Mchaniaji Mwingine: Mussa Kombo
Mtumishi wa Serikali ya mapinduzi zanzibar tume ya kurekebisha sheria
Tusijikite sana katika mada ya jinsia pekee yake.
Niliupitia mswada wenye sheria mbili.
Nipongeze Serikali kwa kuwasilisha hiki na kusomwa mara ya kwanza katika bunge la jamhuri ya muungano Tanzania.
Asubuhi kuna mmoja aliniuliza kwanini tunazungumzia 4R wakati tunaongelea mswada wa sheria.
Nilimjibu kuwa tunaangalia msalah ya taifa kwanza.
Nitazungumza nukta 6 lakini nitaongea nukta 4 za ujumla.
Zanzibar tumeshiriki kwa kina. Na baadhi ya maoni yamezingatiwa
1. Suala la uzingatiwaji wa gharama za uchaguzi vyama vyote.
Katika utafiti niliofanya ni moja ya chanzo cha kuimarisha demokrasia. Kila chama kina falsafa zake. Lakini kwa kukosa fedha vyama vingine vinaweza kushindwa kuwafikia wananchi. Hili siyo jambo geni, limeandikwa kwenye nyaraka mbalimbali. Nimepitia sheria za nchi mbalimbali, wanajaribu kuwezesha vyama vya siasa. Nchi kama Afrika kusini wameweka asilimia kiasi fulani kwaajili ya kugharamia vyama vya siasa. Hiyo ni moja ya kujenga demokrasia. Ujenzi wa demokrasia ni gharama.
2. Tunayo sheria ndani ya Zanzibar inayohusu Gharama za uchaguzi. Inaonekana kama vile sheria hii inalenga kusaidia uchaguzi wa rais na wabunge wa muungana. Kwa mawazo yangu jambo la vyama vya siasa ni la muungano. Nadhani Sheria yetu ingetazama kwa ujumla wake. Nadhani hakukuwa na haja ya sheria ya uchaguzi inayohusu zanzibar pekee yake
3. Uwajibikaji. Mswada huu umegusa baddhi ya maeneo. Kila chama cha siasa kinakuwa na nyraka muhimu kuhusu masuala ya kijinsia. Tunaweza kila chama kikatengeneza nyaraka nzuri. Lakini sasa baada ya kutengeneza nyaraka hizo ikiwamo genda policy uwajibikaji wake ni upi. Tuwe na kifungu cha uwajibikaji
4. Kudhibiti kwa kiwango kikubwa rushwa ya ngono. Nimewahi kufanya utafiti sehemu moja. Kuwa kwanini wanawake hawashiriki kwa wingi. Jambo kubwa ni rushwa ya ngono.
Tofauti na mambo ya kisheria:-
1. Sheria hizi ni muhimu sana kwa wananchi. Wananchi hawana uelewa wa sheria. Nimuhimu sheria hizi zikaandikwa kwa lugha nyepesi. Ili kila mwananchi aweze kuzifahamu kwa wapesi. Popula version iweke kwa lugha nyepesi.
2. Huu mchakato ni mzuri umeshirikisha makundi yote. Napendekeza pia ufanyike Zanzibar
3. Kifungu cha 132 cha katiba ya Zanzibar. Kwa sasa kifungu hiki kipo. Ili kifungu kiweze kutumika zanzibar lazima ipelekwe baraza la wawakilishi. Baada ya kutiwa saini ipelekwe baraza la wawakilishi.