Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, kwanini usijiuzulu?

Mkuu ukifika International Airports eg. Schiphol hawanaga huo muda. Kama haupo utajipanga. Nilishawahi kuachwa na ndege huko Schiphol nikiwa na boarding pass tayari.
NB: ndege inabeba watu 400 wakatafute mzigo wako wakaushushe kisa umecheck-in?
Ama watakutafuta abiria upande ndege au watashusha mzigo wako. Kwa ajili ya usalama wa abiria, hawawezi kurusha ndege na mzigo wa abiria ambaye hayumo kwenye ndege husika!
 
Fala kweli wewe🤣🤣🤣🤣
 
Ona baadhi ya Watanzania wasivyo makini! Mwanzisha uzi huu anazungumzia suala la maana wao wanaleta maneno ya upuuzi. Tukiita Uswahili wanasema tunatukana! Kwa hakika huduma kwenye ofisi nyingi za Umma si jambo la kujivunia. Ukiona Rais anajihusisha na kutangaza watalii waje Tanzania wakati Watanzania hatujafikia viwango vya kimataifa vya huduma ndipo unapomwonea huruma Rais wetu maana anafanya kazi bure. Watalii wanakuja Tanzania sababu ya wanyama na nchi yetu ilivyoumbwa na si kwa sababu ya huduma nzuri. Wengi wa hao watalii wakija Bongo mara moja hawaji tena na pia wanawaambia wenzao wasije kwa sababu ya maudhi ya huduma. Hapo hujazungumzia taxi services na taarifa zao za kumsaidia mtalii/mgeni hapa kwetu! Tukielewana hapo ndipo tutaanza na nini tuanze nacho ili tuweze kuwa na biashara yenye faida na ya kudumu.
 
Ni lini malalamiko Tanzania yameisha....??

Wakitekeleza yote, ikifika uchaguzi wataombea kura kitu gani.....

Serikali kazi yake ni kutengeneza matatizo na kuyatatua ili iendelee kubaki madarakani... Hzo TV walizotoa wakizirudisha utakuja kuona wana Lumumba wanakuja kusifia humu

Hovyo sana...
 
Nenda uone uchafu uliopo kwenye vyoo vya nje vya terminal two. Pale ndo lango la nchi. Kwa mtu aliyeweza kuingia vyoo vya Schippol Airport ya Uholanzi kwa ajili ya kujihifadhi utasikitika sana ukilinganisha na vyo vya JNNIA. Hii ni aibu kwa nchi.
 
Mkuu ukifika International Airports eg. Schiphol hawanaga huo muda. Kama haupo utajipanga. Nilishawahi kuachwa na ndege huko Schiphol nikiwa na boarding pass tayari.
NB: ndege inabeba watu 400 wakatafute mzigo wako wakaushushe kisa umecheck-in?
Uongo
 
Uko sahihi kabisa mkuu kwa huo mfano wa mwendokasi. Sasa hivi hata kuandika kuwa bus linakwenda wapi wameshindwa. Gari ikifika kituoni abiria wliopo wanaanza kukuliza abiria walioko ndani kuwa bus hili linakwenda wapi, au dereva anatoa kichwa nje na kuanza kuwaambia abiria walioko kituoni kuwa bus linaenda kivukoni au Gerezani. Kwenye vituo vingine wameandika sehemu za kusubiria bus za Muhimbili, Morocco na Kimara, ila vituo vingine hakuna bango lolote. Kimara terminal mabango hayaakisi ukweli.
 
Hii NCHI ndio maana yule MZEE alikuwa anatupeleka mchakamchaka, alijua wazi kuna SHIDA kubwa somewhere.

Leo kila kitu kimesimama kila sehemu shida watu wapo busy kutafuta MABAYA ya mzee MAZURI hayazungumzwi.
Ni kwa sababu mabaya yake ni mengi kuliko mazuri. Jiwe alikuwa muuaji.
 
Mkuu umeongea kwa uchungu sana, huu sasa ndiyo uzalendo.

Mamlaka husika kama mmepitia uzi huu chukueni hatua.

Ilifikia mahali eti mpaka vyeti vya Covid-19 navyo ni dili pale uwanjani.
Kuna siku mwaka jana mwishoni jamaa yangu kabisa anafanya hapo terminal 2 nilimwomba msaada wa kupata cheti cha yellow fever bila kudungwa sindano akataka nimpe 70,000/=,kwenda ofisini terminal 3 nikakipata kwa 30,000/= pia bila kudungwa sindano.
 
Tuhuma nyingi ulizozitoa sio za kweli,inawezekana huna taarifa sahihi ,biashara ya aviation ina standard zake sisi wabongo bado tumelala ndio maana ni nadra kuona mzungu ameachwa na ndege.
Kwa hiyo TV na Speaker za matangazo zinafanya kazi?
 
Kuna siku mwaka jana mwishoni jamaa yangu kabisa anafanya hapo terminal 2 nilimwomba msaada wa kupata cheti cha yellow fever bila kudungwa sindano akataka nimpe 70,000/=,kwenda ofisini terminal 3 nikakipata kwa 30,000/= pia bila kudungwa sindano.
Huna tofauti na hao wala rushwa unatakiwa kuwa jela wewe
 
Yule manager alikuwa rafiki wa jiwe ndie aliyempa nafasi nae akampa jiwe hela za kampeni so hakuna wa kumng'oa akitembelea mindset za jiwe.
 
Huna tofauti na hao wala rushwa unatakiwa kuwa jela wewe
Jera nikafanye nini? Yellow fever hakuna kwa nchi niliyokuwa nakwenda sasa nidungwe sindano ya nini?
Though rushwa siyo jambo jema
 
Yaani haitakiwi hata nukta ubao wa matangazo ya ndege uzime au uondolewe, ubao ndio dira ya abiria kujua time.
 
Aaah mkurugenzi umeua,palilia basi kibarua hata tv tu za matangazo unang'oa kwani mafungu hayaji.Mbona una vitega uchumi vingi tu parking,mabango ya matangazo,kodi za frem za maduka,nk.
Pili huduma zote zile pale kuanzia choo,wifi, haki ya matangazo,nk si abiria analipa kupitia makato ya nauli yake,so uoni huo ni wizi.
Au tegemeo lako ni yule karumanzila. Timiza wajibu wako ukuwekwa hapo kuuza sura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…