Mkutano wa 90 wa Kimataifa wa Kazi unaofanyika mjini Geneva umetangaza Juni 12 kila mwaka kuwa "Siku ya Dunia dhidi ya Ajira kwa Mtoto", na kuzitaka nchi zote duniani kutoa kipaumbele kwa tatizo la utumikishwaji wa watoto na kuchukua hatua halisi na zenye ufanisi za kutatua tatizo hili.