Pre GE2025 Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025

Pre GE2025 Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Januari 13 na 16, 2025, mabaraza ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya vijana (Bavicha), wazee (Bazecha) na wanawake (Bawacha) yanafanya uchaguzi wa kupata viongozi wake, huku makundi mawili kwenye Uchaguzi ngazi ya Uenyekiti kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu yakitarajiwa kuibua mvutano mkali kuelekea Januari 21 siku ya Uchaguzi.
1736839350702.png
HELLEN KAYANZA ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU BAZECHA

Wajumbe wa Baraza la Wazee CHADEMA, wamemchagua Hellen Kayanza kuwa Katibu Mkuu wa baraza hilo (BAZECHA) kwa kura 115 akiwabwaga washindani wengine wawili.

Kabla ya matokeo hayo yaliyotangazwa mapema leo Jumanne Januari 14, 2025, Hellen alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa BAZECHA kwa upande wa Tanzania Bara.

MATOKEO BAZECHA

1. Suzane Lyimo —Mwenyekiti Taifa
2. ⁠Hellen Kayanza —Katibu Mkuu
3. ⁠Hamid Mfalingundi —Naibu Katibu Mkuu

Matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) ngazi ya Taifa

Mwenyekiti

01. DEOGRATIAS MAHINYILA - 204

02. HAMIS MAMBO MASUD - 112
03. SHIJA SAMWEL SHIBESHI - alijitoa

Makamu Mwenyekti Bara

01. JUMA MOHAMMED NG’ITU - 90 (28%)

03. NECTO KITIGA - 101 (31.7%)
04. NICE LAZARO SUMARI - 47 (14%)
05. VITUS RUTINWA NKUNA - 24 (7.5%)
06. MKOLLA A MASUD - 32 (10%)
  • Kutokana na matokeo kuonyesha hamna mgombea aliyefikisha asilimia 50+1, uchaguzi ukarudiwa kwa wagombea wawili;
01. JUMA MOHAMMED NG’ITU
02. NECTO KITIGA
  • Baada ya uchaguzi kurudiwa JUMA MOHAMMED NG’ITU akamuunga mkono mshindani wake NECTO KITIGA. Mwenyekiti wa uchaguzi akaitisha kura za ndio na hapana, NECTO KITIGA akashinda kwa kupata kura nyingi za ndio.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
  • Mgombea alikuwa mmoja, akapigia kuwa za ndio na hapana, akashinda ABDALLAH RASHID HAJI kwa kupata kura nyingi za ndio.
Matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) ngazi ya Taifa

Sharifa Suleiman
ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa kwa kura 222 (62%), akimshinda Celestine Simba aliyepata kura 139 (38%) baada ya uchaguzi kurudiwa kutokana na kutokuwa na mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Katika matokeo ya awali, Sharifa alipata kura 167, Celestine kura 116 na Suzan Kiwanga akiambulia kura 100.

Matokeo mzunguko wa kwanza:
  • Sharifa Suleiman - 164 (43%)
  • Suzan Kiwanga - 100 (26%)
  • Celestine Simba - 116 (30.4%)

Vilevile, Elizabeth Mwakimomo amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Bara kwa kura 212 (59%), akimshinda Salma Kasanzu aliyepata kura 147 (41%).

Katika matokeo ya awali, Elizabeth Mwakimomo alipata kura 157, Salma Kasanzu kura 95, kutokuwa na mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura uchaguzi ulirudiwa.

Matokeo ya jumla (round 2) Mwenyekiti Bara

1. Sharifa Suleiman - Kura: 222 (62%)
2. Celestine Simba - Kura 139 (38%)

Idadi ya wapiga kura mzunguko wa pili waliojisajili - 382
  • Kura zilizopigwa - 363
  • Kura halali - 361
  • Kura zilizoharibika 02

Makamu Mwenyekiti Bara

1. Elizabeth Mwakimomo - Kura: 212 (59%)
2. Salma Kasanzu - Kura 147 (41%)

Idadi ya wapiga kura mzunguko wa pili waliojisajili - 382
  • Kura zilizopigwa - 361
  • Kura halali - 359
  • Kura zilizoharibika 02

Makamu Mwenyekiti Zanzibar

Wagombea

1. Bahati Hadji - 212 (54%)

2. Zainab Bakar - 159 (42%)

Idadi ya wapiga kura waliojisajili - 382
  • Kura zilizopigwa - 382
  • Kura halali - 370
  • Kura zilizoharibika 12
Pia, Soma matukio yote kuhusu Uchaguzi Bavicha na Bazecha na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025;
 
Teamb Abdul juu
Hapa ndpo unoa kuwa watanzania bado sana...kama kuna mtu anamshabikia Lisu, ujue bado sana. Lisu ni mropokaji wa mambo with no evidence! Leta ushahidi wa AAbdul...hakuna, bado wanamuamini... Mara Mbowe kahongwa V8 mbili na serikali......docs hizo zikioneshwa zimenunuliwa kwenye mnada wa USA Embasy....Leo sigombei na Mbowe, kesho nagombea, mara nautaka urais.......
 
Samahani mkuu ni lini CHADEMA ilishatoa ushahidi wa LOWASA kuwa fisadi kuu na 1 badala yake iishangaza ulimwengu 2015 kuwa mgombea wake wa urais
 
Hapa ndpo unoa kuwa watanzania bado sana...kama kuna mtu anamshabikia Lisu, ujue bado sana. Lisu ni mropokaji wa mambo with no evidence! Leta ushahidi wa AAbdul...hakuna, bado wanamuamini... Mara Mbowe kahongwa V8 mbili na serikali......docs hizo zikioneshwa zimenunuliwa kwenye mnada wa USA Embasy....Leo sigombei na Mbowe, kesho nagombea, mara nautaka urais.......
Huzo hela za Abdul zimekutoeni akili sana wamachame
 
Back
Top Bottom