TANZIA Mkurugenzi wa Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (TASAC ) Mhandisi Japhet Loisimaye afariki dunia

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,935
Reaction score
3,346

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Utunzaji wa Mazingira ya Bahari (DMSE) Mhandisi Japhet L.Loisimaye kilichotokea Jana Jumapili, tarehe 10 Mei, 2020 jioni jijini Dar es salaam.

Shirika linatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa marafiki na watu wote walioguswa na msiba huu. Taarifa ya mazishi itatolewa kwa wafanyakazi wa Shirika mara baada ya kujulishwa na familia.

Bwana ametoa,Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania.
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

AMEN
 
Poleni wafiwa.

Kigogo atasema ni covid. Jamaaa mjuaji sana

komesha korona
 
Kama nchi jirani wanasoma hii misiba inayotufika, inaweza kuwaogopesha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…