Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Aiseee, nasikia kizungu zungu zungu halafu nguvu zinaniishia, naomba nikafungulie halafu narudi.

Msanii naomba nishikie kiti tafadhali, mwendelee hadi nitakaporudi.

Ila usichakachue, kumbuka hatuzungumzii vyama. Tunaongelea Utaifa na Uzalendo. Maslahi ya taifa Mbele.
 
Sijamuelewa huyu jamaa ana zungumzia nini, bora unge andika kwa lugha moja kuliko hivi unavyo mix swahili na ki-English, fool!
mkuu Fool ndo umesign jina lako hapo mwishoni? kumbuka siyo vema kureveal your name.
 
Wewe hapo sijakuelewa mkuu, una changanya lugha. nakushauri siku nyingine tumia lugha moja kuwasilisha hoja yako utaeleweka vizuri.
 
Nashukuru kwa kuniona, ingawa naona DC anafaa zaidi kwa nafasi hii.
pole kwa mfungo. Tupo pamoja shekhe
 


Mwenyekiti anapokuwa mzushi sijui inakuwaje!
Mkuu ukiambiwa onyesha ni wapi lugha ya M... imetumika sijui utaonyesha nini kwa kweli.Naona hata huruma kukupeleka mahakamani maana nitakufilisi!
 
Mwenyekiti anapokuwa mzushi sijui inakuwaje!
Mkuu ukiambiwa onyesha ni wapi lugha ya M... imetumika sijui utaonyesha nini kwa kweli.Naona hata huruma kukupeleka mahakamani maana nitakufilisi!
Nimeyasaka katika thread hii sijayaona hayo matusi sijayaona labda ulimPM.

Haya turudi kwenye mada sasa. Lete hoja zako hapa
 
Wewe hapo sijakuelewa mkuu, una changanya lugha. nakushauri siku nyingine tumia lugha moja kuwasilisha hoja yako utaeleweka vizuri.

Nimekusoma. Ila uneonyesha hiyo sehemu niliyochakachua ingekuwa vema zaidi. Nitajirekebisha.

Ila matusi na Kejeli uachae. Nimemwambia Kova asikupeleke sello huko Central . . . Du! Au nimechakachua tena?
 
Mkuu Superman
karibu tena kwenye kiti. Amini nakuambia amani ilitawala
 
NIna swali hapa kwa mgombea wa nafasi ya juu kabisa......"Hivi huu uchakachuaji wa rasilimali za Watansanyia hasa Ardhi na Madini utaishi lini"? Ili wananji waweze kufaidika na rasilimali zao na sio hao walitutawala enzi kama wakoloni na leo wanarudi kama wawekezaji. Naomba jibu lenye utekelezaji sitaki longolongo
 
Mwenyekiti anapokuwa mzushi sijui inakuwaje!
Mkuu ukiambiwa onyesha ni wapi lugha ya M... imetumika sijui utaonyesha nini kwa kweli.Naona hata huruma kukupeleka mahakamani maana nitakufilisi!

Ndiyo WoS umenitukana sana, tena mbele ya kadamnasi ya wana JF na nikataka kujiuzulu kama hawalaani kitendo hicho, mpaka wakati huu hakuna iliyefanya hivi. Hii issue yako imejaa harufu ya rushwa:

Hebu angalia matusi yako:

Mwenyekiti..uteuzi huu ni batili..huna mamlaka ya kujipa ujiko wa uenyekiti..kwa msingi huo huwezi kuniteua.Teuzi hizi nazo zinafanya kazi nzima iwe batili

Umeona?

Uteuzi huu ni batili
Huna mamlaka
Unajipa ujiko wa uenyekiti
Huwezi kuniteua.
Teuzi hizi nazo zinafanya kazi nzima iwe batili

Nilikusihi sana matusi hayo ni makubwa sana na mimi ni kama baba yako lakini hukujali na bado ukatishia kunipeleka mahakamani.

Mpaka nikajiimbia wimbo wa "Najiweka pembeni, Naogopa Msongamano"
 
Mwenyekiti, hatimaye nimepata Ilani ya 2005 ambayo most of ahadiz zilitoka humo.
http://www.ccmtz.org/ilani/ilani.pdf
Wajumbe waisome waichambue kisha tuangalie ilivyotekelezwa au telekezwa ndipo tujitutumue kuhoji uhalali wa ahadi mpya za ilani iliyopo.
Naomba kutoa hoja
 
Mkuu Superman
Nimefanikiwa kwa ombi lako kusaka kwenye net na kukuta hii kitu itakayotuongoza kuchambua ahadi za Kikwete 2005. Nimeweka ilani kwanza kama walivyoiweka wenyewe kisha nasaka ahadi ambazo hazikuwekwa kwenye ilani

Mkuu nataka niwe na Uhakika, una maaana Agenda Kuu za JF 2010 ziwe hizi?

 

HII KALI! Wiki hii sijacheka kama nilivyocheka baada ya kusoma post ya mwenyekiti wangu wa mkutano!
Jamani...kiswahili chaenda kikiwa kigumu.Kama haya ni matusi ya nguoni, je yale yenyewe ya nguoni yatakuwa nini?
 
Aisee
kweli hiyo inampasa WOS kukuomba radhi walah.
Mwenyekiti rudi kwenye hoja uendeshe kikao
mie naenda kutabaruku kidogo, ugoro unaiita nje
 

Mkuu, tuko paamoja sana No.1 hadi 3 na tumeyakubali kimsingi.

Hayyo 3 ya mwisho unaweza kuyatolea ufafanuzi wa kina ili wana JF wayaelewe kwa uwazi zaidi?
 
Wiki hii sijacheka kama nilivyocheka baada ya kusoma post ya mwenyekiti wangu wa mkutano!
Jamani...kiswahili chaenda kikiwa kigumu.Kama haya ni matusi ya nguoni, je yale yenyewe ya nguoni yatakuwa nini?
WOS
mie nimecheka kuliko. ila ndo hivyo tena kama Mwenyewe kasema hizo ni tusiz za nguoni. dawa ni kusema sorry tu kisha tuendelee.
 
Mkuu Superman
karibu tena kwenye kiti. Amini nakuambia amani ilitawala

Asante sana Msanii, tuko pamoja. Kwa kuwa amani ilitawala, hii inatoa picha kuwa umekubalika. naomba tafadhali uendelee. Mimi niko hapa jukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…