Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore, amewakaribisha Watanzania kushiriki kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya VETA, yatakayofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 18 hadi Machi 21, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha kituo cha runinga cha TBC1, Machi 17, 2025, Kasore amesema maadhimisho haya ni fursa kwa Watanzania wa rika zote kujifunza kuhusu elimu ya ufundi stadi na nafasi zake katika maendeleo ya taifa.
"Tunawakaribisha wananchi wote, kuanzia waliomaliza darasa la saba hadi wenye Shahada ya Uzamivu (PhD), kwani hata waliomaliza shahada wanaweza kujiunga na VETA," amesema Kasore, akisisitiza kuwa wamewahi kuwa na mwanafunzi mwenye PhD aliyesomea uchomeleaji.