Midomo michafu ya Tundu Lissu na Godbless Lema ikoje? Hebu thibitisha..
Lakini Kwa hakika kabisa, kama huwa humwelewi na ku - admire Tundu Lissu Kila anapojenga hoja zake, basi wewe
1000 digits ni mjinga kabisa.!
Tatizo lenu mmezoea kusikiliza politicians waongo waongo na wanaopenda kupaka rangi upepo.
Watu kama Tundu Lissu na Godbless Lema walishakataa ujinga huo.
##Kama kitu ni nyeupe, lazima useme ni nyeupe na siyo nyeusi.
##Kama u - bodaboda ni moja ya indicator ya umasikini na umasikini ni LAANA katika jamii, basi sema hivyo na siyo kusema "huo ni magawanyo wa majukumu"
##Sasa kama kuusema ukweli kama ulivyo ni
"kutotumia lugha ya hekima na busara" Kwa mtazamo na maoni yako, basi wewe ni mjinga na mnafiki mkubwa usiyestahili kusikilizwa!!
Tofautisha Hadhi ya nafasi ya urais na siasa za kijinga jinga. Lisu aligombea mpaka urais Kwa maana kwamba alitaka kuwa Rais.
Hakuna Rais Bora Tanzania kama Magufuli tangu kuumbwa Kwa kipande Cha Afrika hajawahi kutokea Mtawala Bora kama Magufuli.
Kilichomharibia JPM ni maneno yaliyopitiliza. JPM angekua anachuja maneno huenda hata lawama nyingine zisingemfikia na kimharibia Yale mema Mengi aliyoyafanya.
Wewe ni mwanasiasa wa Juzi na unawaza siasa za kishule shule au Chuo. Hii ni nchi kubwa sana. Huwezi kuwa na Kiongozi asiye na mipaka ya kuongea.
Huwezi kusema kuwa bodaboda ni biashara ya Laana kwenye majukwaa wakati wewe sio mhubiri wa dini Bali ni mwanasiasa ambaye una Upinzani wa Kisiasa mkubwa . Lema asiafikiri Jimbo la Arusha Kwa Sasa ni Jepesi. No. asahau kabisa lile Jimbo kulipata kirahisi. Hata pakiwa na Tume huru.
Saisa zikikosa ustarabu wanaoumia ni wapinzani sio Chama Tawala.
Hivi wale mabodaboda wakiamua kumpiga Lema mawe mitaani na kuvamia nyumba yake na kuchoma moto atawafanyaje?
Unataka siasa za kistarabu halafu unatukana watu.
Hivi Kwa hulka za kibinadami ukiona mtu ana sura mbaya Kwa mtu mwenye busara unaweza kumatamkia kuwa una sura mbaya na pakawa na utulivu tuu. ?
Kuna Vijana wengi wanaendesha maisha yao Kwa kutumia biashara ya Bodaboda.
Mtu ana mtaji wa Milioni Tatu unataka akajenge hoteli ya kitalii au afungue sheli ya mafuta kama Lake Oil!!
Acheni siasa za kitoto. Hazina tija Kwa nchi na Kwa Chama. Mbowe ana akili sana ndio maana anasoma upepo na Chama kinasonga mbele.
Hivi unafikiri CCM ni wajinga kutowaita Vijana wa bodaboda wajinga?
Hivi unadhani ingetokea Gambo akasema Vijana wa Arusha Wana. Laana ,atapata kura ??
Lengo la mwanasiasa ni kuingia mdarakani na sio kubwabwaja majukwaani tuu.
Chama kimekomaa kinapaswa kijiandae kushika madaraka na sio kubaki kuwa mtukanaji wa jamii eti nyeupe inaitwa nyeupe na nyeusi nyeusi. Mbona hawasemi wazi kuwa Mbowe alikiuka katiba ya Mwanzo ya Chadema na kuibadili ili Mwenyekiti asiwe na ukomo kwenye uongozi? Hii sio jambo la kusema wazi ? Kwa Nini ndani ya Chadema wanaosema wazi wanaitwa wasaliti? Jibu ni rahisi kuwa Kuna mambo kama mwanasiasa unatakiwa usiyaseme Kwa wazi mbele ya majukwaa au kwenye vyombo vya habari.
Mimi nineanza kupigia Upinzani kura Tangu mwaka 1995 na sijawahi kuichagua
CCM . Kosa la wapinzani ni kudharau kila anayekosoa Upinzani.
Hizi siasa za kishoga Toka Ulaya hazifai kuzibeba kama zilivyo. Hatuwezi kusema chochote bila kutafakari Kwa sababu ya uhuru wa kutoa Mawazo. Kwani angesema kuwa kuendesha bodaboda sio ajira ya uhakika asingeeleweka mpaka aseme ni ajira ya Laana . Kuna Vijana walianza na boda boda Moja Leo Wana bodaboda Kumi Kwa siku wanaingiza zaidi ya Elfu 70. Unamwitaje kuwa amelaaniwa mtu kama huyo.
Lema na marafiki zake wengi pale Arusha walitajirika Kwa Wizi wa madini,Ujambazi na kupora magari Kenya ,mauaji n.k. Je, hiyo ni ajira takatifu isiyo na laana ? Au Laana ni kukosa pesa nyingi za dhulma au kupata kidogo Kwa halali. ?
Laana ilikua ni biashara ya wizi ambayo Lema haisemi sana.