Januari 13 na 16, 2025, mabaraza ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya vijana (Bavicha), wazee (Bazecha) na wanawake (Bawacha) yanafanya uchaguzi wa kupata viongozi wake, huku makundi mawili kwenye Uchaguzi ngazi ya Uenyekiti kati ya
Freeman Mbowe na
Tundu Lissu yakitarajiwa kuibua mvutano mkali kuelekea Januari 21 siku ya Uchaguzi.
HELLEN KAYANZA ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU BAZECHA
Wajumbe wa Baraza la Wazee CHADEMA, wamemchagua Hellen Kayanza kuwa Katibu Mkuu wa baraza hilo (BAZECHA) kwa kura 115 akiwabwaga washindani wengine wawili.
Kabla ya matokeo hayo yaliyotangazwa mapema leo Jumanne Januari 14, 2025, Hellen alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa BAZECHA kwa upande wa Tanzania Bara.
MATOKEO BAZECHA
1. Suzane Lyimo —
Mwenyekiti Taifa
2. Hellen Kayanza —
Katibu Mkuu
3. Hamid Mfalingundi —
Naibu Katibu Mkuu
Matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) ngazi ya Taifa
Mwenyekiti
01. DEOGRATIAS MAHINYILA - 204
02. HAMIS MAMBO MASUD - 112
03. SHIJA SAMWEL SHIBESHI - alijitoa
Makamu Mwenyekti Bara
01. JUMA MOHAMMED NG’ITU - 90 (28%)
03. NECTO KITIGA - 101 (31.7)
04. NICE LAZARO SUMARI - 47 (14)
05. VITUS RUTINWA NKUNA - 24 (7.5)
06. 02 MKOLLA A MASUD - 32 (10)
- Kutokana na matokeo kuonyesha hamna mgombea aliyefikisha asilimia 50+1, uchaguzi ukarudiwa kwa wagombea wawili;
01. JUMA MOHAMMED NG’ITU
02. NECTO KITIGA
- Baada ya uchaguzi kurudiwa JUMA MOHAMMED NG’ITU akamuunga mkono mshindani wake NECTO KITIGA. Mwenyekiti wa uchaguzi akaitisha kura za ndio na hapana, NECTO KITIGA akashinda kwa kupata kura nyingi za ndio.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
- Mgombea alikuwa mmoja, akapigia kuwa za ndio na hapana, akashinda ABDALLAH RASHID HAJI kwa kupata kura nyingi za ndio.
Pia, Soma matukio yote kuhusu Uchaguzi Bavicha na Bazecha 2025: