Pre GE2025 Mkutano Maalum wa Baraza la vyama vya siasa na wadau wa Demokrasia, January 4, 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimemumuona yule mwakilishi wa zamadamu mwenye miaka 100 anazungumzia reform!!! sielewi labda anataka kujibadili na kuwa binadamu wa kisasa
 
Mchangiaji anamlalamikia Wasira na Mwenyekiti.
Anawalalamikia kuwa hawajafanya genda balance. Anatoa malalamiko

Anasema nini watanzania wanahitaji. Watanzania wanahitaji matokeo ya 4R.
 
Mchangiaji
Thabit Mrangi. Mtaalam wa Geopolitics.
Nikweli mataifa makubwa yanapotaka kuwahujumu wanaangalia vitu vinavyowaungania na vitu vinavyowatenganinsha.

Kwenye katiba kuna chanzo cha cha uvumilivu. (udugu, Uhuru, Haki na amani)
Demokrasia yetu lazima iwe tofauti na nchi zingine. Lazima turidhiane baada ya hapo ndio twende kwenye reforms. Je, matatizo yetu tutaweza kutatulika kwa kutumia 4R. Moja wapo chanzo cha uvumilivu ni uhuru. Je, uhuru wetu unatundwajwe.

Lazima twende kwenye maridhiano
 
Joseph Selasini:
Kama alivyosema Wasira. Migogoro ilikuwepo tangu zamani. Lakini kikombe tulichonyweshwa mwaka 2015 hatutasahau. Rais amekuja na 4R.
Hapa tunabishana tuanze na kipi. Mimi naungana na mzee Wasira tuanze na Reconciliation. Nikiambia eti sote hapa tunaelewa 4R hainiingii akilini. Tumekuwa tunaatengenezewa slogan nyingi tu zinaishia kwa wasomi.

Je, niwatanzania wangapi wanaelewa? Wamesema Wasira mahali ambapo tunakosea ni tunadhani maridhiano kati ya chama na chama. Hakuna maridhiano ni ya wananchi siyo ya chama na chama.

Hizi 4R semina maalum itolewe.
 
Wanajopo wanapewa dakika moja kufunga mjadala.
Kiasi gani sasa tunahakikisha kila kundi halitaachwa nyuma? Nini itakuwa nafasi ya serikali katika hili, Asasi za kiraia, Asasi Binafsi nk.

Wataalam wa Chenge wanasema ukiwa na watu 60% wamekuelewa utafanikiwa
 
Mwalimu: Niliposema reforms siyo kwamba tuande na reforms. Nilisema Key iwe reforms. Huwezi kukibilia kwenye reforms wakati hamjajenga reconciliation. Neno niliotumia refroms ni key.

Ninakubaliana na wote kuwa 4R ni falsafa ambayo inatakiwa tuende nayo. NIjambo sahihi sana. Ili liweze kuwa regace kwa rais Samia Suluhu lazima tuone serikali kuwa wanafanya mambo ya 4R.

4R siyo mambo ya siasa tu. Ni namna ya maisha. Kila sehemu 4R inatakiwa.
Ingawa kwenye siasa ndio kunakuwa na ka mkwamo mkwamo kwa sababu za uchaguzi nk.
Lakini 4R siyo kwaajili ya siasa pekee ni katika mambo yote.
Mimi nadhani ni falsafa nzuri tunaweza kuiishi.
 
Wasira: Mimi nadhani tumefika pazuri. Serikali ifanye nini na vyombo vya habari.
Wote tuna wajibu. Nchi zingine wahariri wanakuwa na panel wanakaa na kuongea. Tofauti sana na zamani tulikuwa tunaenda kuongea na watu. Kwa sasa hivi vyombo vya habari vinaweza kueleza kwa undani zaidi.

Nafasi ya serikali ni haya yanayoendelea. Katika demokrasia, serikali iliunda kikosi kazi na wameanza kutekeleza.
Kuna kitu kinaitwa reform. Tutazame reform kwa mapana yake, mfano elimu haiwapeleki vijana kule wanakotakiwa kwenda. Serikali ina role, vyombo vya habari nk
 
Ado: Mimi ninahitimisha kwa nukta tatu. Kwanza Hoja yangu imeguswa na Mzee wasira. Kuhusu Uvumilivu. Mchakato wa katiba mpya halihitaji uvumilivu linatakiwa lianze sasa.

4R inaumuhimu mkubwa sana. Mh Rais anatakiwa kupongezwa kwahaya na haya yanayoendelea. Rais hakuwa na na shinikizo la kisiasa lakini aliamua mwenyewe tu. Aliamua kuanza na 4R.

4R itapimwa kwa vitendo. Kila mmoja atapimwa. Vyama vya siasa, Asasi za kraia. Kila mmoja. Sisi ACT wazarendo tulipitia mswada na tukaona mambo 10 ambayo tayari yalishapata mwafaka.

Hayo yote yameshapata mawazo
 
Mongella: Mimi nimekumbushwa kitu kimoja cha wa wajapan (5S za wajapan) ndizo ziliwafanya wawe hivyo.
Na hili nalo litakiwa tuliwekee mkakati wa 4R. Hapa hatujaelewa ndio maana kila mmoja anasema la kwake. Siyo ya mtu mmoja inakuwa ya Taifa. Tunaitoa mkononi mwa rais tunaibeba.

Unakimbia na falsafa unakimbia nayo, ndio uchawa mzuri. Kuwepo kikundi kitakachotutenegenezea 4R ziwe za mtazania.

Zinawezakwenda mpaka kwenye familia. Kuwepo na mwendelezo kufikish kwa kila mtu. Kila mtu ukimuuliza anajibu. Tusitupe. Tuvibebe.
 
Adoyo: Mimi ni mshukuru mwenyezi Mungu na wewe mwenyekiti.
Anaomba niweke sawa jambo moja. Niungane na Mzee Lipumba kuwa kulikuwa na vipindi maalum. Serikali tunaomba walichukue.

Kuhusu genda Rais aliomba kuongeza mwanamke mmoja mmoja mwanamke kutoka kila Chama cha Siasa.
Baraza linaenda kuweka kikatiba na siyo hisani ya msajili.

Mimi naomba tutumie 4R kwenye mjadala
 
Msisitizo mkubwa kwenye mjadala wa leo ni kuwa 4R ni nyezo itakayoweza kutufikisha kwenye maendeleo yanchi.

Silaha ni mazungumzo. Kusikiliza sauti za watanzania. Kuna vitu viwili. kushirikishwa na Kusikilizwa.
 
Makamo Mwenyekiti Bara au Zanzibar? Be specific gulu
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa anaongea..............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…