...Hii inawezekana Tanzania tu.
...Kwanza TBC ilijinadi sana kwamba wao pekee ndio watakaooonyesha World Cup.
...Ghafla hapo katikati kukaingia suala la Decorder.
...WAO WENYEWE TBC wakatutoa wasiwasi kwamba TBC one ingeonyesha mpira na TBC two ingekuwa kwa ajili ya mfumo wa Digital.
...WAO WENYEWE TBC ndio walituhakikishia kuwa tungeona mpira kwa kutumia aerial zetu za 'chadema'
...Ghafla wao wenyewe TBC wakaanza kujikanyaga kanyaga huku kila mtangazaji akitupiwa swali kuhusu hili anamtumpia mpira mwingine!
...Ghafla WAO WENYEWE TBC wanatuambia kuwa hatuwezi kuona mpira bila kuwa na Decorder/Malipo ya shilingi 80,000/=
...Suala hapa sio watu kupenda Dezo. Suala ni kwa nini hawakusema mapema??
...Suala hapa ni kwamba hata hizo Decorder zao hata baadhi ya sehemu za mkoa wa Dar hazifiki sembuse Mikoani??
...Suala hapa ni makampuni ya Biashara ambayo yamtoa hela zao nyingi ili kutangaziwa biashara zao halafu mwisho wa siku matangazo ya biashara zao yanaishia kuonwa na ROBO tu ya watazaji watakaoangalia michuano hiyo kupitia Decorder za TBC zinazoishia Kibaha tu!!
...Suala hapa ni kwamba ingekuwa nchi nyingine makampuni haya yaliyolipia matangazo yangeweza kushitaki kwa vile yalilipia matangazo yao ili yaone na watu wengi inavyowezekana na sio ROBO ya watu kutokana na wengine kudhibitiwa na Decorder zisizofika hata Kibaha tu!
...Tatizo ni kuwa Makampuni haya yataogopa kufanya kile yanachopaswa kufanya ambacho si Pungufu ya kuondoa matangazo yao TBC na kuomba kurejeshewa Walicholipa kwa sababu TBC imevunja mkataba kwa kuwaahidi kuwa matangazo yao ya biashara waliyolipia bei kubwa tu yataonekana nchi nzima wakati ukweli sasa ni kwamba yataonekana kwa watu wachache sana!
...Suala hapa ni kwamba hatuna haja ya kutafuta wachawi na mafisadi wa maendeleo yetu kwa sababu katika hili, TBC wamejunga na kundi la Wachawi na mafisadi wanaokwamisha Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!!
...Suala hapa ni kwamba ili kulinda heshima yake na kuzuia kuonekana kwamba anshirikiana na Mafisadi kukwamisha ndoto ya kila Mtanzania kuwa na maisha Bora, Tido Mhando anatakiwa kujiuzulu huku akifarijika kuwa Waziri Mkuu wa Japan amejiuzulu wiki iliyopita kwa vile tu ameshindwa kuondoa kambi ya Jeshi ya Wamarekani kwenye Visiwa hivyo kama ALIVYOAHIDI!!
...Tido Mhando aliahidi kuwa Kila mtanzania mwenye Televisheni angeona Mechi Zote 64 za kombe la Dunia bila kulazimika kuwa na Decorder wala nini, anapogeuka na kutuambia kuwa hatuwezi kuona mechi hizo bila Decorder za Wachina zisizofika hata Kibaha tu, Anapaswa kujiuzulu!
...Tatizo ni kuwa hatuna Utamaduni huo!
...Tatizo ni kuwa Watanzania ni Kondoo!
...Tatizo ni kuwa kila Mtanzania ni Mbinafsi, Mradi yeye na watoto wake wana uwezo wa kununua Decorder wengine wote watajijua wenyewe!
...Tatizo ni mambo kama haya ndiyo yanayofanya tukwame tulipo maana tunagawanywa ili tutawaliwe vizuri.
...Hili linawezekana Tanzania tu.