KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na mambo ya nje hapo jana, kudai kuwa baadhi ya wagombea wa Chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wameenguliwa bila sababu za Msingi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo.
Moja ya eneo ambalo Chadema walidai wagombea wao kuenguliwa bila ya sababu za Msingi, ni Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara na baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Maulid Seleiman Madeni Leo amejitokeza mbele ya waandishi wa Habari na kutolea ufafanunuzi Masai ya Chadema.
Moja ya sababu ambayo Mkurugenzi huyo ametaja, ni baadhi ya wagombea wa Chama hicho ambao walienguliwa walishindwa kukidhi vigezo ikiwemo kutojiandikisha katika Daftari la mkazi la wapiga kura.
" Moja ya sababu ya baadhi ya wagombea wa Chadema kuenguliwa, ni kwamba hawakujiandikisha kwenye Daftari la mkazi la wapiga kura, Chadema lazima wajue sababu za kwa nini watu wao wameenguliwa, wanatakiwa kuwa wanawafundisha kabla ya kuchukua fomu ili wasiharibu"