Mkutano Mkuu Simba

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Hizi timu zetu zina uongo uongo mwingi.
Simba walitangaza kuwa watapokea 4.5bil kwa mwaka kutoka M-BET kama main sponsor, ajabu kwenye kusoma Mapato ya Mwaka 22/23 M-BET anatoa 2.5bil

Ilitamkwa kuwa Vunjabei kama Main KIT sponsor atatoa 1bil kwa Mwaka ila leo imesomwa kuwa Vunjabei atatoa 750Mil.

A One Bottlers, watengenezaji wa Mo Xtra wanatoa 150mil.

Emirate Aluminium 100

Iweje MO Xtra awekwe kifuani afu atoe hela ndogo?
Kwanini Asiwekwe Begani kama Emirates?

Wachezaji wanalipwa mishahara ila wameandikiwa Bonus ya 800mil, kuwa wanalipwa kila mechi wanayocheza, kuna umuhimu gani wa bonus wakati wachezaji wanajua majukumu yao?
Kwamba kila mechi 20mil

Kuwa Maji ya Kunywa kwa ajili ya Kambi zote ni 150mil

Azam TV wanalipa 2.5bil kwa ajili ya haki za Matangazo

Bodi ya Ligi itawalipa 400mil


Bajeti haijatimia sababu mapato ni machache hivyo MO ameahidi kuwapa 3.9bil

Servicebya gari 26mil


Maswali yangu

1. Kwanini Club iwalipe wachezaji kwa kufanya kazi wanayopaswa ifanya? Kwanini bonus isiwe kwenye kutimiza lengo fulani? Mf Kuchukua Ligi kuu, Bonus iwe 200mil, Kufika Robo Final 300mil, Kufika Nusu 400mil, Kufika Final 500mil, kuchukua Kombe 800mil.

Ukiangalia hapo Club itakuwa yatoa Bonus kwa mafinikio fulani na hata ikitokea Wamechukua kombe bado Club itatumia 1bil kama Bonus

2. Hiyo service ya 26mil ni service gani? Maana bus lafanyiwa service na Mdhamini wa bus.

3. Hayo maji ya zaidi ya 100mil ni maji gani?

4.Kwanini Simba isijenge hostel ili ikwepe kulipa hizo milioni 400 kila mwaka?

5. Allowance ya 100mil kwa wachezaji wanapo safiri, hii ni sawa ila audit yahitajika.

6. Usajili wa 2bil+ Huu usajili ndo huu huu au kuna mwingine?

Pia soma: https://www.jamiiforums.com/threads...bu-ya-dimba-sc-kwa-kupata-kura-1-311.2061123/
 
Tulisha Sema mda mrefu M bet wanatoa 2.5 b Kwa mwaka lakini Kuna ma Mbumbumbu walikataa katakata.
Kitendo Cha kumleta Manzoki wakati usajili umesha pita ni jambo la fedheha si Kwa Simba tu ila inaonyesha jinsi kama Watanzamia tunavyo fikiri.
Ingekuwa kipindi Cha usajili ninge waelewa ila Kwa wakati huu ni fedheha kubwa.
Yaani Mimi ni Yanga lakini naona aibu, ningekuwa na uwezo ningezuia taarifa za Manzoki kuhusishwa na mkutano Mkuu zisiende kwenye mitandao ya kijamii.
Yaani taarifa hizo zibaki humuhumu.
 
Bonus ni kawaida mzee duniani kote; biashara ya mpira siyo kazi ya kufagia barabara za halmashauri ya Jiji Ilala, au Temeke wanaoongoza kwa Uchafu
 
kujibu swali lako la kwanza..... hebu kajifunze kwanza kuhusu motivation kisha uje tuendelee na majibu ya maswali mengine.
 
Ujanja ujanja mwingi
 
Leta matumizi na mapato ya Utopolo tokea GSM waichukue?Mapato ya jezi,wadhamini, bonasi,usajili na matumizi mengine.
Ndio utajua hujui.Timu imepokwa na GSM. Hersi yupo pale kulinda maslahi ya GSM. Amekuwa mwanachama wa Yanga miaka mingapi mpaka akateuliwa kuwa Rais wa Yanga bila mpinzani?Toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kuona ubanzi kwenye jicho la mwenzako.
 
Motivation kwenye kazi yako?
Motivation huja baada ya Mafanikio
Hujui hata unaandika nini?Motivation kama bonus wanapewa wakishinda au kutoa droo na hawapewi timu ikifungwa!
 
Kwenye mbet. Hiyo report iliyosomwa imeishia desemba 2022. Kwahiyo ametoa nusu. Nusu nyingine nia kuanzia januari mpaka mwezi wa 6 .
Kwahiyo subiri riport ya mwisho wa mwaka huu ndio utajua m bet ametoa sh ngapi
 
Kwenye mbet. Hiyo report iliyosomwa imeishia desemba 2022. Kwahiyo ametoa nusu. Nusu nyingine nia kuanzia januari mpaka mwezi wa 6 .
Kwahiyo subiri riport ya mwisho wa mwaka huu ndio utajua m bet ametoa sh ngapi
Tatizo hawa gongowazi hawajuii hata wanaandika nini?Ukiwauliza wao mapato na matumizi yao toka yule kibaraka wa GSM aingie hawajui.Kazi kukaza shingo na shughuli za Simba.Inferiority complex at its best.
 
Tatizo hawa gongowazi hawajuii hata wanaandika nini?Ukiwauliza wao mapato na matumizi yao toka yule kibaraka wa GSM aingie hawajui.Kazi kukaza shingo na shughuli za Simba.Inferiority complex at its best.
We jamaa huna akili, ukisikia 2022/23 unahisi nini?
 
Mbona kama ishu ya manzoki imewauma watu wa rangi ya nyoka
 
Reactions: Tui
Nimefuatilia kwa makini huu mkutano nikiwa kama mpenzi na mshabiki wa Simba nimeamini tunasafari ndefu sana kama nchi katika kila sekta mfano Taarifa ya mapato na Matumizi imesomwa lakini hamna hata mmja aliyeuliza swali..wagombea wote wamesema sera zao hamna ata 1 aliyezungumzia Bil 20 za Muwekezaji..Mo alionyesha Mfano wa Hundi na kusema ametoa na ziko Bank na Kuweka kama Tresury Bond..swali langu kama izo pesa ziko bank je zime mature mara ngap na Interest ya iyo pesa iko wapi? Na ni Bei gn kwa Mwezi Tunalipwa? Mbona hatujaskia katika taarifa ya Mapato na Matumizi juu ya faida ya Iyo pesa kuwekwa Bank?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…