Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, kwanini usijiuzulu?

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, kwanini usijiuzulu?

Suala la utoaji huduma bora Tza bado Sana ndo maana watalii huwa awarudi japo tuna vivutio vingi sana.
Kuingiza watalii milioni 2 ni tusi kwa kweli ilitakiwa angalau milioni 10 kwa mwaka
 
Ipo haja ya serikali uendeshaji wa miradi na shughuli zote za uchumi zibinafsishwe waachie watu wenye kumudu fani zao.
Waarabu walichofanya ni kuwaachia wazungu waendeshe miradi yao mikubwa wao Kazi yao kupokea pesa tu maendeleo wameyaona.
Zipo kampuni binafsi nyingi tu zina mudu mambo ya management vizuri kabisa
 
Ukitaka kazi yako iharibike mpe mbongo afu jidai mstaarabu kwenye ufuatiliaji lazima akufurahishe.

December last yr T3 ofisa wa uhamiaji alikua kalala fofofo wakati watu tupo kwenye mstari mrefu, nilimpiga hadi picha bdae nikafuta.
 
Tuna tatizo la ustaarabu,fikra, utendaji wa kazi usio na rushwa, uwazi na uwajibikaji kama taifa.

Hata ukipanda pantoni, ukienda uwanjani kuangalia mpira, ukipanda basi utakutana na hali ya kinyaninyani.
 
Aaah mkurugenzi umeua,palilia basi kibarua hata tv tu za matangazo unang'oa kwani mafungu hayaji.Mbona una vitega uchumi vingi tu parking,mabango ya matangazo,kodi za frem za maduka,nk.
Pili huduma zote zile pale kuanzia choo,wifi, haki ya matangazo,nk si abiria analipa kupitia makato ya nauli yake,so uoni huo ni wizi.
Au tegemeo lako ni yule karumanzila. Timiza wajibu wako ukuwekwa hapo kuuza sura.
Hivi vitu hua vikiharibika tunajiuziaga wenyewe kisha tunasubiri mchakato wa kununua vingine vipya. TV ya Uwanja mkubwa kama wa JKNA haiwezi kua inaungwa ungwa na waya sijui kwa fundi nani.

Mabango, parking, vibanda sipokei Cash Mimi. Halafu ujue sisi mashirika ya umma hatununui tu TV unaenda kariakoo jion umerud na TV, lazima kuna michakato na vikao vyake ambavyo hutegemea na Bajeti iliyopitishwa.
 
Ugali unabidi ufanyiwe uchunguzi kuangalia kama unafaa kuliwa na binadamu...
 
utagundua issue nyingine ni altitude tu za watanzania wenyewe maana ni suala la mtu binafsi kujituma na kufanya kazi yake.... tatizo Ugali hapa...
 
Huku ni kuhamisha magoli, sioni mantiki ya uingizaji wa ccm hapa kwenye mada ya msingi kama hii. Mtoa mada ameeleza kwa ufasaha kabisa. Watanzania tuna shida vichwani mwetu sio bure.
Wewe ndiye unayeshangaza kama huoni uhusiano wa aliyoyaandika na CCM. Hebu piga akili kidogo, utaona uhusiano uliopo. Tena upo wazi kabisa.
 
Mimi mbona nipo hapa terminal 2 nilikua hapo nnje kuna screens za kutosha kuonyesha ndege za departure and arrival.

Pia naskia spika zote ziko vizuri mpaka chooni unasikia announcements

Nimefika kaunta za Precision air nimehudumiwa vyema kabisa kwa tabasamu .

Na ndege yangu kwenda kilimanjaro itachelewa kidogo na wametangaza kupitia PA speaker


TV mpya kabisa za kutoa burudani zipo .

Naskia ndege zingine zina announce abiria waliocheck in lakini hawajaja boarding gates.

Naona kila kitu kiko sawa hapa Julius Nyerere International Airport.

Ushauri wangu mtoa mada aache uongo na ufitini.
 
Anayepeswa kujiuzulu hapa ni waziri mkuu na si mtu mwingine yeyote.
 
Back
Top Bottom