Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera awaonya wasimamizi wa uchaguzi kuwa wataumbuka

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera awaonya wasimamizi wa uchaguzi kuwa wataumbuka

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Mahera amewaonya wasimamizi wa uchaguzi ambao wameficha barua za uteuzi za wagombea wa ubunge na udiwani ambao walishinda rufaa zao kwa sababu majina na picha zao zitakuwepo kwenye karatasi za wangombea halali wa uchaguzi.

Hivyo amewaangiza wasimamizi wa uchaguzi wakabidhi barua hizo kwa wagombea ili waendelee na kampeni kuomba ridhaa kwa wananchi kwa nafasi walizoomba.

Chanzo: Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku.

Swali: Je, Tume ya Uchaguzi haina mamlaka kamili ya kuwadhibiti na kuwasimamia wasimamizi wa uchaguzi?
 
Jambo la kushangaza sana hili. Siku zote alikuwa wapi kusema haya hadi leo hii zikiwa zimebaki siku 13? Hayajui majina ya hao wagombea na vyama vyao ili kuwasiliana nao kujua kama wamepewa barua husika? Na kama hawajapewa kuwachukulia hatua muafaka hao wahuni?
 
Back
Top Bottom