa ugonjwa huo bado upo na unayasumbua mataifa mbalimbali duniani.


By Mwandishi Wetu
More by this Author

IN SUMMARY​

  • Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Amani ametoa waraka akiwataka waumini kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maelezo kuwa ugonjwa huo bado upo na unayasumbua mataifa mbalimbali duniani.
Arusha. Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Amani ametoa waraka akiwataka waumini kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maelezo kuwa ugonjwa huo bado upo na unayasumbua mataifa mbalimbali duniani.

Katika waraka huo kwenda kwa mapadri, watawa na walei wa jimbo hilo aliouita ‘kutembea pekupeku juu ya mbigili’, amesema baada ya kutangazwa kuwa ugonjwa huo haupo nchini, watu wameacha kuchukua tahadhari.

"Maji ya kunawa mikono yameondolewa kanisani na mahala pengine yapo, lakini watu hawanawi tena kwa imani kwamba hakuna corona, ile tahadhali ya kujikinga wameiacha na bado wanashikana mikono,” amesema huku akigusia utaratibu wa utoaji sadaka na kukomunika.

Amesema mapadri na watawa walihimizwa kuwa waangalifu zaidi ili wasisababishe maambukizi miongoni mwao na wanaowahudumia, “ilihimizwa pia kuvaa barakoa kwenye vyombo vya usafiri wa watu wengi, sokoni, kwenye ibada na hospitali.”

"Kutokana na hali halisi inapaswa kujenga utamaduni na tabia mpya za kujinusuru kwa vingine kwa hakika tunatembea sasa pekupeku juu ya mbigiri, tutafakari hali halisi kwani mwenye macho haambiwi tazama,” amesisitiza.

Amebainisha kuwa lengo la waraka wake ni kumwalika kila mtu ajisimamie kwa usalama wake binafsi na kujali usalama wa wengine kwani Corona inatikisa ulimwengu, “na sisi tusijidanganye kiasi cha kutochukua tahadhari.”

"Tusimjaribu Mungu kwakufanya uzembe na afya zetu, Turejee tahadhari za kuzuia maambukizi bila kuwa na hofu, hakuna haja ya kufungiwa, tuendelee kusali na kuchukua tahadhali. Ukiona unawashwa kwenye koo, kukauka koo kikohozi kikavu, joto kubwa na kupumua kwa taabu haraka mwone daktari ili usaidiwe." alisema
 
Nanukuu:"Kwenye chakula wamekaa pamoja na hakuna tuliyemuona amevaa barakoa"

Nashangaa sana,hivi inawezekana vipi kiongozi mmoja mwendawazimu na Juha ambae ameingia madarakani kwa kuiba kura afanye watu wote kuwa wajinga na wapumbavu?!Tanzania kuna kitu hakiko sawa!
 
Ukweli ni kuwa Corona ipo hapo Moshi International School, na shule imefungwa. Kuna mpwa wangu anasoma kwenye hiyo shule na jana jioni amerejea Dar akitokea moshi.

Kilichofanyika ni funika Kombe ili mwanaharamu apite.
Du! Kwahio tunadanganywa?
 
Ukweli ni kuwa Corona ipo hapo Moshi International School, na shule imefungwa. Kuna mpwa wangu anasoma kwenye hiyo shule na jana jioni amerejea Dar akitokea moshi.

Kilichofanyika ni funika Kombe ili mwanaharamu apite.
Ngoja imtafune mmoja hapo kwenye top layer naona ndo akili itawajia na ku-declare uwepo wa tatizo!!!
 
Chukua tahadhari COVID19 ipo Tanzania na inaua haraka sana.
Askofu Amani awataka mapadri, watawa kuchukua tahadhari ya corona...

Mbona wewe ujafa au inauwa ndugu zako? Mkuu pole sana
 
Ukweli ni kuwa Corona ipo hapo Moshi International School, na shule imefungwa. Kuna mpwa wangu anasoma kwenye hiyo shule na jana jioni amerejea Dar akitokea moshi.

Kilichofanyika ni funika Kombe ili mwanaharamu apite.
Tupe jina la mpwa wako huyo ambaye amerudi kwao Dar.
 
Kwa hiyo wale walevi taarifa wamezitoa wapi jaman[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Kunijua hunijui wapi umeniona nimekusanyika hovyo? Na ni nani aliyekudanganya kwamba mimi sivai mask? 😳😳😳
wewe ndio mpumbavu, unae sema covid IPO, wakati huo unakusanyika ovyo Na uvai maski
 
Madai hayo chanzo chake ni taarifa za ndani kutoka katika shule hiyo zilizowekwa katika tovuti yake Januari 19,2021 akitaarifu juu ya kuwepo kwa mwanafunzi aliyethibitika kuwa na Covid-19.
Ungeweka hicho screen shot ya kipande kutoka tovuti ingependeza.
 
Back
Top Bottom