ZAKAYO MATHIAS
New Member
- Nov 20, 2023
- 2
- 0
Ikumbukwe kuwa kabla ya ujio wa wakoloni katika bara la Afrika sisi tulikuwa wamoja kwa kushirikiana katika kila kitu kilicho husiana na Ubuntu wetu kwa kutokuwekeana mipaka katika bara letu. Kwa mfano wangoni chimbuko lao ni South Africa lakini walihama kutoka katika nchi yao kuja mpaka Tanganyika kwa kutafuta chakula, malisho na Mambo mengine kadha wa kadha bila hata passport Wala Visa kutoka nchi moja kwenda nyingine Leo hii au kizazi Cha sasa tunafurahi kuwa tuko huru tumetoka katika utumwa kumbe bado tunatawaliwa tu, Leo hii wajaluo wa Mara hawaonani Wala kukutana na wajaluo wa Kenya kwa sababu ya mipaka iliyowekwa na wakoloni kwenye mkutano wa Berlin, pia wangoni wa south Africa na wangoni wa Tanzania hawawezi onana Wala kukutana kwa sababu ya mipaka hii. Afrika tunatakiwa kuungana na kuondoa mipaka iliyotutenganisha na Mila na tamaduni zetu za kiafrika kwa maana Leo hii Kama Ni mtanzania huwezi kwenda kokote bila passport Wala Visa na wakati uko katika bara lako bila muungano hakutakuwa na ukuu wa Mwafrika Wala waafrika maana huwezi kuniita Mwafrika Kama hata bara lako tu hulijui umeshikiliwa sehemu moja mpaka unafariki dunia huna unachojua kuhusu Rwanda, Congo, Sudan, Nigeria na nchi nyingine za Afrika wazee wetu walikuwa na nguvu na umoja Kwa kuwa walikuwa na Ubuntu kwa mantiki hiyo sasa yatupasa turudishe ukuu wa Mwafrika kwa kuondoa mipaka ya ukoloni iliyowekwa katika mkutano wa Berlin pia kuwa na kiongozi mkuu wa kututetea katika bara letu la Afrika Kama ilivyo katika bara la marekani.
Upvote
4